Miji inayoongoza kwa vumbi Tanzania. Shati jeupe usiende nalo

Malila uiache uyole yetuπŸ€’
 
... nimefuatilia huu uzi kwa umakini sana. It seems maeneo yenye vumbi kali ndio yanayolisha hii nchi; ndiko kilimo kiliko kuanzia nafaka, jamii za kunde, mboga mboga, viazi ulaya, matunda, ndizi, etc. Cha muhimu ni serikali kuboresha miundombinu ya barabara kwa kuweka lami ila mashambani libarikiwe vumbi linalotupa chakula.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]kakonko imefikiwa!
Mara ya kwanza kupita Nyakanazi hadi Kasulu ilikuwa 2014 nilikua naenda harusini. Hiyo njia yote ilikuwa sio poa vumbi lake.... hadi leo huwa najiuliza watu wa Kigoma walifanyaga kosa gani kwa serikali hadi maendeleo kutopelekwa mikoa hiyo? Kwa mfano kwenye umeme wameunganishwa na gridi ya taifa majuzi tu Makamba akiwa waziri. Barabara ya Nyakanazi - Kasulu ndo inajengwa.
 
Nadhani kwa matokeo ya jumla hadi sasa mkoa wa Arusha unaongoza kwa maeneo yenye vumbi. Kutoka Arusha mjini hadi Namanga ni vumbi tupu nje ya lami. Arusha hadi Orkesmet nako ni mavumbini. Mto wa mbu hadi Loliondo kwa babu nako mavumbini. Wilaya ya Karatu ndo haina mpinzani kwa Afrika Mashariki, kati na kusini.
 
Mbeya mjini kuna lile powder la Johnson
 
Karatu kuna vumbi la kufa mtu,hakuna mabati meupe huko
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji28][emoji28][emoji28] sipati picha
Cha kuchekesha wakati tunaenda Kanisani tukakutana na shoe shine tukajifanya kupolish....... asilimia kubwa tukiwa wageni,njia ya Kanisani sasa daah......baada ya kuuliza nikaambiwa nikwasababu eneo lile ni mkondo wa njia ya Tanzanite Arusha,na kipindi cha mvua kunakuwa kama Lami
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Inatia aibu sana serikali yetu inayodai kazi iendelee haifanyi lolote kuondoa haya...

Watakusikia wenzako, urudi ndani ya Mwezi Moja utuambie vumbi sio tatizo tena hayo maeneo umetaja na mengineyo
AiseeπŸ€”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…