Mikoa 10 inayoongoza kwa umasikini. Je unadhani kwa nini wote wako upande mmoja?

Tanga huwezi kuikuta. Hata omba omba utawakuta Dar, Morogoro, Iringa, Dodoma, nk. Tanga yote huwezi kumkuta mtu amekaa barbarani anaomba! Kwetu hiyo ni dharau kubwa familia.
Kukuta omba omba wengi mji fulani siyo lazima iwe kiashiria cha umaskini wa eneo. Ombaomba huwa wana tabia ya kusafiri kutoka maeneo maskini na kwenda kwenye neema kuomba. Infact ombaomba wengi kwenye mji inaweza kuwa n kiashiria cha neema i.e. ombaomba wanapata msaada hivyo wakazi wengi wana maisha mazuri
 
Na hiyo mikoa inaongoza kwa imani za kishirikina na uchawi..!!

Sehemu za wachawi hazijawahi kuwa na maendeleo hata siku moja..!
Mzee mbona wachina wanaimani kali sana za kishirikina na wahindi lakini wametoboa
 
Kagera na Geita?
Embu acheni masihara mnaacha mikoa kama Manyara na Mtwara.
 
Kwa hivyo omba omba ni dharau kwa familia na ushoga ni nini maana tanga mashoga wapo wengi na waliwahi kunitongoza mbwa wale
Mimi ninaishi milima ya Usambaa. Huku hakuna hizo habari zenu za ushoga. Sisi tukishuka barabarani tunakuja kuuza bidhaa zetu za kilimo na kuchukua mahitaji, halafu tunarudi tena milimani kwetu.
 
Umetembea hiyo Kanda ya ziwa?
Simiyu
Shinyanga
Hii mikoa ina ukame wa kufa mtu, afadhali ya wilaya ya mkinga kule Tanga inayofanya mabinti wa sekondari waende shule wamevaa dera.

Geita
Hapa utakuta ng'ombe wanashindana kunywa maji ya kwenye madimbwi na binadamu

Kagera
Hawa ajira za serikari ndio zilikuwa zinawabeba na mlipuko wa ugonjwa wa mnyauko na kushuka kwa Bei ya zao la kahawa kumewadidimiza.
Uvuvi haujawahi kuwa na faida kwao

Mara
Hapa utakutana na masikini wengi na matajiri wachache

Mwanza
Angalau hapa panaweza kuwastiri ila ukiingia vijijini kule Bado sana
 
Mwanza nimefika mwaka 2019 ,yaani fikiria nilikuwa ugali mchana kwa elfu 12 ,ugali na samaki wa elfu 10 ,tena samaki wa kawaida kabisa... Geita nimefika mpaka sehemu inaitwa Bulyanhulu huko ndani ndani , porini kuna mijengo balaa .

Gesti pale mjini ni bei chee sana ila tatizo vyakula ,kila kitu kipo juu yaani
 
Umefika 2019?
Mimi mwaka huu, nilikuwepo huko
Utaniambia nini?
 
Ukiwa unaweka takwimu weka chanzo
 
Umasikini unaambata na population structure. Kama nchi au mkoa una kizazi tegemezi kikubwa kuliko nguvu kazi huhesabika maskini. Ndiposa tunahimiza uzazi wa mpango
Prove that assertion. Mana hapo kuna vitu viwili, umaskini wa mtu na umaskini wa jamii. Kenya population structure yake ni ya phase 2 kwenye evolution. Lakin mtu mmoja mmoja kuna maskini hata pa kulala hawana wanaozudiwa na maskini wa kitanzania ambao ni phase 3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…