Baada yakumaliza chuo 2018, degree ya Mechanical engineering, nilipata internship kiwanda kimojawapo Cha bia mjini Dar es Salaam. Nikafanya kazi kwa miaka 2, Kwa posho ya laki 4 Kwa mwezi. Kisha baada yahapo 02/2020 nikapata kazi kwa makanjibai kiwanda kimojawapo Cha COSMETICS Kwa mshahara wa mil 1.2.
Sasa Mungu sio wa kanjibai, nimefanya Interview nakampuni Moja ya madini kutoka AUSTRALIA week 2 nyuma, Sasa wameniconferm jana, niende kituo cha kazi huko Geita ,mwezi ujao, hapa nilipo nahisi kama naota vile.
Naona siku kama haziendi niende nikalipoti, nahisi kama jamaa wanaweza ahirisha vile, nawaza namna gani maisha yangu yanaenda kubadilika, nawaza namna gani naenda kuitoa familia yangu kwenye umasikini baada yakufanya biashara ndogondogo nikiwa chuo, nahatimae baadae zikaja kuanguka. Nawaza miradi gani Nije nifanye hapo baadae, nawaza usafiri gani ntakuja kununua.
Nawaza zile haso zakwenda Dodoma Kila mara kwenye interview ndio zimeisha au, nawaza safari zakwenda nje ya nchi kwenye training mbalimbali kama walivyoniahidi.
Nawaza Dem wangu niliekua nampenda nakujitoa Kwa Kila kitu kwake ambae tulikua tunakaribiana mshahara yeye akiwa anapokea mil 1. Mie nikiwa napokea mil 1.2 alivyonipiga chini nakwenda kuolewa najamaa mwenye mwenye maisha mazuri kuliko Mimi, atanionaje nakile kigari Cha Jamaa yake kilichochoka choka.
Nawaza sana aisee hivi ndio naondoka kwenye kundi la MAKAPUKU au vipi?
Aisee wakuu tuendelee kumuomba Mungu Sana, maana hii kazi niloomba tu huko LINKEDIN bila kujuana na mtu yeyote.
Bado nawaza Sana na nahisi kama ndoto.
Wapiganaji wenzangu tusichoke tuendelee kupambana.