demigod
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 8,292
- 15,250
Ahsante mkuu sergey. Mimi huwa nafanya betting kupitia premier betting, hizi salama Mara nyingi inakuwa +1. Swali linakuja hivi. Mfano mechi ya Leo man u vs cambridge . Cambridge kapewa +1 nikiweka handicap kuwa man atashinda, na akashinda 2-0 hapo handcap imekubali?
Handcap ni aina ya mchezo, wala si aina ya matokeo.
Kama ulichagua hiyo mechi kuisha kwa Suluhu basi mechi hiyo utakuwa imepoteza, kwa sababu mwisho wa mechi man u atakuwa na goli 2 na Cambridge atakuwa na goli 1.
Kama ulichagua hiyo mechi kuisha kwa man u kushinda basi utakuwa imepatia, kwa sababu mwisho wa mchezo man u atakuwa na goli 2 na Cambridge atakuwa na goli 1.
Kama ulichagua hiyo mechi kuisha kwa Cambridge kuibuka Mshindi basi hiyo mechi utakuwa umepoteza. Kwa sababu mwisho wa mechi man u atakuwa na goli 2 na Cambridge goli 1.
Kumbuka +1 ni goli la kufikirika tu, hata kama hajafunga hilo goli katika mechi yenyewe.
+1 ni goli la kufikirika katika ulimwengu wa GAMBLING.
Last edited by a moderator: