JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limezuia maziko ya James Januari (4) aliyejeruhiwa usiku wa kuamkia Jumapili na kufariki dunia Julai 5, 2022 katika Hospitali ya Rufaa Morogoro.
Aidha, kuna uwezekano wa kufukua miili sita iliyozikwa Jumapili Julai 3, 2022 baada ya tukio la mauaji ya watu sita wa familia moja kwenye Kijiji cha Kiganza Mkoani Kigoma.
Akizungumza katika shughuli ambayo ilitakiwa kuwa ya maziko yam toto huyo, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ester Alexander Mahawe alitoa kauli ya kuahirisha maziko hayo na kusema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi.
“Mkemia Mkuu wa Serikali yupo Kigoma, wanahitaji kukamilisha ushahidi wa damu ya mtoto James na wale sita waliozikwa pia miili yao inaweza kufukuliwa kwa ajili ya kuchukua sample ya damu ili ushahidi usije ukapelea. Baada yah apo kama hakutakuwa na mabadiliko miili yote saba inaweza kuhifadhiwa.”
Tayari Jeshi la Polisi limeshatangaza kumkamata Peter Moris (33), Mkazi wa Mlole Manispaa ya Kigoma Ujiji ambaye ni fundi ujenzi akituhumiwa kwa mauaji hayo yaliyotokea usiku wa kuamkia Julai 3, 2022
Mkuu wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishna Liberatus Sabas alinukuliwa akisema: “Tumemkamata akiwa Kigoma, tumejiridhisha mtuhumiwa ametekeleza mauaji hayo peke yake kwa kutumia panga na kwamba baada ya kumhoji amedai sababu ni marehemu January Mussa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wake (mtuhumiwa).”
Chanzo: Azam TV