TANZIA Michael Ngaleku Shirima mmiliki wa Precision Air afariki dunia

Sikupingi. Kimsingi nina mawazo kama yako. Ila mimi nilikuwa tu naelezea kwenye jamii za kimaskini kama zetu watu wanavyochukulia kila mwenye mafanikio! (wako haki kuwaza namna hiyo kwani ukiumwa na nyoka, kila uonapo ubua utashtuka). Kila ukweli ni kwamba siyo mara zote inakuwa hivyo!
 
Tuko pamoja mkuu. Kawaida huwa napenda kuwa mkweli na kukataa unafiki, ndio maana mzee Shirima nimesifia uwezo wake mkubwa kwenye kusimamia biashara ngumu sana. Ila uwezo binafsi pekee hauleti mtaji, na mtaji wa shirika la ndege hautoki kwenye kahawa na mbao.

Kuna probabilities kadhaa na bahati nyingi zinatakiwa kukaa kwenye mfumo kumfikisha mtu kwenye ubilionea. Kwanza most of them sio intelligent kivile, tafuta hotuba ya Mo Dewji akizungumza kwa dakika walau tano uone anavyozungumza na huyo ni mtu kasoma nje na ana exposure na uzoefu wa kuzungumza mbele ya watu. So hatuwezi wasingizia akili tu ndio zimefanya wawe vile, kama ni kufanya kazi kwa bidii uko ndio kabisa hatutakiwi kugusa kuna watu wanapiga kazi sana ila mifumo haijakubali.

Success requires inspiration, dedication and hard work in addition to lots of luck.
 
Bado nasubiri comment za masikini wenzangu za kujipa moyo utaskia "Hata matajiri wanakufa cha muhimu kuishi kwa upendo"
tutafute pesa huo ujinga hautusaidii
Lakini huo ndo ukweli bro, it's true wote tunapita tu tajiri au maskini
 
Kuna vitu unavyo aise,uko vzr
 
Yule mshamba kaiba sana pesa na kudhulumu watu majumba yeye na biswalo...mungu ni fundi kampiga kelbu moja tu akameza ulimi
 
Atakae elewa ulichoandika labda mlevi wa mataputapu
 
Unajua nguvu ya wenye majority share holders kwenye cooparate world?

Unachoongea wewe ni nadharia

Hao 58% watakuwaje majority share holder na siyo entity moja?
Kuna namna tofauti tofauti za to exercise power & control over kampuni .
Hizi namna huainishwa mapema kwenye memorandum.
Sio kila wakati mwenye share nyingi alpha na omega kwenye kampuni.

Kwa mfano: Kampuni au mtu anaweza kuwa na 10% ya total shares lakini kutokana na expertises na experience akawa ndiye alpha na omega kwenye voting yeyote, anapewa nguvu ya turufu.

Ownership arrangements za makampuni ziko nyingi, hii ya 50% and above ni simple ownership ambayo wengi tunajua ndio common.

Kwa mfano, shares owned by employees zinaweza kuwa entitled to gawio only not voting.
 
Rombo. Wakati jamii ikiomboleza kifo cha mwanzilishi na mwenyekiti wa bodi ya Kampuni ya Shirika la Precision Air, Michael Shirima, imeelezwa namna alivyothubutu kujiuzulu kazi na kwenda kuchoma nyama.

Shirima (80), mzaliwa wa Rombo mkoani Kilimanjaro, alifariki dunia Juni 9, wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa tangu Juni 8, mwaka huu.
Msemaji wa familia, Abdallah Singano alisema mwili wa Shirima utasafirishwa kutoka Dar es Salaam Jumatatu kwenda Arusha, utaagwa Jumanne na kusafirishwa kwenda Rombo kwenye maziko yatakayofanyika Jumatano.
Mbunge wa Rombo, Profesa Adolf Mkenda, akizungumzia maisha ya Shirima alisema ameacha historia nzuri kwa Taifa kwa kuwa alikuwa mtu asiyekata tamaa, licha ya changamoto alizopitia.
Profesa Mkenda ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, alisema kitabu alichoandika Shirima na kukizindua mwaka 2022 'On my father's wings' kinaelezea historia ya maisha yake na uamuzi mgumu aliochukua wa kujiuzulu Shirika la Ndege la Tanzania mwaka 1979.
"Niliwahi kumuuliza ni kwa nini aliacha kazi Air Tanzania, aliniletea barua zake kwa nini alitaka kujiuzulu na mpaka leo nina nakala yake, alivyoona shirika linayumba na kuwatahadharisha kwamba litakufa wakiendelea vivyo hivyo, hawakumsikiliza, hivyo akaamua kujiuzulu.
"Alipofika nyumbani mke wake alishtuka sana, lakini wakati huo walikuwa wanakaa nyumba ya Serikali, alikuwa hana kazi, ikabidi aondoke akatafute mahali pa kujishikiza yeye na familia yake, baadaye alianza kufanya biashara ya kuuza nyama choma kidogo kidogo,” alisema Mkenda.
“Alitafuta mkopo akaanza kununua mafuta ya pamba na alipata lori akaanza kuchukua mafuta kutoka Mwanza kuja kuuza Moshi. Wakati anafanya biashara hiyo akagundua Mwanza kuna ujenzi mwingi, lakini mbao zipo upande wa Moshi, akawa anachukua mbao Moshi na kupeleka Mwanza na kurudi na mafuta, alifanya kazi ngumu."
Alisema kwa kushirikiana na mtu mwingine aliyemtaja kwa jina la Kisinani walianza biashara ya kupeleka kahawa nje ya nchi na siku moja rafiki yake huyo alimwambia kuna mtu anahitaji ndege ndogo kwa ajili ya kufanya kazi shambani.
"Hivyo akaanza na ndege ndogo ya kukodi, baadaye akanunua nyingine, ndivyo alivyoendelea mpaka alipofikia leo," alisema Profesa Mkenda.
Alisema atamkumbuka Shirima kwa namna alivyokuwa mtu wa dini na hata alipofikwa na changamoto za biashara alikuwa akifunga novena siku tisa akiomba.
Rais aomboleza
Rais Samia Suluhu Hassan, kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter ameandika, “Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Michael Ngaleku Shirima, mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Precision Air.
“Baada ya utumishi wake kwa umma kwa zaidi ya miaka 30 amekuwa sehemu muhimu katika biashara ya anga na shughuli za kijamii katika nchi yetu. Natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki.” Mwenyezi Mungu amweke mahali pema. Amina.”

CREDIT: MWANANCHI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…