Miaka mitano ya hayati Magufuli, bei za nafaka hazikupanda namna hii. Sasa zimepanda na wananchi wanakula mlo mmoja na nusu

Na bado watu wanaambiwa wauze nje ya nchi wanavyojisikia.

Hapa tunakaribisha njaa.
Njaa itoke wapi? Wewe unaweza uza chakula chako chote ulicholima Ili upate njaa?

Maghala ya serikali yamejaa pomoni..

Ukitaka bei ya chini kalime
 
Naona unajisahaulisha,sukari,cement,mafuta nyie sindo.mlitibua?
 
Nchi hii imetekwa na WAHUNI wachache, na ndo wanaofaidi na utajiri wa Nchi hii.
Hawa wamemkalia Bibie kooni.
Watakachoamua wameamua. Hana ubavu wa kuwapinga.
Lakini kuna siku ukombozi utakuja kupatikana tu. Allah akbar.
 

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Hakuna mkulima anayepata faida, mnaopata faida ni nyinyi madalali na matapeli mnaompa mkulima bei ndogo na bado mnabana mizani, kujaza lumbesa na kununua mazao shambani aka. kangomba, hovyo kabisa....
Wamekubaliana bei kwa hiari yao. Usimpangie mtu kwa kuuza wala bei ya kuuza mali yake.
 
Jana nimenunua sembe kilo 5 shilingi 8,500/= na kuna watu wanashabikia mahindi yaendelee kupelekwa nje.
Mkuu tuache mwaka huu wakulima tufaidi. Huwa tukilalamika mbolea imepanda bei tunakosa mtetezi hata mmoja!
 
Samahani Mkuu, naomba nikurekebishe kidogo. Mwaka huu wakulima tumefaidika mno. Tena tunaishukuru sana Serikali yetu kwa kutozuia nafaka kuuzwa nje ya nchi.
 
Huyu dereva nchi imemshinda kabisa.watu wameanza kula mara moja tu kwa siku kutokana na vitu kupanda bei kiholela.Hadi tufike 2025 tutakuwa kila mwananchi amejikondea na kuonesha mbavu zake zote mwili mzima
Yakipanda bei mazao ya kilimo tu ndio mnalalamika. Mbona Mafuta ya Gari yamepanda karibu mara 3 hamlalamiki. Mtuache na sie Wakulima tufaudu kidogo.
 
Huu ni uhalisia mtupu ni bora nafaka zisivuke mipaka, Mama kasema ana tani 100,000 kwenye ghala la taifa, watag waliokaribu naye tafadhari apitie uzi huu.
 
Wakulima wetu ndiyo wakati wao wa kupata fedha na kuboresha maisha yao. Wewe badala ya kwenda kulima mahindi unakuja kuandika pumba JF.

Nenda na wewe ukalime halafu uone uchungu wa kuambiwa usiuze mahindi nje ya nchi.
law of demand and supply tumekalia ardhi miaka yote sasa soko la nafaka limepatikana dawa ni kuongeza uzalishaji tu
 
Wanaouza mahindi kwa gharama sio wakulima ni wafanya biashara so kama selikal inasema wakulima wauze bei watakayo uhalisia inakuwa inasema na wafanya biashara wa mazao
Kwani Mfanyabiashara ananunua kwa nani?
 
Mkulima kwanza,ebooh!! nyie wazururaji wa mjini mnataka mshibe ili iwaje? Muendelee kuchakaza lami mnazojengewa huko mjini kwa jasho la Mkulima?

Acheni unyonyaji mwacheni Mkulima anufaike, Magu aliwahi kusema "Serikali Haina Shamba" Sasa mnataka Serikali ifanyeje? Dunia ya kibepari hii, ukiona huuwezi mji nenda kalime usife njaa.

Sent from my Infinix X682B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…