Miji inayoongoza kwa vumbi Tanzania. Shati jeupe usiende nalo

Miji inayoongoza kwa vumbi Tanzania. Shati jeupe usiende nalo

Uswahilini, Sakina yote hiyo kuanzia Kwa Iddi Hadi kiranyi, shuka na vumbi Hadi Ngaramtoni, Kunja Kona nenda nalo Hadi Kisongo, upandishe nalo Kwa Morombo, ingia nalo Sombetini, tokezea Ngusero, dondokea Engo sheratoni, ingia Unga limited, lifuate vumbi Hadi Daraja mbili, Lemara komaa nalo Hadi Njiro, Kijenge, ukiwa Arusha ndo utajua ulitoka mavumbini
 
Hii ni miji kumi inayoongoza kwa vumbi nyakati za kiangazi nchini Tanzania. Ukienda huko achana na habari ya nguo nyeupe. Pendelea rangi nyeusi, brown au kijivu.

1. KARATU
2. KASULU
3. KIBONDO
4. BOMANG'OMBE, Hai
5. SONGEA
6. TUNDUMA
7. ORKESMET, Simanjiro.
8. DODOMA
9. MERERANI
10. MTO WA MBU
Moshi mjini
 
Karatu msimu wa Mvua Kuna kuwa na tope la Hatari sana, Unashindwa kunyanyua mguu kutoka chini, Haswa hayo maeneo ya CCM , uwanja Mboe Hadi kupandisha Maeneo ya Jublate Mnyenye, NMB, Kwa Lekashu, Kadtuli Hadi Peter Ombay , Crater Rim, upande police na TRA shuka mitaa ya NBC kote ni tope ama Vumbi
Karibu sana saiv kuna lami uchwara baadhi ya mitaa!!
 
Vumbi kwanza ni sehemu ya maisha kwa Tanzania nzima kwani maeneo mengi haina miti inayozuia upepo unaotimua vumbi pia barabara nyingi ni za vumbi na miji uliyotaja na mengini mengi haina barabara za lami
 
Umefika Kenya na Zambia? Huko ndo makao makuu ya vumbi. Ukiwa unaenda Nairobi kuna mji unaitwa Kitengela nadhani vumbi la pale ni la mafinga jumlisha Makambako
 
Hii ni miji kumi inayoongoza kwa vumbi nyakati za kiangazi nchini Tanzania. Ukienda huko achana na habari ya nguo nyeupe. Pendelea rangi nyeusi, brown au kijivu.

1. KARATU
2. KASULU
3. KIBONDO
4. BOMANG'OMBE, Hai
5. SONGEA
6. TUNDUMA
7. ORKESMET, Simanjiro.
8. DODOMA
9. MERERANI
10. MTO WA MBU
Namba 2 na 3 juzi nimetoka na gari huko utadhani nimelifukua ardhini, ile nafika mjini kuna mhuni nakuta nyuma kwenye kioo kumeandikwa( "msinioshe kuna balidi)[emoji3] nikibaki nacheka hafi nikapeleka car wash
 
Back
Top Bottom