Mikoa 13 Kinara wa Kuchangia Kodi ya TRA mwaka 2023

Hoja gani?
Mkuu 'Nguruvi', tusilifanye hii kuwa kama 'ligi'! Inaonekana kuwa hujanielewa ninaposimamia katika swala zima la muungano.
Hapana sikuongelea muungano.
Hoja ilikuwa miundombinu ukishadidia kushuka kwa uzalishaji mikoa ya kaskazini.
 
Hapana sikuongelea muungano.
Hoja ilikuwa miundombinu ukishadidia kushuka kwa uzalishaji mikoa ya kaskazini.
Allaaaa. Kumbe!
Kuniradhi kwa kuelekea kwingine.

Hoja hiyo, bado sana mkuu 'Nguruvi'. Kukumbatiwa kwa Tanzania na hiyo nchi jirani kuna namna, siyo bure!
Hili ni dhahiri taasisi zetu husika zimelaza akili sana!

Lakini kidogo kidogo tumeanza kutambua ujinga wetu ulipo. Hili linatia matumaini.
 
Wekeni intern airport uone Mwanza inavyopaa
Mwanza ina kila sifa iliyo nayo Dar, ila sifa hizo hazijatumika kwa stahiki inayo tegemewa.
Bandari kusafirisha mizigo kwenda nchi jirani, Uganda na Kenya na mikoa mingine inayoizunguka.
Reli na barabara zinazoingia na kutoka Mwanza
Uwanja wa ndege wa kimataifa
Utalii, kwa ukaribu wake na mbuga za wanyama
Ziwa halijatumika ipasavyo katika uzalishaji wa samamki, hasa ufugaji wa samaki
Viwanda, bado sana. Mahali palipo na watu wengi huwezi kukosa viwanda

Badala ya Mwanza kutegemea kupeleka bidhaa Dar es Salaam pekee, inatakiwa kuwa kitovu cha kusambazia bidhaa. DRC, Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya ni maeneo yanayotakiwa kuitegemea Mwanza kwa kazi hiyo.
Sifa hiyo haitegemei kuombwa kwa yeyote, ni sifa iliyopo kiuhalisia kutokana na eneo ilipo.
 
1. Umeweka Top 13 ili Mbeya tu iwepo🤣🤣🤣

2. Wapi Iringa?

3. Nimependa jinsi Arusha na Kilimanjaro wanavyoiacha mbali Mwanza. Hivi Mwanza ukitoa Ziwa Victoria inabakiwa na nini?

4. Hongereni Kagera. Naona mnakuja kuja
instanbul
Mwanza hakuna kitu pale badala ya samaki peke yake, Mwanza alikuwa juu kabla Geita haijawa mkoa, na Geita itakuja kuipiku Mwanza utashangaa,
 
Mbona haviendani na takwimu za region GDP.
Kuna ukwepaji kodi ama TRA hawafanyi kazi zao sawa sawa.
 

Geita na Shinyanga hakuna top ten pamoja na migodi yote
 
Tanzania imejenga Uchumi wa Nchi ambao ni tegemezi Kwa Dar ,haya ndio matokeo yake Sasa.

Pili Mwanza inakabiliwa na ushindani wa Miji mingine kama Kahama,Geita na Katoro.

Mwisho sijaona hiyo jiografia ya Mwanza ya kumhudumia hizo Nchi jirani kama unavyosema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…