Buddy
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 7,117
- 8,885
Game on ... Andreescu vs Selena ... hii game tough kwa wote.Katika mchezo sitaki unipite katika hatua hii ya nusu fainali basi ni huo wa Elina Svitolina Vs Serena Williams. Nitafanya juu chini inimla mchezo huu niutizame, ni mchezo utako vutia sana tena wenye kusisimua. Hivyo sito penda unipite maana bingwa mwenyewe atatoka hapo.
Binafsi sikumpa nafasi ata kidogo Naomi Osaka kanyakua ubingwa huu, Osaka amekuwa akisumbuliwa na majeraha toka alipo chukua ubingwa wa Australian Open. Toka hapo amekuwa akisumbuliwa na majeraha sana hivyo sikuona nafasi kwake kwa michuano hii, ata mchezo wake wa mwisho katika michuano hii alitolewa baada ya kupata maumivu ya mgongo.
Mwanadada Barty ndio nilimpa nafasi ya kwanza kunyakua ubingwa huu, namba mbili nilimpa Serena Williams na namba tatu nikampa shemeji yangu Elina Svitolina. Kwanini Barty? Barty amekuwa kwenye kiwango bora kabisa toka amechukua ubingwa wa French Open (Roland Gatos), ikumbukwe kuwa Barty alikuwa akicheza mchezo wa Golf hapo kabla. Hivyo akaona kule hakueleweki akaamia kwenye tennis.
Kwa wanaume nilimpa nafasi Roger Federer, Rafael Nadal kisha Medvedev. Djokovick sikumpa nafasi sababu nilivyo ona ile draft la michuano mpaka robo fainali ilikuwa inawakutanisha Djokovick na Medvedev niliamini kabisa Djokovick asinge toka salama kwa Medvedev.
Kwahiyo utabiri wangu naona umeenda vizuri, naima kubwa kuwa fainali ya wanaume itwakutanisha Daniil Medvedev Vs Rafael Nadal. Aisee itakuwa bonge la fainali hasa ukizingatia hii itakuwa fainali ya pili mfululizo wanakutana kwa mwaka huu huku ya kwanza ikiwa ile iliyowakutanisha kule Montreal, Canada Agosti 11, 2019. Fainali hiyo Medvedev alichezea kichapo, hivyo wakikutana atataka kulipiza kisasi. Ndio maana mimi nataka kujilipua na 300k katika mkeka huu chini mapema kabisa. View attachment 1199228
Namkubali sn Andreescu baada amya Svitolina kutolewa. Nategemea atapata japo set 1.