Miji midogo midogo Tanzania ambayo ina vibe na fursa za kibiashara lakini haivumi

1. Ndanda
2. Matai
3. Lyanzumbi
4. Rungwa
5. Inyonga
6. Lupa Tinga Tinga
7. Dumila
8.Laela
9. Mangaka
10. Madaba
11. Makambako
12. Tinde
13. Ikwiriri
14. Tura

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Yaaaaaas, Makambako, Mafinga hii miji ambayo ilishajitafuta na sasa ishafika viral. Uwepo wa biashara kuu za mbao, viazi, chai inachochea sana maendeleo kwenye hii miji.
Kwangu Mimi sioni tofauti kati ya mtu anayeishi Mbeya Jiji na mtu wa Mafinga/Makambako.. hawa wote kama maokoto yapo mifukoni basi wanakula Raha zote za miji.
Makambako/Mafinga ni rahisi kwenda sehemu yoyote Tanzania hii maana usafiri ni Masaa yote Mzee hata semi za mbao unadandia..
Kipindi Najitafuta kielimu pale Mafinga Town, likizo nilikuwa napanda sana semi za mbao kuelekea Dar😃

Kuhusu Ndanda,, pale bado kiupande wa Fursa labda kama wewe ni kijana umemaliza kozi za Afya basi teremka pale Ndanda Hospital (Abasia Ndanda)ukaombe kazi.. usikubali kukaa kizembe.
Kipindi Niko pale Mwena-Ndanda weekend nilikuwa natoka na wadau tunaenda kuinjoi Masasi Town...
Jida, Kaumu, Uwanja wa fisi tumeinjoi sana.
 
tunawahakikishia watanzania kuwa , tulipotezewa muda sana na mkoa wa mbeya
tunawaahid kuwa miaka kumi mbele tutakuwa sawa na miji mikongwe kama IRINGA mc, kahama, na moshi

na kizuri sisi tuna miji mingi na inakuwa kwa kasi yote
 
Rudi ukapachunguze vizuri pale

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ukuaji wa miji pekee haitoshi,sisi watu wa Bebezi/Totoz,Je Bebez au Totoz zinaendana na kasi ya ukuaji wa hiyo miji?

Siyo natoka kwangu Dar naelelekea Nyangao huko Mkoani Lindi kwenda kushangaa Minazi na Uvunaji wa Ufuta!
Mkuu pale Nyangao kuna toto za Kimwera, kimakonde, kiyao, kimakuwa.. Je utaziweza..?😃
Omba experience kidogo kwa LIKUD maana anazijuaga ni mzoefu wa maeneo yale Lindi/Mtwara
 
Hapo kwenye Kidatu sio kweli, pale panaitwa Ruaha ni wilaya ya Kilosa. Kidatu ni ukivuka daraja linalotenganisha wilaya ya Kilosa na Kilombero. Kidatu ni Kilombero sio Kilosa. Hata viwanda vya sukari pale viko viwili K1 na K2 kimoja kipo Kilosa kingine kipo Kilombero japokuwa vipo pamoja.
 
Ikwiriri iko poa sana
 
tunawahakikishia watanzania kuwa , tulipotezewa muda sana na mkoa wa mbeya
tunawaahid kuwa miaka kumi mbele tutakuwa sawa na miji mikongwe kama IRINGA mc, kahama, na moshi

na kizuri sisi tuna miji mingi na inakuwa kwa kasi yote
Sawa , lakin niny wanyiha na wandari ni ndugu zetu Tu.

Hakuna aliyewapotezea muda maana hata Mbeya kuna miji mingi inayokuwa Kwa Kasi.

Mfano Wilaya ya Mbarali peke yake kuna miji Kama mitano au Zaid inakuja vizuri.
1. Ubaruku
2. Rujewa
3. Igawa
4. Chimala
5. Igurusi
6. Mswiswi
 
Wilaya, Miji midogo na centers zinazokua kwa kasi
1. Makongolosi Chunya Mbeya
2. Tinde Shinyanga
3. Runzewe na Nyakanazi
4. Ifunda Iringa
5. Ilula
6. Kibaigwa Dodoma
7. Saza Songwe
8. Busisi Sengerema
9. Isaka Kahama
10. Lupa Chunya
11. Migoli Iringa
12. Mkwajuni Songwe
13. Igawa Mbeya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…