Miji midogo midogo Tanzania ambayo ina vibe na fursa za kibiashara lakini haivumi

Mwisho wa siku hii nchi sehemu zote zinafanana, ujinga ni ule ule kila mahali!
Labda kwenu ila Tanzania hii kuna sehemu ukipita unaona utofauti sana nilipita kule ubaruku Kwa zile mashine nilizoziona kweli kuna watu wako advanced na wanaelewa nini wanafanya
 
Mimi kwa experience yangu nliushobokea mji wa Katoro kwa story kama hizi za mji wenye fursa nikahama zangu dar, lengo lilikuwa ni kufanya biashara ya nafaka ila muda nilipofika ilikuwa nimepishana na msimu Yani alifika July na mavuno ni April sasa nikapata wazo la kufungua grocery maana huko kuna walevi dar ikasome.. nikachukua eneo pale stendi kuu ya Katoro maboresho kidogo nikatia mzigo.. kilichonikuta ni hatari japo nlifata ethics za biashara niliweka mademu weupe wenye msambwanda, mziki na chakula quality kabisa ila nilikutana na vimbweka sitasahau huo mji watu wanaroga saa moja jioni live bila chenga, mademu weupe wasukuma wanawaoa kwa gharama yoyote Yani bado wanakopesha plus wateja wakawa kama umeme wa TANESCO nikaona nirudi mjini huko wanaoweza kutusua ni wasukuma au wafanyabishara wa madini na wenye mitaji mikubwa ila milioni 5 kushuka chini unachoma pesa yako
 
kwa nini ulienda bila kufanya na wewe utafiti wako kidogo
 
Unapajua vinzuri kidatu kile kiwanda kinaitwa illovo nimeishi kwa baba yangu mdogo anafahamika kwa jina la matungira,miaka ile ya 2012 nikasoma udereva kwenye chuo hicho kipindi hicho nilikuwa nalima mboga na kufunga nguruwe daah umenikumbusha mbali sana,baba mdogo anapakana na mzee mmoja maarafu sana alikuwa mbunge pia ana mtoto wake anaimba singeli anaitwa dragon
 
Mkwajuni unaweza paelezea kidogo, kuhusu fursq zake na jamii husika kiujumla, vipi mzunguko unategeme nn zaid?
Uvuvi kutoka ziwa Rukwa, kilimo ktk bonde la Ziwa Rukwa, biashara, uchimbaji madini (dhahabu-japo si sana).
 
Napajua vizuri mkuu, Illovo moja hiyo.. kule K1 kuna Hospital ya kiwanda kabisa,, ni nzuri sana
 
Kweli... katoro inapewa sana promo ila kiukweli kibiashara bado sana, huwezi amini serengeti walifungua depot yao katoro mwisho wa siku waliifunga kutokana na wana katoro sio wanywaji wa bia kiviiile wenyewe wamezoea pombe za bei rahisi
 
Bila kuisahau katoro-Geita! Alaf mleta uzi umesema kidatu/ruaha ipo kilosa lakini sio kweli hyo ipo wilay ya kilombero hat ukiangalia google map, alfu tunduma sio wilaya hyo ni wilaya ya Momba.
 
Aiseeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…