Ifuatayo ndiyo orodha ya mikoa 10 bora ambayo :
Ambapo binafsi nimeipangilia kwa kuangalia
- Upatikanaji wa chakula
- Urahisi wa Usafiri
- Elimu
- Hali ya Hewa
- Huduma za maji
- Mitandao ya simu
- Usalama
- Biashara
1. Dar es Salaam
Ndiyo mkoa ulioendelea Tanzania kuliko yote.
17% ya watanzania wapo katika mkoa huu...Biashara yako ikikubalika mkoani hapa ujue nchi nzima imekukubali.
Shida pekee ya Dar ni hali ya hewa yake kuwa joto kali.
Pesa yako itakufanya uishi maisha ya kifahari ama ukaishi sehemu duni.
2. Mwanza
Unaukaribia mkoa wa Dar kwa kila sifa tajwa hapo juu. Ukiwa hapa,unakuwa karibu Kenya na Uganda.
Wingi wa vyuo,uwepo wa maji na huduma za hospitali.
3. Mbeya
Mkoa wenye utajiri wa chakula ,hali ya hewa ya kuvutia na upatikanaji rahisi wa huduma za elimu na afya.
Mita inatiririsha maji kila kona.
Shida ya huu mkoa ni usalama finyu barabarani (una ajali za kutosha).
Pia usalama finyu majira ya usiku wa manane....una Viji matukio flani hivi ya kibabe.
4. Iringa
unafuu katika chakula,una shule za kutosha na vyuo.
Shughuli za Biashara za kilimo na Mbao.
Huduma za afya nzuri zipo mijini, na nyingine zinafutwa Mbeya au Dodoma.
5. Arusha
Mkoa wenye moja ya majiji makubwa hapa nchini.Una wingi wa Hospitali, Makazi,Shule na Vyuo.
Ila gharama ya chakula katika huu mkoa ni kubwa mno.
Na hata kwenye ujenzi ,gharama ni kubwa sana
Pia kuna shida ya upatikanaji wa huduma za maji. na kuna baadhi ya maeneo katika huu mkoa ni kame.
6. Ruvuma
Huu mkoa una wingi wa chakula na bei nzuri.Una biashara na nchi jirani.Maji na umeme siyo shida.
Ila bado hakuna barabara za kutosha,upungufu wa vyuo
7. Kilimanjaro
Upo juu kwenye kiwango cha elimu na ubora wa elimu. Una huduma nzuri za afya na maji.Mzuri kwa biashara za utalii.
Ila kuna ugumu wa kupata ardhi kwa baadhi ya Wilaya, Gharama ya vyakula.
8. Dodoma
Ukiondoa Wilaya ya Dodoma ambayo kuna uboreshaji wa miundombinu kwa halia ya juu,na ujenzi wa kutosha tena wenye kupangika.
Lakini nje na hapo kuna shida ya maji,ardhi kame.
9. Njombe
Unataka biashara ya mbao,Viazi,Parachichi au Viazi nenda kwenye huu mkoa. Bado una ardhi ya kutosha ,una hali ya hewa nzuri.
Bado kuna uchache wa shule na huduma za afya.
una kiwango kikubwa cha maambukizi ya Ukimwi.
10. Unguja
Kupo vizuri kwa biashara,kuna vyuo vya kutosha na huduma za afya.
Barabara na huduma za maji.
Ila
Kwa mtu wa bara atapata ugumu kwenye
- Aina za vyakula
- Udini
- Uhitaji wa vitambulisho
- Leseni ya udereva kutokukubaliwa
- Kubaguliwa kwenye baadhi ya huduma.
NOTES
Mikoa ambayo sijawahi fika ni Katavi,Mtwara,Geita,Rukwa,Mara,Pemba na Kigoma.
Mpangilio kulingana na niliyo yaona katika mikoa husika.
Unaweza weka orodha yako.