Hapa hapa naomba kuuliza swali kwamfano mm leo nimebet
Panthrakikos vs Ael kallon
Kukawa na point za namna hii
1-1 2-1 2-2 1-x 2-x x-x
1-1 1-2 2-2 x-1 x-2 x-x
Sasa hapo nashindwa kuelewa unachaguaje ili uweze kuibuka mshindi katika hizo timu mbil hapo naomben maelezo ya kina hapa swali jingine je hiyo n idadi ya magoli ama inawakilisha kitu gani
Maelezo ni kama ifuatavyo:
(A) 1/1-Mwenyeji ashinde mechi mwanzo mwisho(lazima apate goli kipindi cha kwanza,cha pili sio lazima).
(B) 2/1-Mgeni aongoze kipindi cha kwanza,mwenyeji aje achomoe kipindi cha pili aongeze goli jingine ashinde mechi.
(C) 2/2-ni kama hapo juu (A) lkn kwa mgeni
(D) 1/x-Mwenyeji aongoze kipindi cha kwanza,mgeni aje achomoe kipindi cha pili game iishe sare
(E) 2/x-Ni kama hapo juu (D) ila kwa mgeni aongoze kipindi cha kwanza,mwenyeji aje achomoe kipindi cha pili,game iishe sare.
(F) x/x- Hiyo ni sare mwanzo mwisho(vipindi vyote viwili)
(G) 1/2-Ni kama hapo juu (B) lakini kwa mwenyeji
(H) x/1-Sare kipindi cha kwanza,mwenyeji ashinde kipindi cha pili
(I)x/2-sare kipindi cha kwanza,mgeni ashinde kipindi cha pili.
Hivyo,kwa timu zako hapo juu;
Mwenyeji ni Panthrakikos na Mgeni ni Ael kallon.
ALL THE BEST