Natafuta Ajira
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 14,421
- 40,936
Kuna mama fulani wa makamo anauza genge maeneo ya karibu na mtaani kwangu. Ni mama mcheshi kiasi. Huwa napita kununua matunda kwahiyo nimezoeana nae kidogo.
Wiki kadhaa zikizozipita, wikiend moja katika kutembea tembea mtaani kwangu kusalimiana na majirani. Nikafika gengeni kwake. Nikaagiza matunda. Wakati ananifungia kuna binti alitoka nyumba ya karibu akaelekea upande wa pili wa barabara. Nikamshangaa kidogo. Tukaanza mazungumzo sasa na mama muuza matunda.
Mimi: Huyu binti ni nani, anaishi hapa mtaani?
Mama: Ndio anaishi nyumba ile pale(akinionyesha kwa kidole). Amehamia juzi juzi tu hapa mtaani. Ni mwanafunzi kapanga chumba mule ndani. Kwanini unauliza? (huku akitabasamu)
Mimi: ni binti mrembo
Mama: ni binti mrembo sana, lakini ndio hajatulia
Mimi: unamaanisha nini?
Mama: unaona ile pikipiki imepaki pale nje, ni ya boyfriend wake aliempangia chumba pale. Ana mwanaume mwingine huwa anamletaga na gari. Kuna mwingine wa tatu huwa wanakutanaga mtaa wa pili uko. Hapo yupo mbio mbio si ajabu ndio anawahi kukutana nae.
Mimi: oooh.! ana maboyfriend watatu
Mama: unajua maisha ni magumu na yeye ni mwanafunzi. Anatakiwa kulipa kodi, usafiri, kula na mahitaji yake mengine. Ni hela nyingi na mwanaume mmoja anaweza kushindwa kumtimizia mahitaji yote hayo. Nafikiri mwenyewe unaelewa.
Mimi: inaonekana unakubaliana na huo mtindo wa maisha.
Mama: unataka afanye nini, na yeye ni mtoto wa kike yupo mbali na nyumbani.
Mimi: ungekua wewe kwenye nafasi yake ungefanya hivyo?
Mama: hapana hapana hapana. Sisi wakati wetu tulikua na maadili hata maisha hayakua magumu kama sasa. Tuliishi kijamaa unaweza ukaishiwa chumvi na kwenda kuomba kwa jirani ila sasa hivi kila kitu utoe hela, ndio inachangia hawa mabinti kuishi haya maisha
Mimi: na miaka ya mbeleni kuna kijana atakuja kumuoa akiwa hajui haya yote.
Mama: ndio maisha kijana wangu. Kipya kwa mtu ni kichakavu kwa mwingine.
Nikatasamu 😀😀 na kuchukua matunda yangu. Tukaagana
Siku nyingine nikakutana na demu mmoja hivi nikiwa kaunta, akanipa story jinsi yeye na rafiki wanapata hela za kujikimu na maisha.
Kwanza alitaka kuniuzia. Nikamwambia huwa sinunua sex. Napendelea mwanamke mwenye choice, sio ambae yupo tayari kulala na mwanaume yoyote akipewa hela. Akaniomba basi nimnunulie kinywaji. Nikamwambia agiza. Akavuta kiti kirefu akakaa.
Binti: Maisha yamekua magumu sana hapa nahitaji hela ya kumalizia ada ya chuo(akanitajia hela ya ada anayodaiwa).
Mimi: Hiyo ni hela nyingi. Uliwezaje kulipa ada mpaka ulipofikia sasa hivi?
Binti: Nilivyoanza chuo nilikua na mubaba. Alikua ananilipia ada na ananipa hela ya matumizi. Mwaka wa pili tuliachana. Aligundua nilikua na mpenzi wangu. Baada ya hapo maisha yamekua magumu sana. Wanaume kwa sasa hawana hela. Ngumu kupata wa kukupa mahitaji yako yote.
Mimi: sasa ilikuaje ukaanzisha mahusiano mengine wakati tayari una mwanaune anaekuhudumia mahitaji yako.
Binti: huyo mpenzi wangu nilikua nae tangu sijakutana na huyu mubaba, na nisingeweza kumuacha kwa sababu ndie ninaempenda.
Mimi: ooh.! Kwahiyo ukaushi vipi sasa baada ya hapo?
Binti: (anaanza kwa kucheka) kuna siku rafiki angu alinipigia kuniambia amepata hela ya kulipa ada. Nikamuuliza umepata sponsor wapi uko. Akaniambia hakuna mwanaume huyo sasa hivi. Huko alipo kumer inawaka moto. Amelazimika kulala na wanaume kadhaa ili apate hela
Nikatabasamu kidogo halafu akaendelea na story.
Binti: hali sio hali yaani sasa hivi inabidi tuanze tu kuwalenga mpaka nyie waume za watu.
Mimi: umejuaje kama mimi nimeoa?
Binti: huwa tunanusa.
Nikacheka kidogo na kuangalia muda kwenye saa ya mkononi then nikainuka kwenye kiti. Tukaagana. Nikalipa bill yangu na yake. Nikamwambia achukue chenchi atapanda bodaboda akiwa anaondoka. Nikasepa.