Mikoa 10 Yenye Watu Maskini Zaidi Tanzania: Kagera namba 2, Dodoma namba 5. Nini Kinaiponza Mikoa Hii Maarufu?

Mikoa 10 Yenye Watu Maskini Zaidi Tanzania: Kagera namba 2, Dodoma namba 5. Nini Kinaiponza Mikoa Hii Maarufu?

Kagera sio tu kwamba inaongoza kwa umaskini wa Mali, hata ushamba.
Ukitaka ku prove hebu panda ndege ukute ndani Kuna mhaya. Au tu ukute mhaya anakula nyama, mtaa mzima utajua au ukute mhaya amenunua Bajaj! Maweee , lazima wiki hiyo anunue walau utumbo nusu kilo kusheherekea.
cc The Great Haya 😁😁😁😁
 
Akina nshomile walikwenda kujenga mikoa mingine! Nafikiri walikimbizwa na janga la Ukimwi ndiyo maana mkoa wao ni moja ya mikoa maskini.
Ndo unajifariji hivo unadhani huku kuna nyumba za tembe kama huko kwenu
 
Unaongelea umasikini kwa ku base kwenye pato la kila mtu bila kuangalia gharama za maisha na matumizi husika ya sehemu husika ?!!!

Hivi hata tunajua maana ya umasikini ? Unaongelea mtu wa Kagera halipi kodi ya nyumba, chakula anatoa shambani na hata elfu kumi ya kunywa konyagi hamalizi starehe yake kwenda kwenye ngoma ni bure....

Alafu homeless yupo Dar hajui hata kama atapata milo mitatu anajiona ni tajiri kwa kutokana na kwamba mkoa huo una viwanda au wazalishaji ingawa pesa hiyo haimsaidii huyu jamaa zaidi ya polution na kuchafuliwa hewa...

Nauliza tena hivi tunajua hata maana ya umasikini au ndio yale sababu kuna namba E nyingi mtaani tunaona tumeendelea kama jamii ?
Ulichofanya ni umeonyesha udhaifu wa kutumia hiyo njia kujua nani maskini lakini ndiyo kusema wote huko Kagera wana chakula na elfu 10 isiyoisha kwenye starehe?

Wakiumwa wanamudu gharama za matibabu? Likitokea janga ghafla mfano tetemeko wanaweza kujiendesha hadi wapi?
 
Ulichofanya ni umeonyesha udhaifu wa kutumia hiyo njia kujua nani maskini lakini ndiyo kusema wote huko Kagera wana chakula na elfu 10 isiyoisha kwenye starehe?
Tanzania wote hio mikoa ambayo wewe unaita sio masikini wana pesa ya chakula hata cha siku moja ? Bora sehemu ambazo hazina ukame wanaweza wakapata chakula na wana malazi (ndani ya kajumba) majority huko kwenye so called mikoa ambayo sio masikini wanakaa kwenye slums
Wakiumwa wanamudu gharama za matibabu?
Ni wapi Tanzania wakiumwa wanamudu gharama za matibabu au haujatembelea hospitali watu hadi maiti zinawekwa rehani ?
Likitokea janga ghafla mfano tetemeko wanaweza kujiendesha hadi wapi?
Ni wapi likitokea janga wanajiendesha.., tena achana na janga la once in a lifetime kuna watu Dar kila mvua zikinyesha mito inahamia sebuleni kwao
 
Hukuti Lindi wala Mtwara hapo kusini kuchele!!!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mikoa ya Kusini inafanya vizuri Sana kwenye Kilimo Kwa Sasa hasa Korosho na Ufuta.

Tandahimba & Kilwa 👇👇
20240729_091957.jpg
20240729_092032.jpg
 
Back
Top Bottom