Wakuu nawakumbusha.
Maswali mengi ambayo watu wa ku-Bet huwa tunajiuliza ni
1. Kuna Website ambayo ina Tabiri Mechi zote kwa uhakika wa Asilimia 100%?
2. Je, Kuna App ambayo Inakupatia Utabiri wa Mechi kwa 100%?
3. Je haya Matangazo ya VIP BETTING TIPS, TELEGRAM, Whatsapp Ni Ya Kweli kwa Asilimia 100?
Ukweli ni kuwa HAKUNA. Betting ni all ABOUT PROBABILITY, TAKING CHANCES, TAKING RISK na Kufuatilia mienendo ya TIMU.
Katika Ulimwengu wa Kubet kwa sasa, Kuna Makundi 2. Kundi la Kwanza Wanao taka Kumpasua Kanji (Wengi wetu), Na Kundi La Pili ni Hawa Wanao taka KUTUPASUA SISI ambao Tunamsaka KANJI Kwa Udi na Uvumba. Ndio Wanajiita VIP BETTING TIPS, Apps na Websites Mbalimbali. Ni kama WAGANGA wa Kienyeji [emoji28]
Kama Mganga wa Kienyeji anaweza kukufanya wewe uwe BILLIONEA kwanini Asijifanyie Yeye aaache KAZI YA UGANGA WA JADI [emoji28], Kama Mtu anakutaka ULIPIE HELA KUKUPA ODDS za Uhakika, Kwanini Hiyo Nguvu anayo tumia kujitangaza asiitumie Katika Kubet kwa Kutumia hizo hizo ODDS anazo kupatia WEWE? Amkeni Hakuna Kitu kama Hicho. Tuache kupoteza HELA
USHAURI WANGU, KAMWE USIJIUNGE NA MAGROUP YANAYO UZA ODDS