Angalizo msomaji wangu bandiko ni refu kidogo
Naomba uwe mvumikivu katika usomaji wako
Karibu sana kwenye mada 😊
Hello Great Thinkers 🫡
Katika pita pita zangu huko IG nimekuta kuna dada mmoja amepost kuhusu vifo vinavyotokana na migogoro ya kimahusiano hapa Tanzania 🇹🇿
Nimekuwa shocked baada ya kuona takwimu zinaogopesha na kushangaza
Ikanisukuma niende kwenye mtandao ku search na nione hali ilivyo kwa kujihakikishia mimi tomaso nimeshtushwa
Sikujua hali ni mbaya kwa ukubwa huu!
Nimepigwa butwaa
Hali inatisha
Chanzo cha takwimu (LHRC Tanzania)
Niweke sawa hapa
Hizi takwimu ni kati ya mwaka 2019_2023
Hebu tuangalie hizi takwimu za mauaji yanayohusisha wenza wa kimapenzi Tanzania
2019: LHRC ilirekodi wanawake 12 waliouawa na waume/wenza wao ambapo 8 ya matukio hayo yalihusishwa na wivu
2020: LHRC ilirekodi wanawake 32 waliouawa na waume/wenza wao, ambapo 23 ya matukio hayo yalihusishwa na wivu
Hii ilikuwa zaidi ya mara mbili ya matukio yaliyorekodiwa mwaka 2019
2021: LHRC ilirekodi jumla ya matukio 35 ya mauaji yaliyohusisha wenza wa kimapenzi
Kati ya waathirika hao, 31 walikuwa wanawake na 4 wanaume, huku wanawake wakiwa takribani 89% ya waathirika
Pia, 72% ya matukio hayo yalihusishwa na wivu
2022: Kulikuwa na matukio 33 ya mauaji yaliyohusisha wenza wa kimapenzi
Kati ya waathirika, 31 walikuwa wanawake na 2 wanaume, wanawake wakiwa takribani 94% ya waathirika. 52% ya matukio hayo yalihusishwa na wivu
2023: LHRC ilirekodi matukio 50 ya mauaji yaliyohusisha wenza wa kimapenzi, ikiwa ni ongezeko la matukio 17 ukilinganisha na mwaka 2022
Kati ya waathirika hao, 45 walikuwa wanawake na 5 wanaume, wanawake wakiwa 90% ya waathirika. Takribani 46% ya matukio yalihusishwa na wivu.
Mjumuisho 2019–2023: Jumla ya matukio 162 ya mauaji yaliyorekodiwa katika takwimu hizi. Kati ya waathirika waliotajwa, wanawake ni 151
Mjadala👇
Sitaki kusema hakuna wanawake wanaofanya ukatili
Tumeona wapo na siwezi kufumbia macho hili hata kidogo
Wanawake wenzangu JF hakuna haja ya kukatisha maisha ya mtu kwa sababu tu ya mapenzi au migogoro mbalimbali
Ukiona mzigo ni mkubwa, tafuta msaada
Usimue mtu
Huna haja ya kuua, hilo sio jukumu lako
Kwa sababu hata usipomuua, kwa nature ya mwanadamu kila mtu lazima atakufa siku yake
Nina hakika wanaofanya mauaji huishia kwenye majuto ya milele
Tuje kwa wanaume ambao ni tishio...
Enyi wanaume, acheni kuua wanawake
Hawa ni mama zenu, dada zenu, wadogo zenu
Hakuna mwenye haki ya kuua mwingine kwa sababu tu amesalitiwa, amevunjwa moyo au amekataliwa
Ukihisi umefika sehemu huwezi kujidhibiti, tafuta msaada
Tafuta hata wataalamu wa saikolojia
Kama umechanganyikiwa na hujui ufanye nini, ongea uponeeee
Acha kubeba uchungu peke yako. Tafuta mtu wa kuongea naye
Kama unaogopa jambo lako kutangazwa, tafuta hata mtu asiyekujua, funguka na zungumza
Usiue Please
Hakuna mwenye haki ya kuua mwingine
Kama unaona hakuna future kwenye mahusiano, jikatae mapema na muachane kwa amani
Niseme hili👇
Wanaume, mkubali mkatae, mna udhaifu ambao mnatakiwa kuushinda
Kujifunza kustahimili maumivu rejection usaliti na kuvunjika moyo ni sehemu ya kukomaa
Chukulieni mfano hata hapa jukwaani
Watu wanaoongoza kuwakalia kooni wengine ni wanaume nyie hapo🫵
Nasikia wengine wanapita mpaka PM wakisambaza picha za wanawake ambao hawana hata uhakika nao
Kitu ambacho ni nadra kwa wanawake kufanya
Kuweni wakomavu
Jifunzeni kustahimili
Mbona wanawake wanahangaika na maisha?
Unakuta mama kaachiwa watoto, anakomaa na haui mtu
Amedhulumiwa anatulia
Anamfumania mume wake kitandani, tena na house girl kwenye kitanda chake mwenyewe lakini mama anapiga moyo konde
Mnazalisha nje huko, wanawake wanapiga moyo konde
Enyi wanaume, nyie mna roho za barafu?
Wanawake wana roho za chuma?
Sitetei yeyote
Sitetei mwanamke msaliti wala mwanaume msaliti
Lakini ukiona umeshindwa kabisa kuendelea na mahusiano, achaneni kwa amani
Tatizo ni nini mpaka hali imefika hivi?
Karibu tujadili kwa pamoja
Na kuelemishana 🙏🙏
ShesRise_1 ✋️
Mkuu Hongera kwa maada mupya na mujarabu kabisa.
katika maada ya Leo nimekusoma neno kwa neno, nimekuelewa na data zote nimezizingatia lakini bado mzizi wa fitna unaonekana ni mkubwa.
Kutokana na data tatizo limeonekana likiongezeka na chanzo Cha tatizo kwa asilimia kubwa ni wivu wa mapenzi.
Sasa mimi sitaki kujadili nani mbaya au nani mwenye makosa natamani tulijadili tatizo na tupate ufumbuzi wake.
Kutokana na tatizo lilivyojielekeza, linasomeka kama ni ukatili wa kijinsia, Yaani jinsia moja (KE)inabeba madhira ya janga lote la wivu wa mapenzi.
Sasa tujiulize kwanini? Jinsia hii (KE) ibebe hili janga lote la wivu wa mapenzi? Maana mapenzi yanahusisha jinsia zote mbili (ME&KE). Sasa kwanini madhira ya janga lote ibebe jinsia moja?
Kwa asili mwanaume ameumbwa kutamani na kupenda. Mwanaume akimpenda mwanamke anaweza kuibeba dunia yote kwaajili ya huyo mwanamke, mara nyingi mwanaume akimuoa mwanamke bhasi jua anampenda kweli.
Mwanaume akimpenda mwanamke atamuhudumia, atampa anachotaka mwanamke na wengine huenda mbali zaidi hata kufanya majukumu ya mke wake.
Wivu unaanzia wapi?
Kutokana na mapenzi ya mwanaume kwa mwanamke kujumlisha kujitoa ambako mwanaume amesacrifice Kila kitu kwaajili ya huyo mwanamke, bhasi mwanaume hutegemea jambo moja tuu kutoka kwa huyo mwanamke ambacho ni ROYALTY.
Sasa je! Hawa wanawake wanaonyesha hiyo ROYALTY kwa waume zao??
Binafsi mimi naona hapa ndipo penye mzizi wa fitna na huu ndio unahitaji kukatwa.
Mwanaume kama unamuhudumia mwanamke na kumpa Kila kitu lakini bado haoneshi ROYALTY yoyote kwako bhasi ni bora ukajiondoa mapema.
Usiongeze juhudi yoyote ya kumuhudumia mwanamke wa aina hiyo maana mwisho wake utakua ni maumivu na ni maumivu zaidi endapo umeshatumia gharama kubwa kwa huyo mwanamke.
Hapa wanaume tunahitaji kujifunza kuachwa, kuachwa isiwe kama ni changamoto kwetu bali tunahitaji kuona kama chura amepigwa teke.
Mwanaume mwenzangu tafadhari sana chukua tahadhali kubwa sana kwa mwanamke asiyeridhika na kidogo au kile unachompa. Usijitie sana ili kumridhisha mwanamke maana mwisho wake utaishia kuwaza kuua. Najua hii mara nyingi ndio huwa tunaona kama solution kwetu wanaume.
Pia mwanaume mwenzangu, tujifunze tabia za wanawake. Mwanamke akiwa na mwanaume mwingine huwa hajifichi huanza kukudharau na kukupuuzia. Ukiona hizo dalili sitisha haraka hayo mahusiano maana mwisho wake utakua mbaya tuu. Men's love by condition, only women and animals are love unconditionally.
Nije kwa nyie wanawake.
Kwenu swala ni Moja tuu, kuwa mkweli kwa huyo DUBWANA wako, kama upo kwake kimaslahi mwambie ukweli kwamba wewe UNAJIUZA, na hata akitaka kukuweka ndani na kukupa Kila kitu, mwambie wewe ni kunguru na hufugiki. Hili jambo litaokoa uhai wako kutokana na hasira na machungu usiyoyafahamu kutoka kwa huyo DUBWANA.
Pia mwanamke ukiwekwa ndani jitahidi sana kuwa royal kwa huyo mwanaume wako, usichepuke au kufanya mambo yatakayo mfanya akutilie mashaka. Hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke mpole,.mnyenyekevu, msikivu na muaminifu.
Kwa Leo yangu ni hayo tuu.