Mikoa 10 bora ya kuishi Tanzania

Mikoa 10 bora ya kuishi Tanzania

Wewe bado hujakaa Arusha wewe. Yani Arusha hakuna maji? Chakula gharama? Yani ilitakiwa Arusha ndio iwe ya kwanza. Dar inaongoza kwa wingi wa watu na mzunguko wa pesa basi. Vingine vyote ni kizungumkuti. Maji shida, usafiri tabu, joto kama tanuru, we mzima kweli kichwani?
Arusha nilikaa Sakina na nikaa Moshono pale njia Ng'ombe...
Kwa mkoa ambao una jihusisha na Kilimo pia na ufugaji....haiwezekani gharama ya chakula ikawa sawa na Dar...
  • Barabara nyingi ni kuwekwa Moram kuliko rami,Vumbi mwanzo mwisho
  • Stendi yenu ni Haibu,yani hata ya Kibaha kubwa.
  • Uwanja wa ndege ni haibu
  • Usafiri wa umma kuna maeneo saa 4 hakuna
  • Jiji pekee lenye kutumia vipanya kwenye usafiri mpaka sasa.

Aya sasa nenda Wilaya za Monduli na Longido....
Ndiyo utajua shida za maji katika huo mkoa....
Kweli ukae na kuilinganisha Arusha na Dar...!
mentality ya Chugga ni nchi ndiyo ina waharibu....
 
Mzee ingia youtube andika mafuriko karatu ujionee maana mimi siwezi kuandika aya ndefu kitu ambacho hata kwenye vyombo vya habari walionyesha
Mi siyo Fan wa Arusha kiivyo,,,
Ila kwenye ukweli utazungumzwa....
Ni nadra sana kwa hali ya namna hiyo kutokea....
Sehemu prone kwa mafuriko nchi hii zajulikana na Arusha si mojawapo....
 
Arusha nilikaa Sakina na nikaa Moshono pale njia Ng'ombe...
Kwa mkoa ambao una jihusisha na Kilimo pia na ufugaji....haiwezekani gharama ya chakula ikawa sawa na Dar...
  • Barabara nyingi ni kuwekwa Moram kuliko rami,Vumbi mwanzo mwisho
  • Stendi yenu ni Haibu,yani hata ya Kibaha kubwa.
  • Uwanja wa ndege ni haibu
  • Usafiri wa umma kuna maeneo saa 4 hakuna
  • Jiji pekee lenye kutumia vipanya kwenye usafiri mpaka sasa.

Aya sasa nenda Wilaya za Monduli na Longido....
Ndiyo utajua shida za maji katika huo mkoa....
Kweli ukae na kuilinganisha Arusha na Dar...!
mentality ya Chugga ni nchi ndiyo ina waharibu....
We umefika ukonga na chanika? Mbande? Tandale. We mimi ninaishi dar. Yani kama sio shughuli, nikipata mzigo wa maana, naenda kuishi Arusha, wala sio kipengele. Maji ni shida hatari.
 
Kama unataka hela fanya kazi na watu wa Dar es salaam , au mikoa ya kaskazin hasa Kilimanjaro na Arusha hawa watu hawana bambamba, wamenyooka Sana , mikoa mingine wanaunga unga sana
Wewe mpaka leo unaamini watu wa Kaskazini tu ndo wanafanya biashara? Endelea kuwa na akili hizo za miaka ya 90 huko!
Yaani maeneo kama Mwanza,Kahama,Mbeya Iringa,Morogoro kwako hawajui biashara?
 
Ifuatayo ndiyo orodha ya mikoa 10 bora ambayo :
Ambapo binafsi nimeipangilia kwa kuangalia
  • Upatikanaji wa chakula
  • Urahisi wa Usafiri
  • Elimu
  • Hali ya Hewa
  • Huduma za maji
  • Mitandao ya simu
  • Usalama
  • Biashara
1. Dar es Salaam
Ndiyo mkoa ulioendelea Tanzania kuliko yote.
17% ya watanzania wapo katika mkoa huu...Biashara yako ikikubalika mkoani hapa ujue nchi nzima imekukubali.
Shida pekee ya Dar ni hali ya hewa yake kuwa joto kali.
Pesa yako itakufanya uishi maisha ya kifahari ama ukaishi sehemu duni.

2. Mwanza
Unaukaribia mkoa wa Dar kwa kila sifa tajwa hapo juu. Ukiwa hapa,unakuwa karibu Kenya na Uganda.
Wingi wa vyuo,uwepo wa maji na huduma za hospitali.

3. Mbeya
Mkoa wenye utajiri wa chakula ,hali ya hewa ya kuvutia na upatikanaji rahisi wa huduma za elimu na afya.
Mita inatiririsha maji kila kona.
Shida ya huu mkoa ni usalama finyu barabarani (una ajali za kutosha).
Pia usalama finyu majira ya usiku wa manane....una Viji matukio flani hivi ya kibabe.

4. Iringa
unafuu katika chakula,una shule za kutosha na vyuo.
Shughuli za Biashara za kilimo na Mbao.
Huduma za afya nzuri zipo mijini, na nyingine zinafutwa Mbeya au Dodoma.

5. Arusha
Mkoa wenye moja ya majiji makubwa hapa nchini.Una wingi wa Hospitali, Makazi,Shule na Vyuo.
Ila gharama ya chakula katika huu mkoa ni kubwa mno.
Na hata kwenye ujenzi ,gharama ni kubwa sana
Pia kuna shida ya upatikanaji wa huduma za maji. na kuna baadhi ya maeneo katika huu mkoa ni kame.

6. Ruvuma
Huu mkoa una wingi wa chakula na bei nzuri.Una biashara na nchi jirani.Maji na umeme siyo shida.
Ila bado hakuna barabara za kutosha,upungufu wa vyuo

7. Kilimanjaro
Upo juu kwenye kiwango cha elimu na ubora wa elimu. Una huduma nzuri za afya na maji.Mzuri kwa biashara za utalii.
Ila kuna ugumu wa kupata ardhi kwa baadhi ya Wilaya, Gharama ya vyakula.

8. Dodoma
Ukiondoa Wilaya ya Dodoma ambayo kuna uboreshaji wa miundombinu kwa halia ya juu,na ujenzi wa kutosha tena wenye kupangika.
Lakini nje na hapo kuna shida ya maji,ardhi kame.

9. Njombe
Unataka biashara ya mbao,Viazi,Parachichi au Viazi nenda kwenye huu mkoa. Bado una ardhi ya kutosha ,una hali ya hewa nzuri.
Bado kuna uchache wa shule na huduma za afya.
una kiwango kikubwa cha maambukizi ya Ukimwi.

10. Unguja
Kupo vizuri kwa biashara,kuna vyuo vya kutosha na huduma za afya.
Barabara na huduma za maji.
Ila
Kwa mtu wa bara atapata ugumu kwenye
  • Aina za vyakula
  • Udini
  • Uhitaji wa vitambulisho
  • Leseni ya udereva kutokukubaliwa
  • Kubaguliwa kwenye baadhi ya huduma.

NOTES
Mikoa ambayo sijawahi fika ni Katavi,Mtwara,Geita,Rukwa,Mara,Pemba na Kigoma.
Mpangilio kulingana na niliyo yaona katika mikoa husika.
Unaweza weka orodha yako.
DSM umechemka
 
Vipi kuhusu bei ya vyakula kwa mikoa uliyoitaja!!!
 
1. Dar es Salaam
Ndiyo mkoa ulioendelea Tanzania kuliko yote.
17% ya watanzania wapo katika mkoa huu...Biashara yako ikikubalika mkoani hapa ujue nchi nzima imekukubali.
Shida pekee ya Dar ni hali ya hewa yake kuwa joto kali.
Pesa yako itakufanya uishi maisha ya kifahari ama ukaishi sehemu duni.
Kuna baadhi ya watu hawalisikii hilo joto. Mfano, ofinisi AC, garibinafsi AC, nyumbani AC, nyumba ya Ibada AC, supermarket AC, etc.
 
DSM umechemka
Sawa,
kwenye vipengele vipi Dar ipo nyuma...
Wewe mpaka leo unaamini watu wa Kaskazini tu ndo wanafanya biashara? Endelea kuwa na akili hizo za miaka ya 90 huko!
Yaani maeneo kama Mwanza,Kahama,Mbeya Iringa,Morogoro kwako hawajui biashara?
Siku akifika Kahama atashangaa...
 
Arusha nilikaa Sakina na nikaa Moshono pale njia Ng'ombe...
Kwa mkoa ambao una jihusisha na Kilimo pia na ufugaji....haiwezekani gharama ya chakula ikawa sawa na Dar...
  • Barabara nyingi ni kuwekwa Moram kuliko rami,Vumbi mwanzo mwisho
  • Stendi yenu ni Haibu,yani hata ya Kibaha kubwa.
  • Uwanja wa ndege ni haibu
  • Usafiri wa umma kuna maeneo saa 4 hakuna
  • Jiji pekee lenye kutumia vipanya kwenye usafiri mpaka sasa.

Aya sasa nenda Wilaya za Monduli na Longido....
Ndiyo utajua shida za maji katika huo mkoa....
Kweli ukae na kuilinganisha Arusha na Dar...!
mentality ya Chugga ni nchi ndiyo ina waharibu....
Chuggastan babaake!!
 
We umefika ukonga na chanika? Mbande? Tandale. We mimi ninaishi dar. Yani kama sio shughuli, nikipata mzigo wa maana, naenda kuishi Arusha, wala sio kipengele. Maji ni shida hatari.
Mkuu
Kuanzia Kata ya Pugu ,Pugu Kajiungeni,Majohe,Buyuni,Chanika,Msongola a,Zingiziwa,Mvuti hadi Mbade...
Kuna Visima binafsi zaidi ya 1,000...
Tena watu wanachota maji bure....
Mimi nakaa Kigezi kata ya Buyuni...
shida ipi ya maji ipo Chanika...

Jake wewe ushafika Ketumbeine na Longido mjini mkoani Arusha? ...uone palivyo na balaa la ukame na Joto....
Wamasai wanatembea Km zaidi ya 10,just kumfikisha mtoto hospitali...
 
2011 Nipo Mbeya mjini,,,
Mvua kubwa ilipiga, mazao yalisombwa na maji...na Kuna walisombwa na maji kule ikuti,maiti zao zikaenda kuopolewa pale kwenye karakana ya Tazara karibia na kota zao.
Sawa ila Dar ni hatarishi.Kama walikuwa mabondeni ulitaka wasisombwe na maji? Dar Iko bondeni ,Dar kama Kigamboni tambarare maji hayatoki yaani ni majanga tupu.kuishi huko.
 
Back
Top Bottom