Miji midogo midogo Tanzania ambayo ina vibe na fursa za kibiashara lakini haivumi

Miji midogo midogo Tanzania ambayo ina vibe na fursa za kibiashara lakini haivumi

Tunduru na Masasi ni Wilaya ambazo zinakaribiana japo ziko ndani ya Mikoa miwili tofauti ila Masasi inazidi kukua zaidi, Sasa hivi Masasi wanamiliki Council mbili ambazo ni Masasi District Council & Masasi Town Council.
Mara ya mwisho kupita Masasi ni May 2023.. Duuh Masasi ya sasa ina barabara za lami mitaani, Ile Hospital ya Wilaya Mkomaindo na vyuo ya Afya(Masasi- COTC) vyote vimeboreshwa. Pale sokoni Kaumu Maghorofa yanajengwa. Stand kuu inahamishwa ili kutanua Mji, stand ya kisasa itaanza kujengwa soon.
Jengeni stendi Kwa sababu ya mahitaji sio kutanua Mji.Mji haukui Kufuata stendi huo ni ujinga wa watu wa Serikali,Mbeya walikataa huo upuuzi wanajenga Old Airport na Mji unaendelea kukua.

Sumbawanga,Iringa nk hakuna mtu anajenga Kufuata stendi matokeo yake stendi hazitumiki hata baada ya kulazimsha watu Kwa sababu wamejemga maporini huko Kwa akili hizo hizo za kukariri eti kutanua Mji.
 
Kwa Tanzania hii miji iliyopangiliwa ni michache sana tena inawezekana nisiijue,, hata Jiji la Dar maeneo mengi ya Mji/Jiji yako shaghalabaghala kimpangilio
Binafsi napenda Miji iliyopangiliwa vizuri na yenye mandhari kuliko mnayoita imechangamka ,in most cases Huwa kama magulio,madampo ni hovyo no order but Kwa wafanyabiashara ndio maeneo wanapenda.
 
K
Jengeni stendi Kwa sababu ya mahitaji sio kutanua Mji.Mji haukui Kufuata stendi huo ni ujinga wa watu wa Serikali,Mbeya walikataa huo upuuzi wanajenga Old Airport na Mji unaendelea kukua.

Sumbawanga,Iringa nk hakuna mtu anajenga Kufuata stendi matokeo yake stendi hazitumiki hata baada ya kulazimsha watu Kwa sababu wamejemga maporini huko Kwa akili hizo hizo za kukariri eti kutanua Mji.
Husitake kwa 100% Ila kwa kiasi inasaidia,,
 
Tunduru na Masasi ni Wilaya ambazo zinakaribiana japo ziko ndani ya Mikoa miwili tofauti ila Masasi inazidi kukua zaidi, Sasa hivi Masasi wanamiliki Council mbili ambazo ni Masasi District Council & Masasi Town Council.
Mara ya mwisho kupita Masasi ni May 2023.. Duuh Masasi ya sasa ina barabara za lami mitaani, Ile Hospital ya Wilaya Mkomaindo na vyuo ya Afya(Masasi- COTC) vyote vimeboreshwa. Pale sokoni Kaumu Maghorofa yanajengwa. Stand kuu inahamishwa ili kutanua Mji, stand ya kisasa itaanza kujengwa soon.
Masasi pamechangamka kuliko Lindi Municipal
 
Jengeni stendi Kwa sababu ya mahitaji sio kutanua Mji.Mji haukui Kufuata stendi huo ni ujinga wa watu wa Serikali,Mbeya walikataa huo upuuzi wanajenga Old Airport na Mji unaendelea kukua.

Sumbawanga,Iringa nk hakuna mtu anajenga Kufuata stendi matokeo yake stendi hazitumiki hata baada ya kulazimsha watu Kwa sababu wamejemga maporini huko Kwa akili hizo hizo za kukariri eti kutanua Mji.
Kama kuna miji ya kipuuzi isiyoeleweka basi ni Mbeya, hilo jiji sijui lilipangwa vipi tu.
 
Wakuu,

Uzi huu ni kwa ajili ya kutaja miji midogomidogo ndani ya nchi yetu ambayo ina vibe kubwa kama miji mikubwa na ina fursa za kibiashara lakini haivumi wala kujulikana sana na watu.

Mimi naanza kama ifuatavyo:

1. MLOWO
Huu ni miongoni mwa miji midogomidogo inayokuwa kwa Kasi, ni Mji Mdogo unaopatikana Mkoa mpya wa Songwe, Wilaya ya Mbozi. Mji huu upo barabara kuu ya kutoka Mbeya Jiji kuelekea Tunduma. Ni Mji unaokua kwa kasi na unafursa ya kibiashara hasa mazao. Mji huu unazungukwa na vijiji vingii ambavyo wakazi wake wanajishughulisha na kilimo cha Mahindi, karanga, Maharagwe Alizeti, parachichi, kahawa n.k

Mji huu wa Mlowo una pacha/njia ya kuelekea miji mingine kama Kamsamba, Momba na Chunya. Pacha hii ndio pacha inayofika hadi kwenye Shamba kubwa la serikali la mahindi ambalo kwa sasa liko chini ya Wakala wa Mbegu wa Taifa(ASA).

2. MPEMBA
Huu pia ni Mji unaokua kwa kasi, upo mkoani Songwe Wilaya ya Tunduma, kilometers 10 kutoka Tunduma mji. Mji huu una fursa za kibiashara na Kilimo.

3. VWAWA
Hapa ndipo Makao makuu ya Mkoa wa Songwe ambapo kwa sasa Mkuu wa Mkoa huu ni Daniel Chongolo. Ni Mji unaokua kwa kasi kutokana na kusimikwa kwa huduma nyingi za kijamii zenye hadhi ya mkoa. Miaka michache Mji huu utaungana na Mji wa Mlowo kutokana na ukaribu bila kusahau mijengo mikali inayoendelea kuporomoshwa ndani ya Mji huu.
Karibu Vwawa.

4. NYANGAO
Ni Mji unaopatikana Kusini Mashariki mwa Tanzania ndani ya Mkoa wa Lindi, Wilaya ya Lindi DC. Mji huu mkongwe ambao wajerumani waliweka ngome yao hapa na kufanikiwa kujenga kanisa kubwa na Mission yao. Mbali na hilo wajerumani walijenga hospital kubwa sana ndani ya Mji huu(St Walburgus referral Hospital Nyangao).

Wakazi wengi wa Mji huu ni wakulima wa mazao kama Mahindi, mpunga, Alizeti, karanga na mazao ya biashara Kam Ufuta na Korosho, bila kusahau biashara za samaki/dagaa.. ambapo Mji huu umekuwa kama center ya biashara hii ambapo samaki/dagaa wengi wanaotoka bahari ya Kilwa na kuja Nyangao. Watu mbalimbali kutoka katika vijiji vilivyo karibu na Mji wa Nyangao wanakuja kujumua samaki/dagaa hapa.

Kitu lingine Cha kufahamu ni kuwa Mji huu upo mpakani kati ya Mkoa wa Lindi na Mtwara kutokea Masasi Town, Pia ni sehemu ambapo Mbunge wa Mtama na Waziri mwenye dhamana ya habari, masiliano na Teknolojia(Nape Nnaye) huwa anapategemea sana kuchukuwa/kupigiwa kura za kutosha katika chaguzi zinazofanyika, hii ni kutokana na idadi ya watu waliopo Mji huu ambao ni wanachama wa Chama Mapinduzi.

Nyangao kuna shule za level ya juu (High) kama MAHIWA HIGH SCHOOL na NYANGAO HIGH SCHOOL ambayo inasemekana inamilikiwa na Waziri mkuu(Mh : Kassim M Kassim). Ukitaka kufahamu shule hii kwa undani basi fuatilia Zamaradi TV. Pia kuna chuo cha kati cha Afya kilichopo karibu na Hospital ya Nyangao na vyuo vingine vya ufundi.

KIDATU
Mji huu upo ndani Wilaya ya Kilosa japo watu wengi wanachanganya kwa kufahamu kuwa upo wilayani kilombero. Mji huu unakuwa kwa Kasi sana, hii inachagizwa na uwepo wa kiwanda kikubwa Cha sukari almaarufu kama Kilombero Sugar Company. Wakazi wengi wa mji huu ni wakulima hasa Kilimo cha miwa ambapo soko lake kuu la miwa linapatikana katika kiwanda hicho cha sukari. Mji huu una fursa za kibiashara hasa kutokana na wageni wanaokuja kununua sukari kiwandani hapo bila kusahau Crew kubwa ya wataalam kutoka kiwandani hapo.

Kuna chuo kimoja kikongwe sana kinachofahamika kama NATIONAL SUGAR INSTITUTE. Chuo hiki kinatoa kozi mbalimbali za Stashahada ya uhandizi Umeme, Kilimo na Sukari n.k

Pia Mji unahuduma za kibenki na sehemu nyingi za starehe bila kusahau Mji huu umepitiwa na barabara kuu ya kuelekea Mji wa Ifakara.

Karibu Kidatu.

ITAENDELEA...
Hongera sana ndugu Kwa kujaribu kututajia baadhi ya Miji inavyokua Kwa haraka.....naomba nikueleweshe kitu kuhusu KIDATU......katika wilaya ya Kilosa ambayo mimi ni Mzaliwa wa hapo hakuna Mji unaoitwa KIDATU....Bali KIDATU hipo wilaya ya KILOMBERO na si KILOSA....Mji unaousema wewe unaitwa Mji wa RUAHA....huu ni Mji uliopo katika wilaya ya Kilosa na ni mpakani mwa Wilaya ya Kilosa na Kilombero....Mji huu hupo upande wa Wilaya ya Kilosa na Mwi sho wa Mji huu ni KWENYE daraja la Ruaha ambapo pembeni yake upande wa pili wa Wilaya ya KILOMBERO Kuna bwawa kubwa la umeme...( Bwawa la Kidatu)...
Hivyo Mji ambao umeulenga wewe ni Mji wa RUAHA wenye chuo Cha Sukari,,Kiwanda kikubwa Cha Sukari maarufu kama K2,,Kiwanda Cha kutengeneza Sprit,,,na Kiwanda Cha kutengeneza....Mji wa RUAHA maarufu kama Kilombero una Mashamba Makubwa sana ya Miwa...na ni Mji ambao umechangamka saaana....nyumbani Kwao Mecky Maxime kocha wa Hiefu...nyumbani Kwao kabila la Wavidunda....Ruaha ni Kijiji kikubwa sana na chenye uwezo wa kufananishwa ata na Miji baadhi mikubwa
 
Yaani Katoro ije kuipiku Geita? Acha stori za kutunga ,Geita TC ni Kati ya Miji mikubwa 10 ,Kwa Tanzania kwa

Seems Moro Ina Vimiji vidogo vinavyoibukia vingi sana
idadi ya watu.
Yeah Moro ni funga kazi Ina miji midogo mingi yenye mzunguko mkubwa wa hela kuliko baadhi ya mikoa.
Mfano.
Dumila
Mikumi
Ifakara
Mikese
Dakawa
Gairo etc

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Acha ujinga basi..Makambako sio Mji mdogo ni Mji mkubwa na una Halmashauri kabisa.

Lyazumbi,Ndanda,Matai,Lupa,Tinde,Tura hivyo ni Vijijini na Wala havijachangamka Kwa lolote na hakuna vibe.

Laela,Mataifa na Lyazumbi kuna vibe gani hapo? Kwanza hata Inyonga pamepoa watu wanakoboa mipunga tuu,Ungekuwa na akili ungetaja hata Majimoto
Umekuja kutukana au kueleza fursa ?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kagongwa ndiyo kata yenye idadi kubwa ya watu kuliko kata zote za Kahama MC pana harakati nyingi sana pale na barabara ya Kagongwa-Nzega ikitiwa lami maana yake magari Nzega-Kahama hayapita tena Tinde maana ni short cut.

Nkinga-Igunga DC napo pamechangamshwa na uwepo wa ile Hospital.

Didia-Shinyanga DC napo si haba.
 
Sasa kama Iko ndani ya Kahama MC haiqualify kuwa independent town
 
Mku
Hongera sana ndugu Kwa kujaribu kututajia baadhi ya Miji inavyokua Kwa haraka.....naomba nikueleweshe kitu kuhusu KIDATU......katika wilaya ya Kilosa ambayo mimi ni Mzaliwa wa hapo hakuna Mji unaoitwa KIDATU....Bali KIDATU hipo wilaya ya KILOMBERO na si KILOSA....Mji unaousema wewe unaitwa Mji wa RUAHA....huu ni Mji uliopo katika wilaya ya Kilosa na ni mpakani mwa Wilaya ya Kilosa na Kilombero....Mji huu hupo upande wa Wilaya ya Kilosa na Mwi sho wa Mji huu ni KWENYE daraja la Ruaha ambapo pembeni yake upande wa pili wa Wilaya ya KILOMBERO Kuna bwawa kubwa la umeme...( Bwawa la Kidatu)...
Hivyo Mji ambao umeulenga wewe ni Mji wa RUAHA wenye chuo Cha Sukari,,Kiwanda kikubwa Cha Sukari maarufu kama K2,,Kiwanda Cha kutengeneza Sprit,,,na Kiwanda Cha kutengeneza....Mji wa RUAHA maarufu kama Kilombero una Mashamba Makubwa sana ya Miwa...na ni Mji ambao umechangamka saaana....nyumbani Kwao Mecky Maxime kocha wa Hiefu...nyumbani Kwao kabila la Wavidunda....Ruaha ni Kijiji kikubwa sana na chenye uwezo wa kufananishwa ata na Miji baadhi mikubwa
Asante mkuu.
Hili la KIDATU nilishaliweka wazi kuwa ule mji unatumia majina yote mawili japo sijui kwa nini. Mimi Nimeishi pale 2 yrs, So naelewa vizuri. Hata hicho chuo Cha Sukari Cha Taifa kwenye profile zake kinaonesha kuwa kipo KIDATU, yaan ni namna tu watu wanaona inafaa kuita na inaeleweka.
Nakutumia picha hapa ya pale chuoni utaona neno Kidatu kwenye Address
yao na College Joining instructions utakuta hivyo, halikadharika kile kiwa Cha Sukari K2 pia K1, taarifa zao zinazohusu location ya kiwanda huwa wanataja Kidatu
IMG_20191023_183025.jpg
 
Back
Top Bottom