Mikoa 10 bora ya kuishi Tanzania

Mikoa 10 bora ya kuishi Tanzania

Kama unataka hela fanya kazi na watu wa Dar es salaam , au mikoa ya kaskazin hasa Kilimanjaro na Arusha hawa watu hawana bambamba, wamenyooka Sana , mikoa mingine wanaunga unga sana
Kilimanjaro enyewe wanalia shida nkafanye nao kazi tena budder hizi story kwa mtu ambae hajawah kanyaga anga hzo ndio atadanganyka.

Pambana popote pale kama ni kutoboa utatoboa tu.
 
Napambana nkaishi Mwanza, Mungu anisaidie nitimize napakubali sana licha ya miundombinu mibovu ila 🙌

NB:Mwanza, Arusha,Kahama, Morogoro are the best for me.
 
Nafkiri bado haujajua matukio ya Kanda ya Ziwa....Sumbawanga ni jina ...
Ila kuna maeneo ni watabe...
Hv huko KandaYaNyonyo huwa nyie mnafanywa nn jmn 😁 mbona mm ndio huko ndio shega sasa, dream yangu nkaish Mwanza na I'm huko ndio yatakuwa makazi sio hii Dodoma
 
Wewe bado hujakaa Arusha wewe. Yani Arusha hakuna maji? Chakula gharama? Yani ilitakiwa Arusha ndio iwe ya kwanza. Dar inaongoza kwa wingi wa watu na mzunguko wa pesa basi. Vingine vyote ni kizungumkuti. Maji shida, usafiri tabu, joto kama tanuru, we mzima kweli kichwani?
We umedata kweli.
Arusha nimefika moshono vyakula bei we jamaa.
Dar es salaam unaweza ishi kwa 5k Arusha ili ule ushibe ni zaidi ya 10k.
Umewahi ishi Kigamboni!?
Maji bwerere kila kitu bei rahisi.
Umewahi fika Manzese?
Hadi nazi ya 300 unapimiwa.
Unafananishaje kwa maisha Dar na Arusha!?
Embu kuwa serious Arusha MAISHA BEI GHALI SAAANAAA.
 
Halafu mleta mada unaweka dodoma unasahau morogoro na mara kweli?
Mara sijaiorodhesha kwasababu sijawahi fika kabisa.....ila hata data zake hadhiridhishi japo ndipo kwa wakwe.
Morogoro shida ipo kwenye miundombinu ya barabara na mawasiliano....
Yani kuna Wilaya ndani ya Morogoro kufikika ni kipengele....
 
Mbeya upatikanaji wa maji ni changamoto kubwa, miuondombinu mibovu, hali za nyumba ni duni, kipindi cha kiangazi vumbi huwa ni kubwa sana. Kwa ufupi Mbeya ni Mkoa mbaya sana kuishi.
 
We umefika ukonga na chanika? Mbande? Tandale. We mimi ninaishi dar. Yani kama sio shughuli, nikipata mzigo wa maana, naenda kuishi Arusha, wala sio kipengele. Maji ni shida hatari.
Mbande ipi unayosemea wewe maji shida!?
Chanika ipi unayosemea wewe hali ngumu?
Maana Zingiziwa hadi vyakula bei rahisi,usisahau Mbande kuna soko kubwa watu hununua vitu hadi wanaotoka Mbagala rangi 3.
Kaishi Temeke Mtongani,Tandika,Manzese,Kigamboni,Azizi Ally,Sinza,Kongowe,Mbagala yote,Buza,Mwanagati kesha urudi hapa.
 
Wewe mpaka leo unaamini watu wa Kaskazini tu ndo wanafanya biashara? Endelea kuwa na akili hizo za miaka ya 90 huko!
Yaani maeneo kama Mwanza,Kahama,Mbeya Iringa,Morogoro kwako hawajui biashara?
Ajabu yeye mwenyew hayupo huko Kaskazin na hafanyi kazi na hao watu wa huko 😁 anachofanya hapa ni kujifariji tu
 
We umedata kweli.
Arusha nimefika moshono vyakula bei we jamaa.
Dar es salaam unaweza ishi kwa 5k Arusha ili ule ushibe ni zaidi ya 10k.
Umewahi ishi Kigamboni!?
Maji bwerere kila kitu bei rahisi.
Umewahi fika Manzese?
Hadi nazi ya 300 unapimiwa.
Unafananishaje kwa maisha Dar na Arusha!?
Embu kuwa serious Arusha MAISHA BEI GHALI SAAANAAA.
Acha uongo. Kote nimeishi eti kigamboni maji bwerere. Tuangalie na quality ya foods. Dar ni malaplap ma matakataka mnakula. Nyama za hovyo, makuku ya hovyo yani in short quality ni zero. Viazi ya hovyo, anything you name. Poor quality of life ipo Dar. Ndio maana wageni wengi wanaishia kuweka makazi Arusha na sio Dar for your info.
 
Mbande ipi unayosemea wewe maji shida!?
Chanika ipi unayosemea wewe hali ngumu?
Maana Zingiziwa hadi vyakula bei rahisi,usisahau Mbande kuna soko kubwa watu hununua vitu hadi wanaotoka Mbagala rangi 3.
Kaishi Temeke Mtongani,Tandika,Manzese,Kigamboni,Azizi Ally,Sinza,Kongowe,Mbagala yote,Buza,Mwanagati kesha urudi hapa.
Kote huko hakuna la maana. Dar ni Upanga, mikocheni, msasani , o bay , na mbezi. Kwingine ni jehanam na nusu
 
Acha uongo. Kote nimeishi eti kigamboni maji bwerere. Tuangalie na quality ya foods. Dar ni malaplap ma matakataka mnakula. Nyama za hovyo, makuku ya hovyo yani in short quality ni zero. Viazi ya hovyo, anything you name. Poor quality of life ipo Dar. Ndio maana wageni wengi wanaishia kuweka makazi Arusha na sio Dar for your info.
We hukuishi Dar umepita Dar.
Sema Kigamboni ipi ina shida ya maji.
Maana hata mwaka juzi na jana kulivyokua na ukame Kigamboni ndio imetumika kusambaza maji Dar es salaam maeneo ambayo maji yalikua shida.
Kigamboni ina visima vingi binafsi na vya serikali pia.
Kipindi cha ukame ni Kigamboni pekeyake haikupata hadha ya maji pamoja na Temeke yote.
Vyakula kula kulingana na pesa yako huwenda labda wewe pesa huna.
Nenda Tandika na Stereo kuna mabanda ya kuku wa kizungu na wa kienyeji,wakizungu bei 7000 mzima wa kienyeji 18k mpk 20k.
Pia ukitaka vipande wanakukatia huyo wa kienyeji.
Mchele unaoliwa Dar ndio unaoliwa sehemu zingine maana Dar hawalimi halkadhalika nyanya na viungo vingine.
Mboga za majani Kigamboni kuna bustani kibao wanalima bila madawa.
DAR HUKUKAA WEWE UMEPITA TU.
 
Mbeya upatikanaji wa maji ni changamoto kubwa, miuondombinu mibovu, hali za nyumba ni duni, kipindi cha kiangazi vumbi huwa ni kubwa sana. Kwa ufupi Mbeya ni Mkoa mbaya sana kuishi.
Kipindi ikifika ukakaa mikoa kama 10,utakuja kusema Mbeya afadhali....
Ukifika kanda ya kati utajua maana ya shida maji....
 
Kote huko hakuna la maana. Dar ni Upanga, mikocheni, msasani , o bay , na mbezi. Kwingine ni jehanam na nusu
Hukukaa Dar mzee umepita wewe.
Hiyo Mbezi unayosemea iwe Mbezi beach iwe Mbezi makabe kote maji shida na maji bei ghali sana kununua mpaka Kimara yote maji ghali.
Vyakula pia usiseme bei ghali sana.
Huko Msasani,Upanga,Mikocheni,Masaki na Oysterbay uwe na pesa hakuna wali wa buku kama Temeke na nyanya za 200 kama Temeke.Huko maisha bei ghali kwa matajiri.
Dar huijui wewe.
 
Tatizo la Mwanza ni slums na hela hakuna
Oh to me Mwanza is the best city in Tanzania, no matter what slums ziko in every city hapa Tz, na tuwe wakweli tu Mwanza hata kwa muonekano tu ni pazuri kichiz...

Imagine Mwanza ingekuwa nchi zilizoendleaa🔥🔥 ikawekwa infrastructures zakwendaa dah! Ni vle pia serikali ni kama imepazila kule kwenye swala la barabara.... Nktoka DOM naenda kujichimbia RockCity.
 
Back
Top Bottom