Miezi hii miwili ni ya muhimu sana ili kupata maridhiano ya kisiasa

Miezi hii miwili ni ya muhimu sana ili kupata maridhiano ya kisiasa

my friends ladides and gentlemen,
ni muhimu zaidi kama Taifa la wazalendo kuendelea kuhakiki majina yetu kwenye dafatari la kudumu la wapiga kura ili hatimae tukamilishe maandalizi haya ya mwisho kuelekea uchaguzi mkuu wa kihistoria mapema october mwaka huu2025 :putinWalk:
Kuhakiki majina kwa ajili ya kumpigia kura nani wakati mfumo mzima wa upigaji kura ni mbovu na hao wanaotaka kupigiwa kura wapo tayari kushinda?

Kwanini fedha hizo za uchaguzi zisifanye kazi nyingine za kujenga taifa hao waliopo madarakani waendelee tu kuwepo hadi mabadiliko ya kanuni na utaratibu wa upigaji kura yafanyike kwani tumekuwa tukipiga kura miaka yote na hakuna mabadliliko ya kiutendaji.
 
Nchi imefika hapa ilipofika kwa sababu ya Magufuli, Kabla ya 2015 wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi wa Wilaya, Miji, majiiji hawakuwa hivi walivyo leo, Taasis za kusimamia haki zikaacha kutenda haki. professionalism kwenye kila kitu ikaondoka, Uchawa ikawa ndiyo sifa kuu ya mtu kuteuliwa katika nafas fulani. Uonevu ukazid, watu wakaanza kupotea na kuuawa. Bunge na mahakama vimejigeuza kuwa idara za serikali.

Tangu Ndugai na Tulia wamekalia kiti cha spika wa bunge, ni ajenda gan tangible inayomhusu mwananch wameruhusu ikajadiliwa?? au serikali imesimamiwa katika jambo gan?? zaidi sana wabunge wameguka wasifiaji wa mambo ya Rais, matokeo yake tumezalisha taifa la watu wa hovyo kabisa.

Namna pekee ya kutoka hapa ni kwanza Bunge na Mahakama vijitambue. vijue wajibu wao kwa wananchi, kwa sababu serikal isipomtendea haki mwanachi basi Bunge limtetee na mahakama impe haki yake.

Watu wanatekwa, Tulia hatak bunge lijadil na liweke maazimo maanae Tulia anataka watu waendelee kutekwa.

Watu wanapeleka kesi mahakamani wakipinga wakurugenzi kusimamia uchaguz lakini mahakama inaona ni sawa waendelee kusimamia.

Kama nchi tuna safar ndefu sana ya namna ya kutoka kwenye umagufulification.
Njia ya kutoka katika hali hii ni katiba MPYA isiyoegemea upande wowote. CCM wakubali katiba iliyopendekezwa na wananchi. Hata kama ikibidi,mchakato wa kupata katiba uanze na UCHAGUZI uahirishwe Kwa mwaka 1. Kwa kuwa walio na shine hawajali wenye njaa, hakuna jipya litakalotokea
 
Back
Top Bottom