Miji midogo midogo Tanzania ambayo ina vibe na fursa za kibiashara lakini haivumi

Miji midogo midogo Tanzania ambayo ina vibe na fursa za kibiashara lakini haivumi

MPEMBA na Tunduma nakubali,, Ila Mlowo-Vwawa bado kuungana kihivyo. Kuwa hadhi ya Manispaa sana,, wakazi na serikali inabidi kuzidi kuboresha miji hii zaidi Hadi ifikie huko.
Kwa mantiki hyo kama Mlowo/Vwawa zikiwa Manispaa basi Moshi, Morogoro Mtwara, Iringa inabidi yawe Majiji😃
Zitakuwa Manispaa zikiunganishwa sio kusimama kama Mji unaojitegenea.Ndio maana Makao Makuu ya Mkoa yakajengwa pale katikati kurahisisha Hilo zoezi.
 
Igawa imepata bahati ya kupitiwa na ile barabara yenye hadhi ya juu iliyoanzia pale Igawa mpaka Iringa,, kwa kifupi Igawa imependezeshwa na yale mataa ya barabarani bila kusahau ule upanuzi wa barabara kwa ajili ya kuegeshea malori. All in All Igawa ni kituo ya ku-park Malori tu nyakati za usiku..
Siku Igawa ikija kuungana vizuri hadi kule Ubaruku basi Mji utakuwa mkubwa sana,, But fursa kule ni Kilimo cha Mpunga tu😁
Mtwango Njombe
Kilyamatundu,Ilemba Rukwa
Majimoto,Katavi
Katoro Geita
Igawa,Ubaruku Mbarali
Igwachanya,Wanging'ombe
Makongolosi ,Chunya
 
Hii miji midogomidogo mingine hebu niitaje tu ili wadau wengine waweze kuifahamu na kama wanahitaji kutafuta/kufuata fursa huko basi wafuate.
• Kibaigwa
• Nanyamba
• Mahuta
• Chimala
• Ikwiriri
• Mangaka
• Nagaga
• Nangurukuru
• Ilula
• Kalenga
• Mlimba
Nanyamba sio Mji mdogo,Ni Halmashauri ya Mji wa Nanyamba TC
 
Labda kama unamaanisha Mangaka, BUT Nanganga ni kijijini tu sema ni Kijiji kilichopo njia kuu ya kwenda Masasi na Lindi/Mtwara bila kusahau hapa ndipo pacha/barabara ya kuelekea Ruangwa kwa Wamwera au kwa Mh: Kassim Majaliwa(PM), barabara hii ya kutoka Nanganga to Ruangwa ipo katika matengenezo ya hali ya juu kuelekea kiwango cha lami(Trunk Road)
Upo sahihi Nanganga pale bado labda Lami ya Ruangwa ikamilike...ila Ikwiriri pamechangamka japo mafuriko mwaka huu yaliwanyoosha
 
Igawa imepata bahati ya kupitiwa na ile barabara yenye hadhi ya juu iliyoanzia pale Igawa mpaka Iringa,, kwa kifupi Igawa imependezeshwa na yale mataa ya barabarani bila kusahau ule upanuzi wa barabara kwa ajili ya kuegeshea malori. All in All Igawa ni kituo ya ku-park Malori tu nyakati za usiku..
Siku Igawa ikija kuungana vizuri hadi kule Ubaruku basi Mji utakuwa mkubwa sana,, But fursa kule ni Kilimo cha Mpunga tu😁
igawa kuna vitunguu pia
 
Igawa na Rujewa zimeshaungana so is like Mji mmja na itafika huko Ubaruku.

Lakini Igawa Ina viwanda vikubwa vya nataka hasa kukoboa na kupaki Michele.
 
Nakubaliana na wewe Kuna Nanyamba ni Town Council ili kuwa TC sio shida.. Hivi unajua kuwa pale Mtama Jimboni kwa Nape Nnauye ni District Council Ila bado pamepoa sana. Pale Mtama hata hospital ya Wilaya/Halmashauri hawana nasikia Kuna kituo cha Afya kidogo kimejengwa pale Maumbika kama sio Kiwalala[QUOTE="The Sunk Cost Fallacy 2, post: 50387495, member: 689752"PP
Nanyamba sio Mji mdogo,Ni Halmashauri ya Mji wa Nanyamba TC
[/QUOTE]
 
Jamani msiisahau Namtumbo, ni Wilaya iliyojificha sana na si maarufu,, ipo umbali wa Kilomita 70 kutokea Manispaa ya Songea kuelekea kusini Mashariki..
Sasa hivi hii Wilaya inajenga sana, mara ya mwisho kwenda pale ilikuwa mwezi March 2024.
Kwa Sasa wana Mkuu wa Wilaya Mrembo sana pale namtumbo
Sehemu yeyote Barabara za lami zikifika tayari inaanza kukua.

Namtumbo Kuna ufuta sana huko ila sijasikia mtu akitaja Tunduru
 
Mafuriko yamekuja kuharibu hadi ukuaji wa Wilaya ya Kibiti, Yale maeneo yote ambayo yalikuwa yanaporomoshwa mijengo, sasa hivi serikali imeamuru watu wahame,, kwa mantiki hiyo Mji hauwezi kukua
Upo sahihi Nanganga pale bado labda Lami ya Ruangwa ikamilike...ila Ikwiriri pamechangamka japo mafuriko mwaka huu yaliwanyoosha
 
Nakubaliana na wewe Kuna Nanyamba ni Town Council ili kuwa TC sio shida.. Hivi unajua kuwa pale Mtama Jimboni kwa Nape Nnauye ni District Council Ila bado pamepoa sana. Pale Mtama hata hospital ya Wilaya/Halmashauri hawana nasikia Kuna kituo cha Afya kidogo kimejengwa pale Maumbika kama sio Kiwalala[QUOTE="The Sunk Cost Fallacy 2, post: 50387495, member: 689752"PP
Nanyamba sio Mji mdogo,Ni Halmashauri ya Mji wa Nanyamba TC
[/QUOTE]
Elewa hizo classification,Ili sehemu iwe TC lazima iwe imekidhi idadi Fulani ya watu tofauti na DC ambapo wanaweza chagu kimji au Kijiji chochote wakaweka Makao Makuu eg Usevye kule Mpimbwe ni Kijiji tuu lakini Mji mkubwa wa biashara Wilaya ni Majimoto.

So Nanyamba TC ni Mji mkubwa Kwa vigezo vya Mji kabisa unless utaje Mji ambao haujapata hiyo status ya TC ila umezidi Nanyamba
 
Wakuu,

Uzi huu ni kwa ajili ya kutaja miji midogomidogo ndani ya nchi yetu ambayo ina vibe kubwa kama miji mikubwa na ina fursa za kibiashara lakini haivumi wala kujulikana sana na watu.

Mimi naanza kama ifuatavyo:

1. MLOWO
Huu ni miongoni mwa miji midogomidogo inayokuwa kwa Kasi, ni Mji Mdogo unaopatikana Mkoa mpya wa Songwe, Wilaya ya Mbozi. Mji huu upo barabara kuu ya kutoka Mbeya Jiji kuelekea Tunduma. Ni Mji unaokua kwa kasi na unafursa ya kibiashara hasa mazao. Mji huu unazungukwa na vijiji vingii ambavyo wakazi wake wanajishughulisha na kilimo cha Mahindi, karanga, Maharagwe Alizeti, parachichi, kahawa n.k

Mji huu wa Mlowo una pacha/njia ya kuelekea miji mingine kama Kamsamba, Momba na Chunya. Pacha hii ndio pacha inayofika hadi kwenye Shamba kubwa la serikali la mahindi ambalo kwa sasa liko chini ya Wakala wa Mbegu wa Taifa(ASA).

2. MPEMBA
Huu pia ni Mji unaokua kwa kasi, upo mkoani Songwe Wilaya ya Tunduma, kilometers 10 kutoka Tunduma mji. Mji huu una fursa za kibiashara na Kilimo.

3. VWAWA
Hapa ndipo Makao makuu ya Mkoa wa Songwe ambapo kwa sasa Mkuu wa Mkoa huu ni Daniel Chongolo. Ni Mji unaokua kwa kasi kutokana na kusimikwa kwa huduma nyingi za kijamii zenye hadhi ya mkoa. Miaka michache Mji huu utaungana na Mji wa Mlowo kutokana na ukaribu bila kusahau mijengo mikali inayoendelea kuporomoshwa ndani ya Mji huu.
Karibu Vwawa.

4. NYANGAO
Ni Mji unaopatikana Kusini Mashariki mwa Tanzania ndani ya Mkoa wa Lindi, Wilaya ya Lindi DC. Mji huu mkongwe ambao wajerumani waliweka ngome yao hapa na kufanikiwa kujenga kanisa kubwa na Mission yao. Mbali na hilo wajerumani walijenga hospital kubwa sana ndani ya Mji huu(St Walburgus referral Hospital Nyangao).

Wakazi wengi wa Mji huu ni wakulima wa mazao kama Mahindi, mpunga, Alizeti, karanga na mazao ya biashara Kam Ufuta na Korosho, bila kusahau biashara za samaki/dagaa.. ambapo Mji huu umekuwa kama center ya biashara hii ambapo samaki/dagaa wengi wanaotoka bahari ya Kilwa na kuja Nyangao. Watu mbalimbali kutoka katika vijiji vilivyo karibu na Mji wa Nyangao wanakuja kujumua samaki/dagaa hapa.

Kitu lingine Cha kufahamu ni kuwa Mji huu upo mpakani kati ya Mkoa wa Lindi na Mtwara kutokea Masasi Town, Pia ni sehemu ambapo Mbunge wa Mtama na Waziri mwenye dhamana ya habari, masiliano na Teknolojia(Nape Nnaye) huwa anapategemea sana kuchukuwa/kupigiwa kura za kutosha katika chaguzi zinazofanyika, hii ni kutokana na idadi ya watu waliopo Mji huu ambao ni wanachama wa Chama Mapinduzi.

Nyangao kuna shule za level ya juu (High) kama MAHIWA HIGH SCHOOL na NYANGAO HIGH SCHOOL ambayo inasemekana inamilikiwa na Waziri mkuu(Mh : Kassim M Kassim). Ukitaka kufahamu shule hii kwa undani basi fuatilia Zamaradi TV. Pia kuna chuo cha kati cha Afya kilichopo karibu na Hospital ya Nyangao na vyuo vingine vya ufundi.

KIDATU
Mji huu upo ndani Wilaya ya Kilosa japo watu wengi wanachanganya kwa kufahamu kuwa upo wilayani kilombero. Mji huu unakuwa kwa Kasi sana, hii inachagizwa na uwepo wa kiwanda kikubwa Cha sukari almaarufu kama Kilombero Sugar Company. Wakazi wengi wa mji huu ni wakulima hasa Kilimo cha miwa ambapo soko lake kuu la miwa linapatikana katika kiwanda hicho cha sukari. Mji huu una fursa za kibiashara hasa kutokana na wageni wanaokuja kununua sukari kiwandani hapo bila kusahau Crew kubwa ya wataalam kutoka kiwandani hapo.

Kuna chuo kimoja kikongwe sana kinachofahamika kama NATIONAL SUGAR INSTITUTE. Chuo hiki kinatoa kozi mbalimbali za Stashahada ya uhandizi Umeme, Kilimo na Sukari n.k

Pia Mji unahuduma za kibenki na sehemu nyingi za starehe bila kusahau Mji huu umepitiwa na barabara kuu ya kuelekea Mji wa Ifakara.

Karibu Kidatu.

ITAENDELEA...
Huo mji wa Kidatu jina lake halisi ni Ruaha. Patamu sana hapo.
 
Sehemu yeyote Barabara za lami zikifika tayari inaanza kukua.

Namtumbo Kuna ufuta sana huko ila sijasikia mtu akitaja Tunduru
Tunduru na Masasi ni Wilaya ambazo zinakaribiana japo ziko ndani ya Mikoa miwili tofauti ila Masasi inazidi kukua zaidi, Sasa hivi Masasi wanamiliki Council mbili ambazo ni Masasi District Council & Masasi Town Council.
Mara ya mwisho kupita Masasi ni May 2023.. Duuh Masasi ya sasa ina barabara za lami mitaani, Ile Hospital ya Wilaya Mkomaindo na vyuo ya Afya(Masasi- COTC) vyote vimeboreshwa. Pale sokoni Kaumu Maghorofa yanajengwa. Stand kuu inahamishwa ili kutanua Mji, stand ya kisasa itaanza kujengwa soon.
 
Back
Top Bottom