Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Daaaah.. kwahyo ulishamtea KOHOZI la kiutu uzima😅😅Ni Tonia halisi
Ndio ndio mkuu walishindwa kujizuiaMaana yake Kaka na Dada walizalishana
Mzee hujawahi kusikia Mtoto kuzaa na Mama yake Mzazi?Na hapo bado kuna story kubwa sana, inakuwaje unazaa na dada yako hata kuficha inashindikana mtoto unakaa naye wewe tena na mke wako halisi sasa [emoji3064][emoji3064][emoji3064]
😂😂😂Rafiki kwio😐
Hii inawezekana kweli?Mzee hujawahi kusikia Mtoto kuzaa na Mama yake Mzazi?
now yupo wapi au ndio mkeSimsapoti ...ilitukia na matunda ya mshua nikayashudia labda nikayachuma pia
Jibu tu mkuu.. nataka nikupongeze bao lako uliliacha panapostahiliAcha ufala babaa😂
Ok mkuuHili naomba nisikujibu mkuu.
Duh! [emoji848]2. MKASA WA PILI;
Ilipita kama mwaka mmoja wa kutokuwa pamoja na Tonia...
(usiniukize sababu) nilikutana na mrembo mwingine
jina lake Vick..sio jina halisi.
Huyu Vick kwa kweli naye hana deni na Muumba
kwani amekamilika kila idara.
Yaani yeye na Tonia huenda uumbaji wao ulifanyika
alfajiri wakati muumbaji ana ari, nguvu na ubunifu huku
akili ikiwa imejaa utashi wa kufyatua vitu vya mfano.
Huyu Vick nilifahamiana naye kazini kwake kwani mimi nilikuwa
mteja wake katika biashara yake nzuri tu.
Kama ujuavyo ubinadamu una mahitaji yake yasiyopingika
hata uwe nani katika dunia hii ya Mungu.
Siku isiyokuwa na jina...japo ninaikumbuka[emoji1][emoji1][emoji1]
Tukajikuta tumekuwa marafiki wa kukata na shoka japo bond
haikuwa kama ya Tonia...Vick hakuwa mtu wa kupata nafasi
ya kutosha kuonana nami bali tuliweza kukaa pamoja
mara chache sana katika mwezi.
Kuna siku tulikuwa tunapiga stori za familia zetu.
Nikamuuliza hivi mbona katika mazungumzo yetu huwa unamtaja
baba tu na sijawahi kuona umposti wala kumzungumzia mama?
Baada ya swali hilo ghafla Vick alibadilika ghafla na kujaa huzuni.
Nikamuuliza mbona umeshtuka sana Vick wangu?.
Ndipo alipofunguka na kusema.
Glenn; bila shaka umehisi nilifiwa na mama yangu, hasha.
Mama yangu ni mzima wa afya na Jumapili ijayo ninaweza
kwenda kumtembelea wilaya flani.
Lakini kuna mkasa mzito ulionifanya mimi na mdogo wangu
kukosa upendo na mama yetu mazazi.
Baba yetu ndiye baba na mama kwetu kwakweli.
Nikamuuliza hili linawezekana je Vick?
Ndipo aliposema; Baba yetu alizaa na mama yetu
alipokuwa kidato cha pili.
Baada ya baba kufikia kidato cha 4 aliamua amzalishe
mama tena ili amfanye asiondoke kwa bibi amsubirie amalizie
masomo yake ili waje kuungana pamoja kama mke na mume.
Lakini cha kushangaza mdogo wangu akiwa na miezi 3,
mama alikutana na
Mtu aliyekuwa mpenzi wake kabla ya baba hivyo walianza
uhusiano wao upya na mama alitoroka na kwenda kuishi
na huyo.
Huko alipoolewa hakumweleza huyo mume wake kuwa aliwahi kuzaa.
Ulifika wakati baada ya miaka kadhaa huyo mume wake
alipata fununu kuwa mama yetu alizaa na mwanaume
mwingine lakini alipoulizwa alikana katu katu kuwa yeye
hajawahi kuzaa na hana watoto.
Glenn baba yetu alipitia wakati mgumu mno baada ya
mama yetu kutoroka.
Kuna wakati alilazimika kutokuendelea na kidato cha 5
ili atulee kwa kushirikiana na bibi kwani umri wa bibi ulisonga sana.
Baba alibahatika kupata kazi katika shirika flani binafsi.
Kuna wakati alilazimika kwenda nasi kazini alipokosa
mahali pa kutuacha.
Mama yetu alikuja kututafuta baada ya miaka 22 kupita na
kilichomsababisha atutafute ni baada ya mume wake
kuachishwa kazi yake nzuri na kuwa mlevi kupindukia.
Hivyo mama alitutafuta baada ya kusikia sisi na mdogo
wetu na baba yetu kipenzi kuwa tumefanikiwa kimaisha.
Lakini pamoja na kumfahamu mama kuna nyakati najuta
kumfahamu kwani ni mtu asiye na shukrani.
Tunajitahidi kumsaidia lakini amejaa lawama anaona
kama hatufanyi anavyotamani tumsaidie..
Mikasa ya kuskitisha we unacheka.. una nn lakn
Kilichotokea ni kwamba mtoto(first born) alimrithi mama baada ya kifo cha mshua na akafanikiwa kuzaa mtoto wa kike ambaye ni mtoto dada na baadae akapata wajukuu wapwa😄😄Hii inawezekana kweli?