Safe space is created by a woman herself.Labda hakuna safe space ya wao kuwa feminine, Hatuwezi kuwatupia lawama kwa 💯
Hapana leo hukua unatania banaNatania tu! Mi huwa nakwenda na vibes za watu humu 😂
Hata wewe ungezungumza mkuuKuna yule dada aliyemuua mme wake akamfukia nyuma ya nyumba yao, yule watu hawakumzungumzia.
Hamna kitu hayo ni maneno mdomoni ila inside wanakigagazikoUkiwakuta sasa wanajisifia kuwa huwa wanatumia akili na sio hisia kufanya maamuzi ndio utachoka🙆♂️🙆♂️🙆♂️
Niheshimu tu bibie kama zamani. Kosa Moja halimfukizi mke 😅Hapana leo hukua unatania bana
Hakika mkuu ifanyike namnaNi kweli kabisa kuuwa mtu sio jambo zuri hata kidogo apa ilitakiwa sasa wanasaikolojia wawe wengi kwenye Nchi yetu ikiwezekana kuwe na vipindi vya kutosha kwenye Tv na kwenye Radio tupate elimu ya kutosha ya kisaikolojia inaweza ikasaidia kwa kiasi kikubwa.
Wanawake tamaa za Mali zitawaua muishe na kama ni mambo ya wivu Kwa nini uolewe na limwanaume linajifanya linakupenda saaana? Huoni kwamba ni hatari?Angalizo msomaji wangu bandiko ni refu kidogo
Naomba uwe mvumikivu katika usomaji wako
Karibu sana kwenye mada 😊
Hello Great Thinkers 🫡
Katika pita pita zangu huko IG nimekuta kuna dada mmoja amepost kuhusu vifo vinavyotokana na migogoro ya kimahusiano hapa Tanzania 🇹🇿
Nimekuwa shocked baada ya kuona takwimu zinaogopesha na kushangaza
Ikanisukuma niende kwenye mtandao ku search na nione hali ilivyo kwa kujihakikishia mimi tomaso nimeshtushwa
Sikujua hali ni mbaya kwa ukubwa huu!
Nimepigwa butwaa
Hali inatisha
Chanzo cha takwimu (LHRC Tanzania)
Niweke sawa hapa
Hizi takwimu ni kati ya mwaka 2019_2023
Hebu tuangalie hizi takwimu za mauaji yanayohusisha wenza wa kimapenzi Tanzania
2019: LHRC ilirekodi wanawake 12 waliouawa na waume/wenza wao ambapo 8 ya matukio hayo yalihusishwa na wivu
2020: LHRC ilirekodi wanawake 32 waliouawa na waume/wenza wao, ambapo 23 ya matukio hayo yalihusishwa na wivu
Hii ilikuwa zaidi ya mara mbili ya matukio yaliyorekodiwa mwaka 2019
2021: LHRC ilirekodi jumla ya matukio 35 ya mauaji yaliyohusisha wenza wa kimapenzi
Kati ya waathirika hao, 31 walikuwa wanawake na 4 wanaume, huku wanawake wakiwa takribani 89% ya waathirika
Pia, 72% ya matukio hayo yalihusishwa na wivu
2022: Kulikuwa na matukio 33 ya mauaji yaliyohusisha wenza wa kimapenzi
Kati ya waathirika, 31 walikuwa wanawake na 2 wanaume, wanawake wakiwa takribani 94% ya waathirika. 52% ya matukio hayo yalihusishwa na wivu
2023: LHRC ilirekodi matukio 50 ya mauaji yaliyohusisha wenza wa kimapenzi, ikiwa ni ongezeko la matukio 17 ukilinganisha na mwaka 2022
Kati ya waathirika hao, 45 walikuwa wanawake na 5 wanaume, wanawake wakiwa 90% ya waathirika. Takribani 46% ya matukio yalihusishwa na wivu.
Mjumuisho 2019–2023: Jumla ya matukio 162 ya mauaji yaliyorekodiwa katika takwimu hizi. Kati ya waathirika waliotajwa, wanawake ni 151
Mjadala👇
Sitaki kusema hakuna wanawake wanaofanya ukatili
Tumeona wapo na siwezi kufumbia macho hili hata kidogo
Wanawake wenzangu JF hakuna haja ya kukatisha maisha ya mtu kwa sababu tu ya mapenzi au migogoro mbalimbali
Ukiona mzigo ni mkubwa, tafuta msaada
Usimue mtu
Huna haja ya kuua, hilo sio jukumu lako
Kwa sababu hata usipomuua, kwa nature ya mwanadamu kila mtu lazima atakufa siku yake
Nina hakika wanaofanya mauaji huishia kwenye majuto ya milele
Tuje kwa wanaume ambao ni tishio...
Enyi wanaume, acheni kuua wanawake
Hawa ni mama zenu, dada zenu, wadogo zenu
Hakuna mwenye haki ya kuua mwingine kwa sababu tu amesalitiwa, amevunjwa moyo au amekataliwa
Ukihisi umefika sehemu huwezi kujidhibiti, tafuta msaada
Tafuta hata wataalamu wa saikolojia
Kama umechanganyikiwa na hujui ufanye nini, ongea uponeeee
Acha kubeba uchungu peke yako. Tafuta mtu wa kuongea naye
Kama unaogopa jambo lako kutangazwa, tafuta hata mtu asiyekujua, funguka na zungumza
Usiue Please
Hakuna mwenye haki ya kuua mwingine
Kama unaona hakuna future kwenye mahusiano, jikatae mapema na muachane kwa amani
Niseme hili👇
Wanaume, mkubali mkatae, mna udhaifu ambao mnatakiwa kuushinda
Kujifunza kustahimili maumivu rejection usaliti na kuvunjika moyo ni sehemu ya kukomaa
Chukulieni mfano hata hapa jukwaani
Watu wanaoongoza kuwakalia kooni wengine ni wanaume nyie hapo🫵
Nasikia wengine wanapita mpaka PM wakisambaza picha za wanawake ambao hawana hata uhakika nao
Kitu ambacho ni nadra kwa wanawake kufanya
Kuweni wakomavu
Jifunzeni kustahimili
Mbona wanawake wanahangaika na maisha?
Unakuta mama kaachiwa watoto, anakomaa na haui mtu
Amedhulumiwa anatulia
Anamfumania mume wake kitandani, tena na house girl kwenye kitanda chake mwenyewe lakini mama anapiga moyo konde
Mnazalisha nje huko, wanawake wanapiga moyo konde
Enyi wanaume, nyie mna roho za barafu?
Wanawake wana roho za chuma?
Sitetei yeyote
Sitetei mwanamke msaliti wala mwanaume msaliti
Lakini ukiona umeshindwa kabisa kuendelea na mahusiano, achaneni kwa amani
Tatizo ni nini mpaka hali imefika hivi?
Karibu tujadili kwa pamoja
Na kuelemishana 🙏🙏
ShesRise_1 ✋️
Kwa namna yoyote ile huna haki ya kuua mtu wewe unaweza kuumba ?Asilimia kubwa ya vifo vimetokana na wivu wa mapenzi, na hapa kinachoongelewa ni usaliti uliosababishwa na tamaa, na waathirika wakubwa wa jiji kadhia ni wanawake sasa tuje kwenye hoja ya msingi:
1. Ni wanawake kuacha tamaa ya pesa au ya mali na kutumia ulaghai wa mapenzi ili kupata, punguzeni tamaa badala yake tumieni nguvu na uwezo aliopewa na Mungu kuchuma vya kwenu, msiifanye ndoa ndio ili mchume mali.
2. Ukisema wanaume waache, ilihali chanzo cha hayo yote ni usaliti wa wanawake itakuwa haujatibu tatizo nadhani liwekwe hivi, Wanawake kama mwanaume hauna mpango naye au haumtaki usile vya kwake wengine mnakimbilia kula chakula vya wanaume kwa kigezo cha namchuna bila kujua anapotia njia gani kuzipata hizo fedha, wengine wanazipata kwa njia ngumu sana sasa ukimfanyia ndivyo sivyo reaction yake ndio hiyo
Ningali nakumbuka kisa cha mtangazaji wa ITV ufoo Saro, alimpoteza mama yake mzazi, pamoja na mume wake kwa sababu ya haya haya mambo na yeye alijeruhiwa na jamaa alikusudia kuchapa wote risasi wafe bahati mbaya akafa yeye na mama mkwe wake. Wanawake wana jambo la kujifunza kwenye haya mambo pia
😅💔Niheshimu tu bibie kama zamani. Kosa Moja halimfukizi mke 😅
Mbona wengine wanauwana na ni makapuku mmekazana na mali weee hakuna lolote watu wanalala wanaona mali zao zote na still wanauana kuna mali gani hapoWanawake tamaa za Mali zitawaua muishe na kama ni mambo ya wivu Kwa nini uolewe na limwanaume linajifanya linakupenda saaana? Huoni kwamba ni hatari?
Mimi nikipata mwanamke nikaona ana dalili za kunipenda sana sijui nini Huwa sihitaji mtu wa hivyo namuacha Kwa sababu nafahamu hana balance ya hisia na Kuna siku atakuja kusema tukose wote.
Rudi kusoma tena nilichoandika.Unaolewa na mtu mpumbavu unategemea nini? Kwa nini uolewe na mtu ambae eti anajifanya kukupenda saaana huoni Kuna siku atakuua?Mbona wengine wanauwana na ni makapuku mmekazana na mali weee hakuna lolote watu wanalala wanaona mali zao zote na still wanauana kuna mali gani hapo
Nyie wanaume Jifunzeni ukomavu ebooo
Unaongelea nini mkuu?Wanawake waache kutumiwa na maadui zetu - wapinzani wetu, waache tamaa ya kumiliki mali, hizi sheria zilizotungwa kwa shinikizo la hao LHRC (wanaharakati) zimeanza kulipuka kwa vitendo.
Miaka ya nyuma migogoro ya ndoa iliamuliwa kwa busara - wazazi/walezi kuonya vijana wao bila upendeleo; hivi sasa wazazi wanavutia upande wa mkosaji kisa tu mali.
Hizi sheria zimewapa kiburi wanawake (hizo mahakama ndio janga zaidi), huku wanaume wakiamua kuwa aggressive; mambo hayo ni hatari sana kwa ustawi wa jamii.
Unaolewa na anaekupenda kidogo kwamba huyu ndio atakua na huruma na wewe akiamua lake ?Rudi kusoma tena nilichoandika.Unaolewa na mtu mpumbavu unategemea nini? Kwa nini uolewe na mtu ambae eti anajifanya kukupenda saaana huoni Kuna siku atakuua?
Nimekwambia Mimi hata mwanamke au demu nikigundua hivyo tunaachana mapema kabisa,sitaki upumbavu kabisa.
Sio swala la huruma huyo manake haishi Kwa kuendeshwa na mihemko ,mtu anaejitawala hisia zake.Unaolewa na anaekupenda kidogo kwamba huyu ndio atakua na huruma na wewe akiamua lake ?
Mkuu haya 🙏
Men are angels right?Safe space is created by a woman herself.
Ukija kuangalia wanawake wana wa manipulate wanaume wao wenyewe.
Then kikiwalamba lawama wanampelekea mwanaume. Safe space is a good woman, who knows her position in the family
Wanawake mmekuwa vichwa ngumu sana.Men are angels right?
Bye!!✌🏻
MUNGU ameumba watu wa jinsi tofauti×2Huyu hakuwa anatinga kwenye vikao vyetu. sisi tunakutengenezea ka ugonjwa uishi nako, kakufirisi ufe nako.
Tukishindwa tunaenda kupiga kombola la ajari bus zima unakufa peke yako.
Hapana tunapaswa kujua namna ya kutumia akili zetu, ukilitazama tukio, unalitazama kwa mantiki si kwa kufata hisia. Kwenye lile tukio la yule mshkaji na hili ni same scrpt, utofauti ni aina ya mauwaji.Bata wewe ungezungumza mkuu