Miji midogo midogo Tanzania ambayo ina vibe na fursa za kibiashara lakini haivumi

Miji midogo midogo Tanzania ambayo ina vibe na fursa za kibiashara lakini haivumi

1. Ndanda
2. Matai
3. Lyanzumbi
4. Rungwa
5. Inyonga
6. Lupa Tinga Tinga
7. Dumila
8.Laela
9. Mangaka
10. Madaba
11. Makambako
12. Tinde
13. Ikwiriri
14. Tura

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Yaaaaaas, Makambako, Mafinga hii miji ambayo ilishajitafuta na sasa ishafika viral. Uwepo wa biashara kuu za mbao, viazi, chai inachochea sana maendeleo kwenye hii miji.
Kwangu Mimi sioni tofauti kati ya mtu anayeishi Mbeya Jiji na mtu wa Mafinga/Makambako.. hawa wote kama maokoto yapo mifukoni basi wanakula Raha zote za miji.
Makambako/Mafinga ni rahisi kwenda sehemu yoyote Tanzania hii maana usafiri ni Masaa yote Mzee hata semi za mbao unadandia..
Kipindi Najitafuta kielimu pale Mafinga Town, likizo nilikuwa napanda sana semi za mbao kuelekea Dar😃

Kuhusu Ndanda,, pale bado kiupande wa Fursa labda kama wewe ni kijana umemaliza kozi za Afya basi teremka pale Ndanda Hospital (Abasia Ndanda)ukaombe kazi.. usikubali kukaa kizembe.
Kipindi Niko pale Mwena-Ndanda weekend nilikuwa natoka na wadau tunaenda kuinjoi Masasi Town...
Jida, Kaumu, Uwanja wa fisi tumeinjoi sana.
 
Wakuu,

Uzi huu ni kwa ajili ya kutaja miji midogomidogo ndani ya nchi yetu ambayo ina vibe kubwa kama miji mikubwa na ina fursa za kibiashara lakini haivumi wala kujulikana sana na watu.

Mimi naanza kama ifuatavyo:

1. MLOWO
Huu ni miongoni mwa miji midogomidogo inayokuwa kwa Kasi, ni Mji Mdogo unaopatikana Mkoa mpya wa Songwe, Wilaya ya Mbozi. Mji huu upo barabara kuu ya kutoka Mbeya Jiji kuelekea Tunduma. Ni Mji unaokua kwa kasi na unafursa ya kibiashara hasa mazao. Mji huu unazungukwa na vijiji vingii ambavyo wakazi wake wanajishughulisha na kilimo cha Mahindi, karanga, Maharagwe Alizeti, parachichi, kahawa n.k

Mji huu wa Mlowo una pacha/njia ya kuelekea miji mingine kama Kamsamba, Momba na Chunya. Pacha hii ndio pacha inayofika hadi kwenye Shamba kubwa la serikali la mahindi ambalo kwa sasa liko chini ya Wakala wa Mbegu wa Taifa(ASA).

2. MPEMBA
Huu pia ni Mji unaokua kwa kasi, upo mkoani Songwe Wilaya ya Tunduma, kilometers 10 kutoka Tunduma mji. Mji huu una fursa za kibiashara na Kilimo.

3. VWAWA
Hapa ndipo Makao makuu ya Mkoa wa Songwe ambapo kwa sasa Mkuu wa Mkoa huu ni Daniel Chongolo. Ni Mji unaokua kwa kasi kutokana na kusimikwa kwa huduma nyingi za kijamii zenye hadhi ya mkoa. Miaka michache Mji huu utaungana na Mji wa Mlowo kutokana na ukaribu bila kusahau mijengo mikali inayoendelea kuporomoshwa ndani ya Mji huu.
Karibu Vwawa.

4. NYANGAO
Ni Mji unaopatikana Kusini Mashariki mwa Tanzania ndani ya Mkoa wa Lindi, Wilaya ya Lindi DC. Mji huu mkongwe ambao wajerumani waliweka ngome yao hapa na kufanikiwa kujenga kanisa kubwa na Mission yao. Mbali na hilo wajerumani walijenga hospital kubwa sana ndani ya Mji huu(St Walburgus referral Hospital Nyangao).

Wakazi wengi wa Mji huu ni wakulima wa mazao kama Mahindi, mpunga, Alizeti, karanga na mazao ya biashara Kam Ufuta na Korosho, bila kusahau biashara za samaki/dagaa.. ambapo Mji huu umekuwa kama center ya biashara hii ambapo samaki/dagaa wengi wanaotoka bahari ya Kilwa na kuja Nyangao. Watu mbalimbali kutoka katika vijiji vilivyo karibu na Mji wa Nyangao wanakuja kujumua samaki/dagaa hapa.

Kitu lingine Cha kufahamu ni kuwa Mji huu upo mpakani kati ya Mkoa wa Lindi na Mtwara kutokea Masasi Town, Pia ni sehemu ambapo Mbunge wa Mtama na Waziri mwenye dhamana ya habari, masiliano na Teknolojia(Nape Nnaye) huwa anapategemea sana kuchukuwa/kupigiwa kura za kutosha katika chaguzi zinazofanyika, hii ni kutokana na idadi ya watu waliopo Mji huu ambao ni wanachama wa Chama Mapinduzi.

Nyangao kuna shule za level ya juu (High) kama MAHIWA HIGH SCHOOL na NYANGAO HIGH SCHOOL ambayo inasemekana inamilikiwa na Waziri mkuu(Mh : Kassim M Kassim). Ukitaka kufahamu shule hii kwa undani basi fuatilia Zamaradi TV. Pia kuna chuo cha kati cha Afya kilichopo karibu na Hospital ya Nyangao na vyuo vingine vya ufundi.

KIDATU
Mji huu upo ndani Wilaya ya Kilosa japo watu wengi wanachanganya kwa kufahamu kuwa upo wilayani kilombero. Mji huu unakuwa kwa Kasi sana, hii inachagizwa na uwepo wa kiwanda kikubwa Cha sukari almaarufu kama Kilombero Sugar Company. Wakazi wengi wa mji huu ni wakulima hasa Kilimo cha miwa ambapo soko lake kuu la miwa linapatikana katika kiwanda hicho cha sukari. Mji huu una fursa za kibiashara hasa kutokana na wageni wanaokuja kununua sukari kiwandani hapo bila kusahau Crew kubwa ya wataalam kutoka kiwandani hapo.

Kuna chuo kimoja kikongwe sana kinachofahamika kama NATIONAL SUGAR INSTITUTE. Chuo hiki kinatoa kozi mbalimbali za Stashahada ya uhandizi Umeme, Kilimo na Sukari n.k

Pia Mji unahuduma za kibenki na sehemu nyingi za starehe bila kusahau Mji huu umepitiwa na barabara kuu ya kuelekea Mji wa Ifakara.

Karibu Kidatu.

ITAENDELEA...
tunawahakikishia watanzania kuwa , tulipotezewa muda sana na mkoa wa mbeya
tunawaahid kuwa miaka kumi mbele tutakuwa sawa na miji mikongwe kama IRINGA mc, kahama, na moshi

na kizuri sisi tuna miji mingi na inakuwa kwa kasi yote
 
Yaaaaaas, Makambako, Mafinga hii miji ambayo ilishajitafuta na sasa ishafika viral. Uwepo wa biashara kuu za mbao, viazi, chai inachochea sana maendeleo kwenye hii miji.
Kwangu Mimi sioni tofauti kati ya mtu anayeishi Mbeya Jiji na mtu wa Mafinga/Makambako.. hawa wote kama maokoto yapo mifukoni basi wanakula Raha zote za miji.
Makambako/Mafinga ni rahisi kwenda sehemu yoyote Tanzania hii maana usafiri ni Masaa yote Mzee hata semi za mbao unadandia..
Kipindi Najitafuta kielimu pale Mafinga Town, likizo nilikuwa napanda sana semi za mbao kuelekea Dar[emoji2]

Kuhusu Ndanda,, pale bado kiupande wa Fursa labda kama wewe ni kijana umemaliza kozi za Afya basi teremka pale Ndanda Hospital (Abasia Ndanda)ukaombe kazi.. usikubali kukaa kizembe.
Kipindi Niko pale Mwena-Ndanda weekend nilikuwa natoka na wadau tunaenda kuinjoi Masasi Town...
Jida, Kaumu, Uwanja wa fisi tumeinjoi sana.
Rudi ukapachunguze vizuri pale

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ukuaji wa miji pekee haitoshi,sisi watu wa Bebezi/Totoz,Je Bebez au Totoz zinaendana na kasi ya ukuaji wa hiyo miji?

Siyo natoka kwangu Dar naelelekea Nyangao huko Mkoani Lindi kwenda kushangaa Minazi na Uvunaji wa Ufuta!
Mkuu pale Nyangao kuna toto za Kimwera, kimakonde, kiyao, kimakuwa.. Je utaziweza..?😃
Omba experience kidogo kwa LIKUD maana anazijuaga ni mzoefu wa maeneo yale Lindi/Mtwara
 
Hapo kwenye Kidatu sio kweli, pale panaitwa Ruaha ni wilaya ya Kilosa. Kidatu ni ukivuka daraja linalotenganisha wilaya ya Kilosa na Kilombero. Kidatu ni Kilombero sio Kilosa. Hata viwanda vya sukari pale viko viwili K1 na K2 kimoja kipo Kilosa kingine kipo Kilombero japokuwa vipo pamoja.
 
Hii miji midogomidogo mingine hebu niitaje tu ili wadau wengine waweze kuifahamu na kama wanahitaji kutafuta/kufuata fursa huko basi wafuate.
• Kibaigwa
• Nanyamba
• Mahuta
• Chimala
• Ikwiriri
• Mangaka
• Nagaga
• Nangurukuru
• Ilula
• Kalenga
• Mlimba
Ikwiriri iko poa sana
 
tunawahakikishia watanzania kuwa , tulipotezewa muda sana na mkoa wa mbeya
tunawaahid kuwa miaka kumi mbele tutakuwa sawa na miji mikongwe kama IRINGA mc, kahama, na moshi

na kizuri sisi tuna miji mingi na inakuwa kwa kasi yote
Sawa , lakin niny wanyiha na wandari ni ndugu zetu Tu.

Hakuna aliyewapotezea muda maana hata Mbeya kuna miji mingi inayokuwa Kwa Kasi.

Mfano Wilaya ya Mbarali peke yake kuna miji Kama mitano au Zaid inakuja vizuri.
1. Ubaruku
2. Rujewa
3. Igawa
4. Chimala
5. Igurusi
6. Mswiswi
 
Wilaya, Miji midogo na centers zinazokua kwa kasi
1. Makongolosi Chunya Mbeya
2. Tinde Shinyanga
3. Runzewe na Nyakanazi
4. Ifunda Iringa
5. Ilula
6. Kibaigwa Dodoma
7. Saza Songwe
8. Busisi Sengerema
9. Isaka Kahama
10. Lupa Chunya
11. Migoli Iringa
12. Mkwajuni Songwe
13. Igawa Mbeya
 
Back
Top Bottom