Tetesi: Miezi michache tu mbele wapo watumishi wa umma watakaotoa pesa kwenye ATM machine huku wanatoa machozi.

Tetesi: Miezi michache tu mbele wapo watumishi wa umma watakaotoa pesa kwenye ATM machine huku wanatoa machozi.

Kama nilivyoandika uzi mwezi May 2017 "Msoto mwingine kwa watumishi waja" ndani yake nikaelezea kuwa watu wasitarajie ongezeko la mshahara mwezi Julai 2017 walionielewa walielewa.

Sasa nawaambia jambo lingine kuwa miezi si mingi kuanzia leo watumishi wa sekta fulani watatoa pesa za mshahara huku wanalia baada ya kulimwa pesa ili wafanane na wale wa serikali kuu.

Mi simo kwenye mjadala, nakaa pembeni.
Mkuu hebu ongezea nyama thread yako kaka....
1.lini zoezi litaanza?
2.Inawezekana kweli mshahara wa mtu ukapunguzwa?
3.Ni mashirika/Taasisi za umma ndo kuna mishahara mikubwa?
4.wanapunguza posho/au kukata mishahara kabisa?
5.Ni kiasi gani cha mshahara ambacho ni kikubwa kinatakiwa kupunguzwa kaka?
 
Itakuwa poa sana,hapo niko upande wa magufuli asee
 
nafikiri ni vyuo Na wakala wa serikali. Taasisi ziko nyingi hiz

Mkuu mishahara ya vyuo ni ya kawaida sana wala asikudanganye mtu. Hapo wanaozungumziwa ni TRA, TANROADS, BOT, TTCL, TANESCO na yanayofanana na hayo.
 
Hili ndilo linanifanya kuacha kazi sekta ya umma mapema sana February. Unaweza kupata kichaa bure
 
Watakuwa ni waalimu tu. Ndo wanaonyanyashwa sana inchi hii.

Hakuna mtu wa kuwanyanyasa walimu bali ni mishule ya ccm miaka minne yanalia uchaguzi ukifika yanapewa sukari na kanga kisha ya.asahau mateso ya nyuma miaka4

$wissme
 
Mshahara wa TRA sio mkubwa kama watu wanavyofikiria. Ukiwa na degree mshahara ni 850,000/=.
 
Mkuu hebu ongezea nyama thread yako kaka....
1.lini zoezi litaanza?
2.Inawezekana kweli mshahara wa mtu ukapunguzwa?
3.Ni mashirika/Taasisi za umma ndo kuna mishahara mikubwa?
4.wanapunguza posho/au kukata mishahara kabisa?
5.Ni kiasi gani cha mshahara ambacho ni kikubwa kinatakiwa kupunguzwa kaka?
Ndugu katika Mungu na katika Nyerere(baba wa taifa) haya maswali yako ni mazuri sana na yakijibiwa yote basi itakuwa si tetesi bali ni taarifa, si unajua jamaa zetu siku hizi wanakanusha mpaka jambo walilolinena hadharani.
Jela mbaya sana, wakili wa burebure Tundu Lisu wa kunitoa nje yuko Nairobi.
ahahahaaaaaaaaaa
 
KWA HILI MAGUFULI HEKOO BABAAAA, IWE HIVYO, NCHI HII NI YETU YOTE HAIWEZEKANIKI MWALIMU ALIPWE LAKI NNE NA MTU WA PSPF ,BANDARINI WALIPWE MILIONI MOJA NA MAPOSHOPOSHO KIBAOO, Kwahili likifanyika nitamuunga mkono Rais Wangu Magufuli kabisaa,
 
Nchi ni yetu sote, Kwa HILI nipo pamoja na Rais Magufuli ninampongeza sanaa.Mfanyakazi wa bandari elimu Yake ni diploma tu ,lakini analipwa mshahara mzito kuliko Mwalimu mwenye Digrii, MISHAHARA IANGALIWE UPYA KILA MMOJA TULIPWE SAWA KWA SAWA ,HEKOOO RAIS MAGUFULI
 
Watakuwa ni waalimu tu. Ndo wanaonyanyashwa sana inchi hii.
Walimu ni watumishi wa serikali kuu. Jamaa ameongelea watumishi wasio kuwa wa serikali kuu mfano TANESCO, TRA, TANROADS, NHC, ATCL, TRL, N.K.
 
Kodi siyo hivyo mnavyofikiri kwamba kuna vijana wengi wako mtaani. Wakiajiriwa itawachukua miaka kumi kuweza ku master kazi ya kukusanya kodi. Sasa katika kipindi hiki cha mpito unategemea nini?
Hawawezi kuacha wote kwa Mara moja, watu wana njaa[emoji2]
 
Mkuu mishahara ya vyuo ni ya kawaida sana wala asikudanganye mtu. Hapo wanaozungumziwa ni TRA, TANROADS, BOT, TTCL, TANESCO na yanayofanana na hayo.
Mkuu waonee huruma TTCL na uwaondoe kabisa kwenye hilo kundi. Badala yake ongezea taasisi kama TCRA, SUMATRA, EWURA, TPDC n.k.
 
UNAMAANISHA WOTE WATALIPWA TGS?

TRA
BOT
NSSF,PSPF,PPF,GEPF,LAPF,SSRA,
EWURA
TFDA
FCC
SUMATRA
TCRA
TPA
TCCL
TPB
MZUMBE
UDSM
LGTI
TPSC
UDOM
SUA
PPRA
TBC n.k

WOTE HAWA WATALIPWA KWA SCALE ZA TGS? KAMA HVYO NI SAWA TU.
 
UNAMAANISHA WOTE WATALIPWA TGS?

TRA
BOT
NSSF,PSPF,PPF,GEPF,LAPF,SSRA,
EWURA
TFDA
FCC
SUMATRA
TCRA
TPA
TCCL
TPB
MZUMBE
UDSM
LGTI
TPSC
UDOM
SUA
PPRA
TBC n.k

WOTE HAWA WATALIPWA KWA SCALE ZA TGS? KAMA HVYO NI SAWA TU.
Mkuu unapenda washushwe? Ingekuwa vizuri ungeomba wa chini apandishwe.Akishushwa wa juu wa chini unafaidikaje?
 
Nchi ni yetu sote, Kwa HILI nipo pamoja na Rais Magufuli ninampongeza sanaa.Mfanyakazi wa bandari elimu Yake ni diploma tu ,lakini analipwa mshahara mzito kuliko Mwalimu mwenye Digrii, MISHAHARA IANGALIWE UPYA KILA MMOJA TULIPWE SAWA KWA SAWA ,HEKOOO RAIS MAGUFULI
Unashauri wa Bandari ashushwe au unashauri huyu wa Degree apandishwe?
 
Back
Top Bottom