Miji inayoongoza kwa vumbi Tanzania. Shati jeupe usiende nalo

Miji inayoongoza kwa vumbi Tanzania. Shati jeupe usiende nalo

Kwa comments za humu inaonekana kila mahali Tanzania kuna vumbi ila Kibondo kwangu mimi ni balaa. Utofauti mara nyingi huletwa na rangi ya udongo. Vumbi la udongo mwekundu ni hatari sana bora kuna sehemu zina vumbi lakini sio jekundu hivyo halichafui sana.
Kibondo nadhani ndio inaongoza kwa Tz, kiangazi vumbi, masika tope la kuzamisha mpk miguu. Na masika huku safari ya saa moja mnaweza tumia siku nzima kwsbb magari yanateleza
 
Pole, Kibondo wenyewe wanasema hawataki maendeleo kwani siku zote walikuwa wanaishije? Waha kwa ubishi kwa kweli hawajambo, yaani wanawazidi wanyamwezi na waluguru kwa ubishi wa kijinga, Muha haoni hasara kutembea kilomita 100 na kulisusa basi kisa limechelewa kufika kituoni muda uliokadiriwa.
Hilo la kutembea Km 100 unawasingizia bana! Maendeleo pia sio hawayataki, ila wamecheleweshewa.

Mf Lami asingekua Magu na Mpango asee wangeisoma namba sana tu.

Kasulu pana Maendeleo sana kwa mkoa wa Kigoma, ila changamoto ni vumbi na tope ila wako poa sana. (Nimefanya kazi huko kwa makambi ya wakimbizi)
 
Kibondo nadhani ndio inaongoza kwa Tz, kiangazi vumbi, masika tope la kuzamisha mpk miguu. Na masika huku safari ya saa moja mnaweza tumia siku nzima kwsbb magari yanateleza
Safiri siku moja kwenda liwale lindi huko, kiangazi vumbi mpaka mafua kifuku ndo maji yanakata barabara kukwama kawaida serikali iwaonee huruma wakazi wa huko wanateseka sana
 
😂😂😂

Inatia aibu sana serikali yetu inayodai kazi iendelee haifanyi lolote kuondoa haya...

Watakusikia wenzako, urudi ndani ya Mwezi Moja utuambie vumbi sio tatizo tena hayo maeneo umetaja na mengineyo
Haifanyi lolote au mahitaji ni makubwa kuliko uwezo wa Serikali? Unajua gharama ya kujenga km 1 ya Barabara? Kuna Miji mingapi hapa Tanzania? Ukuaji wa Miji unaosababishwa na Ongezeko la watu haiendani na uwezo wa Serikali.

Serikali iliwaletea tozo mkakataa unadhani pesa italetwa na mvua? Kodi zenyewe mnakwepa,komaeni tuu na hapo ni sekta Moja tuu na sekta zingine ziko hivyo hivyo.
 
Hii ni miji kumi inayoongoza kwa vumbi nyakati za kiangazi nchini Tanzania. Ukienda huko achana na habari ya nguo nyeupe. Pendelea rangi nyeusi, brown au kijivu.

1. KARATU
2. KASULU
3. KIBONDO
4. BOMANG'OMBE, Hai
5. SONGEA
6. TUNDUMA
7. ORKESMET, Simanjiro.
8. DODOMA
9. MERERANI
10. MTO WA MBU
Geita Iko wapi? Kiufupi Miji Yenye nafuu ni Ile ambayo walau Ina Ardhi ya kichanga tofauti na hapo ni majanga tupu.
 
sehemu kubwa ya nchi ni vumbi, wana mpo US nini!
Hata Mimi nawashangaa wakati Kuna Miji ya Wilaya hakuna hata km 1 ya lami au kama zipo haizidi hata 4 sembuse hiyo Miji mikubwa walau mjini kati Kuna lami.

Ni hivi Tanzania yote ni hivyo hivyo mahitaji ni makubwa kuliko uwezo wa Serikali kuhudumia.
 
Ila dodoma nyie kuna upepo na baridi sijawahi ona. Bahati nzuri nilifikia area D sikuona hata vumbi sikupata bahati ya kutembea kwa miguu ila baridi na upepo watu wa dodoma mtakuwa mmepauka balaa.
Dodoma Kuna Baridi? Acha mzaha basi hata huo upepo ni Kwa sababu ya msimu wa upepo ambao Huwa unaanza mwezi wa 6 Hadi wa 10
 
Kumbe tunaoishi Mpanda& Sumbawanga tujihesabie tuko Pwani hakunaga mavumbi ya kisengerema huku 😂😂
 
Dodoma Kuna Baridi? Acha mzaha basi hata huo upepo ni Kwa sababu ya msimu wa upepo ambao Huwa unaanza mwezi wa 6 Hadi wa 10
Usibishe mkuu kitu usichokua na uhakika nacho.
Ukweli ni kwamba Dodoma mjini kuanzia mwezi wa sita hadi wa kumi kuna baridi kali sana pamoja na upepo mkali(hasa nyakati za kuanzia usiku hadi asubuhi).
Maeneo kwa mfano Mkonze,Matangini,Kikuyu,Maghorofani,Chinyonya,Chidachi huko baridi ni balaa(yaani ni marambili ya baridi ya mitaa mingine ya mji)manake kule ni juu mlimani.
Kule Matangini,Mkonze kuna stendi ya mabasi ya kwenda Iringa,Njombe,Mbeya,Songea ukifika pale saakumi na mbili asubuhi hilo baridi lake ni kamavile uko Makete ...wasafiri ambao ni wageni au wanasafiri kwa mara ya kwanza wakifika pale kama hawajavaa makoti na majaketi huwa wanakiona cha mtema kuni😀😀.
Eneo lingine lenye baridi sana ni kule Udom-Ofisi za Sekretariati ya ajira.Waulize wanaoendaga kule kufanya interview watakwambia baridi la pale si mchezo hasa nyakati za asubuhi
 
Back
Top Bottom