Miji inayoongoza kwa vumbi Tanzania. Shati jeupe usiende nalo

Umefika Kenya na Zambia? Huko ndo makao makuu ya vumbi. Ukiwa unaenda Nairobi kuna mji unaitwa Kitengela nadhani vumbi la pale ni la mafinga jumlisha Makambako
Zambia naweza kukubali mwaka jana nilikua Nakonde vumbi lipo japo sijajua huko mbele.
 
Manyoni
Singida
Makambako
Mbeya
Gairo
Igawa
Mbarali
Ubaruku
Same
Hedaru
 
Hivi ile barabara kuelekea hotel inayomilikiwa na VETA ilishawekwa rami. Maana ilikua inatoa vumbi sio mchezo
Mwenyeji wetu Arusha alitupeleka Morombo kula nyama kipindi cha mvua,sina hamu kabisa na nyama za huko,nikapata na tumbo la kuhara huko.
 
Umeiacha babalao mbeya Kuna vumbi flani hivi ukitembea kwa Tz 11 mpaka kope na nyusi huzioni
 
Zote ni ngome za ccm
 
Vumbi jekundu Kama la songea jau Sana. Nguo nyeupe kule hazivaliki. 🙌🙌
 
Aloo sio mchezo karatu baba lao. Nilienda msibani kurudi wife anauliza kwani walikugeuza maksai nn maana nguo zinachafuka vumbi la maana. Lile vumbi la karatu unaweza ombea hata mkopo bank.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji28][emoji28]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…