Watakuja kukupa muongozo ndio slogan ya smart, kila post anapita hatakama ya magumashi/Mwana hayupo kwa ajili ya kuponda, wala mengi kueleza/
Bali hum tag Mahondaw, na kuandika INAPENDEZA/
Hauna haja ya kutoka nduki, mkuu Injili ya Gheto/
Bali hakikisha hawainuki, wanao ku snitch na kufuata upepo/
wasivamie Tempo/ warudi Depo/ tukiwaona hatuna mchecheto/ kama tumemuona Mobetto/ Mvumbo sina mbeleko/ wananiogopa kama Meko/ Ukonga na Keko/ kote mpaka Soweto/
Rap imekupiga kanzu, ukiforce utaonekana kavu/Eti mnajifanya mnarap hivi nyinyi mnaijua rap? / rap tunafanya sisi kina nanii japo hatupati mshiko chap chap /
Mi ni boya hunikosi katika bahari ya rap, bila mimi hufiki popote hata kama mkononi una map/]Nyie wote maboya kama mnabisha njooni niwatie ndani ya kapu /
Uliyeanzisha uzi wewe ni kolo kama nanii anayeamini ili ufanikiwe lazima uende shule ukasome fasihi / au nakosea kama yule nanii aliyesema historia huwa haijurudii? / hahaha nacheka kifala kama mbwa alotokwa na manii.
By the way kuanzia ulipo si sawa na kubakia ulipo Nikise 'chini hapana' ina maana fanya unyanyuke / me ni mkushi zaidi yako ukichukia karibu nikupaushe.
African - Japanese
Kukopi sio mchongo bora umesema mapema, hii ni freestyle nawatakia battle njemaHakika umeanza vema, hivyo endeleza mkuu/
Ili wana wasije kusema, ume copy sehemu tuu/
Kidole kwa triger, nawakili ma niga/Unanifundisha nisnichi niwin bila ya jasho
Wakati mwenyewe umefeli na mwalimu mkuu mamaako
Kwanza naipokea tano, kisha naweka mkono juu kama Mandela/
Na lile swali la kwenye mabano, nalifungua zaidi ya umbrella/
Masela hatutoki, kwa sababu kenge wameunga tela/
Na pia tayari kimaisha tupo Konki, ya nini tuuze sura ndio tupate hela/
Hola hola hola!
Attention plz we nanii hii nayo unaiita rap au ngonjera za kina nanii? / acha niteme semi mpaka nukta kama nanii / nikiwapiga risasi za tenzi semeni maji kama braza nanii / mkifa mkabaki sita semeni basi kama mtemi mkwawa wananii /
Dan dana boyz mnataka kufanya mitundo huru na mimi nanii? / hahaha kaeni kando nisije nika spit fire words kama masihi / mawaki kama nyie hatuwashirikishi kwenye dili zetu za nanii / ulifikiri nini wewe nanii? Aaa nilikuwa namaanisha dili za kupiga puli nanii hahaha
Hii sio mada/ ya siasa au anasa/ ili watoto wachangie/
huwezi ona makada/ warembo wa kisasa/ wanataka za "njoo ubambie"/
Hakuna ada/ ila vipi wajaze kurasa/ lazima wakimbie/
Juu kama KISHADA/ Mvumbo nawanyanyasa/ ni vipi niwahurumie/
Nachoma dawa/ nakohoa nipo sawa/ wanapagawa wanaandika mashudu/
Hawana power/ nawanawa hawa chawa/ nawachinja kibudu/
Salute mkuuNakubali mwana, tuko pamoja kimtazamo hadi ki chama/
Man u huleta burudani, sio kama timu za mchangani/
Mpira dakika tisini, wapinzani tushawavua vimini/
Arsenal ilikua ile ya wenga, hii ya sasa haina tofauti na yanga/
Natoka ndukiii/Hauna haja ya kutoka nduki, mkuu Injili ya Gheto/
Bali hakikisha hawainuki, wanao ku snitch na kufuata upepo/
wasivamie Tempo/ warudi Depo/ tukiwaona hatuna mchecheto/ kama tumemuona Mobetto/ Mvumbo sina mbeleko/ wananiogopa kama Meko/ Ukonga na Keko/ kote mpaka Soweto/
Natoka ndukiii/
Kuwawahi wale washika bunduki feki/
Arsenane qudadaadekii/
Mashabiki wake wamenuna mwezi mzima hawacheki/
Unaanzaje kucheka wakati matokeo hupati/
Ndukiiii [emoji125][emoji125][emoji125]
Wana wanaflow kali kinoma wanatoa punch za maana [emoji23][emoji23][emoji23] rap battle hii [emoji119][emoji91]Utani ukipitiliza dharau huibuka, Mvumbo kaza acha kubabaika/
Nafurahi kuona hip hop inatangazwa jf, taarabu na bana pua ni zaidi ya kichefuchefu/
Hakika sina huruma nao, maana sioni wanachoimba/Hii sio mada ya vimada, au umbea kwa kina dada/
Piga chini ukuda jaribu kwenda na muda, mmenisikia nyie matozi wapaka poda?
Mvumbo usiwahurumie we wakanyagie, nakupa mistari uwapigie ukichoka niambie/
Mvumbo siku hizi silali, wachawi wananiita Bundi/Mvumbo usilale utavunda utakua mvundo, mc mwenye machale nadunda ndani ya tungo/
Wanga hamniwezi maana sikuizi nalala na nyundo, jikanyageni nyie washenzi muone navyozichana hizo nyungo/
Wezi kueni makini nyuma ya mlango nimeifadhi nondo, natoa rai mapema kabla sijashusha kipondo/
Nawapiga kwa mistari mlale vizuri vizuri, yaani kama lwakatale kwenye upepo wa kisulisuli/