Mikoa 13 Kinara wa Kuchangia Kodi ya TRA mwaka 2023

Kutoka kwenye takwimu za Mapato ya Kodi za TRA yaani Regional Tax Statistics za mwaka 2023/2024 zimebainisha Mikoa 13 ambayo imechangia Mapato makubwa ya Kodi Kwa mwaka 2023.

Uchambuzi wa awali nilioufanya umebainisha Mikoa 13 ambayo imechangia zaidi Mapato ya Kodi ya kuanzia Bilioni 60 na zaidi.

Orodha hiyo Kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 inasomeka kama ifuatavyo;(Figures are in "000" Million Tanzania Shillings).

1. Dar es Salaam =7,416.95
2. Arusha =356.28
3. Kilimanjaro =234.88
4. Tanga =203.28
5. Songwe = 176.81
6. Dodoma =163.17
7. Mwanza =160.66
8. Mara =143.13
9. Kagera =118.94
10. Mtwara =116.44
11. Mbeya =85.10
12. Morogoro =67.60
13. Pwani =60.60

View attachment 3063007

My Take
1.Vyanzo vya Kodi kama Utalii, Property Tax,OPMU,MTD na Large Tax Payers Sio sehemu ya takwimu za Mikoa Kwa sababu ni Kodi ya Jumla ambayo Haina mchanganuo wa Mkoa ilikokusanywa.

2.Figurrs za Mkoa wa Dar es Salaam zimehusisha Mikoa ya kikodi iliyoko Dar ambayo ni Ilala,Kinondoni,Temeke,Tegeta,Kariakoo,DSM Service Centre na JNIA.

✓Credits;TRA Regional Tax Statistics 2023/2024.

Observation
•Mapato ya Kodi Kwa Mikoa Mingi mwaka ulioisha wa 2023/2024 Yalishuka sana ukilinganisha na Mwaka 2022/2023. Huenda Mvua za El Nino zilichangia Hali hiyo na sababu zingine.Utalii na Makaa ya Mawe viliokoa jahazi.

•Mkoa wa Mtwara umefanya vizuri Sana kwenye Mapato Kwa sababu ya Bandari ya Maboresho ya Bandari ya Mtwara ,amri ya Rais kusafirisha korosho Kupitia mtwara na Kusafirisha shehena kubwa kabisa ya Makaa ya Mawe kutoka Ruvuma na Njombe.

•Mwanza inazidi kupotea kwenye Ramani ya Uchumi wa Tanzania huku nafasi yake ikichukuliwa na Mikoa mingine.Mlioko Mwanza Jiji lenu limekumbwa na nini Hadi shughuli za Uchumi zinazorota?

Mwisho.
•Pamoja kwmaba TRA ndio taasisi mama ya kukusanya Mapato ila Tanzania Ina taasisi nyingi sana zinazokusanya Mapato ya Serikali,hivyo mchango wa Mkoa kwenye Uchumi wa Nchi unapimwa sawaia Kupitia GDP.

Pia soma Mikoa 15 Inayoongoza Kuchangia Kodi za TRA Tanzania

Angalizo
•Uchambuzi huu sio rasmi hivyo uchukuliwe Kwa muktadha huo.Taasisi Zenye mamlaka husika ndio zitafanya Uchambuzi wake wa kina kama zikiona inafaa.
Mikoa ya kaskazini inafanya vizuri sana kwenye ukusanyaji wa kodi. Imagine hapo hakuna kodi itokanayo na utalii lkn bado mikoa mitatu mikubwa ya kaskazini imepangana kwa mfuatano nyuma ya DSM.
This should be a case study.
Mbeya ina madini kule Chunya na Mpaka wa Kasumulu, lkn bado inachangia mapato ya kodi kidogo sana.
 
Mikoa yote ya Kaskazini Ina border posts na Nchi yenye uchumi mkubwa EAC na largest trading Partner wa Tzn so lazima watafanya vizuri.

Pili Ina Utalii ambao ni Moja ya taxable activity sana.

Mbeya Ina migodi ya Wachimbaji Wadogo ambao sio walipakodi wakubwa ingawa kule kwenye Mapato ya Tume ya Madini,Mbeya inaongoza.

Mwisho Mikoa yenye migodi mikubwa kama Geita,Mara nk haijatokea hapo Kwa sababu Mapato yake Yako kwenye Large Tax Payers ambao hawajayachanganua.

GDP ndio inatoka taswira halisi ya Mchango wa Mkoa kwenye Uchumi maana Ina account Kila economic activity na value yake.
 
How GDP ina account kila activity?
Hakuna economic indicator yenye deviation kama GDP. GDP ni uongo mkubwa.
 
Mzee hatuli GDP. Tunakula kodi. Huwezi kutumia GDP kulipa deni la Taifa. Tunatumia kodi kulipa mishahara katika ulinzi na usalama, Utumishi wa umma. Hatutumii GDP. Na kamq GDP haijitokezi katika kodi, ina maanisha ni zero, ni nothing, ni uongo.
 
Umefanya analysis ndogo sana.Kwa mfano tuchukue taasisi zote za Serikali zinazokusanya pesa , unadhani hiyo Mikoa yote itaizisi Mbeya?

-Mapato ya Halmashauri
-Tume ya Madini
-Vyama vya Ushirika wa mazao
-Utalii
-Tanesco
-Ewura
-Mamlaka ya Bandari
-Tazara
-TBS
-Walipakodi wakubwa mfano TBL,Vodacom,Coca-cola,Mbeya Cement nk ,,Mkoa gani utazidi Mbeya ukiacha Dar,Mwanza labda na Arusha ingawa sidhani (10.8T-8.8T=2T),hii ni Gap kubwa.

So inaelekea hujajua vyema tafsiri ya GDP,ukitoa Government Spending kwingine kote ni flow ya hela.
 
How GDP ina account kila activity?
Hakuna economic indicator yenye deviation kama GDP. GDP ni uongo mkubwa.
Uongo upi? Mfano mdogo TBL ,Mo energy,Alaf nk Wana Matawi Mbeya ila wamesajiliwa kama walipakodi wakubwa Kwa Tin namba ya kiwanda Mama Cha Dar so Kodi yake inalipwa Dar ila haiwezi kusoma kwenye TRA Mbeya.

Lakini GDP Ina track source ya Kila activity na ku valuate kwenye currency value ndio inakupa jawabu la mchango wa Uchumi wa Mkoa.

Sasa hiyo haifanyiki Kwa TRA,ndio maana nakwambia hiyo sio Kipimo pekee Cha malipo.

Mwisho mfano Makusanyo ya Halmashauri,mwaka huu 2023/24 Mbeya ni namba 2 baada ya Dar ila hayo hayapo kwenye TRA ila GDP inaya account yakiwemo ya TRA na mengineyo.👇👇
juma_zuberi_homera_1720609958796204.jpg
 
Wanaogopa sana hiyo kitu
Hicho ni Kisingizio,kwamba Uwanja wa Ndege wa Mwanza unashindwa kutia ndege zipi ikiwa dreamliner zinatua?

Mbona hatuoni routes za Mwanza to Kampala,Mwanza to Zanzibar,Mwanza to Kigali nk licha ya uwepo wa ndege kubwa zinazofanya safari ndani ya Nchi?

Jibu ni kwamba hakuna Abiria wa Kimataifa.

Wangeongea watu wa Muhimu ningeelewa kwamba Wanabaniwa Kwa sababu ya KIA.
 
Tanzania imejenga Uchumi wa Nchi ambao ni tegemezi Kwa Dar ,haya ndio matokeo yake Sasa.

Pili Mwanza inakabiliwa na ushindani wa Miji mingine kama Kahama,Geita na Katoro.

Mwisho sijaona hiyo jiografia ya Mwanza ya kumhudumia hizo Nchi jirani kama unavyosema.
Dah!

Hujui maana ya jiografia ilipo Mwanza?

Jiji la Mwanza liwe na ushindani na hizi' satellite' ulizo taja hapa?

Sijui 'background' yako kitaaluma ni nini, lakini hata 'common sense' pekee ingetosha kukuonyesha upungufu mkubwa katika hayo uliyoweka hapo!
Sasa unataka tujadili hisia zako, tuache uhalisia wa mambo yalivyo na yatakavyoendelea kuwa?

Bado naendelea kukupima, lakini kadri ninavyozidi kuona upeo mdogo unaouonyesha hapa katika maswala mengi, ni wazi kuwa kipimo chako ni hafifu.
 
Jiografia hailazimishwi, yaani hayo unayoongea yangeshakuwa yanatokea Hadi Sasa so kuharibu kulazimisha ni kupoteza Nguvu Bure.

Soma hapa Mwanza wamebaki na milima yenye mawe, Dhahabu, Geita, Kwa jicho la ndani, Kufurahia kuzaliwa mkoa mpya Geita,ni maumivu kwa jiji la Mwanza!
 
Umefanya analysis ndogo sana.Kwa mfano tuchukue taasisi zote za Serikali zinazokusanya pesa , unadhani hiyo Mikoa yote itaizisi Mbeya?

-Mapato ya Halmashauri
-Tume ya Madini
-Vyama vya Ushirika wa mazao
-Utalii
-Tanesco
-Ewura
-Mamlaka ya Bandari
-Tazara
-TBS
-Walipakodi wakubwa mfano TBL,Vodacom,Coca-cola,Mbeya Cement nk ,,Mkoa gani utazidi Mbeya ukiacha Dar,Mwanza labda na Arusha ingawa sidhani (10.8T-8.8T=2T),hii ni Gap kubwa.

So inaelekea hujajua vyema tafsiri ya GDP,ukitoa Government Spending kwingine kote ni flow ya hela.
Hayo yote unayoyasema, na Arusha zipo. Ukiweka utalii, si ndio balaa. Mikoa yote ya kaskazini inafanya vizuri sana kwenye utalii. Arusha ni mkoa wa pili kwa matumizi ya umeme nchini, ni mkoa wa kwanza kwa hoteli kubwa za kitalii.
 
Kuwakamua wafanyabiashara wadogo kwenye leseni na viushuru vya ajabu ndio vinaongeza mapato ya Halmashauri za Mbeya.
 
Arusha kwa miaka mingi imekua ikichangia mno pato la Taifa lakini huduma muhimu hawapewi.

Stendi ya mkoa tu ya maana hakuna.

Barabara za lami chache, maeneo mengi ni vumbi tu.

Wamasai ni kunyanyaswa tu kwa kufukuzwa makazi yao ya asili.
 
Umefanya analysis ndogo sana.Kwa mfano tuchukue taasisi zote za Serikali zinazokusanya pesa , unadhani hiyo Mikoa yote itaizisi Mbeya?

-Mapato ya Halmashauri
-Tume ya Madini
-Vyama vya Ushirika wa mazao
-Utalii
-Tanesco
-Ewura
-Mamlaka ya Bandari
-Tazara
-TBS
-Walipakodi wakubwa mfano TBL,Vodacom,Coca-cola,Mbeya Cement nk ,,Mkoa gani utazidi Mbeya ukiacha Dar,Mwanza labda na Arusha ingawa sidhani (10.8T-8.8T=2T),hii ni Gap kubwa.

So inaelekea hujajua vyema tafsiri ya GDP,ukitoa Government Spending kwingine kote ni flow ya hela.
Mzee ulizia vizuri makusanyo ya tozo za huduma za taasisi za umma katika ofisi za Kanda ya Kaskazini ambazo nyingi zipo Arusha au ofisi za mikoa na makusanyo ya ofisi za Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambao nyingi zipo Mbeya. Mbeya ni mkoa mdogo kiuzalishaji isipokuwa mazao ya chakula na kitimoto.
 
Serikali isingeamua kwa makusudi kabisa kuuhujumu mkoa wa mara,makao makuu ya mbuga ya serengeti yangekua ndani ya mkoa wa Mara, hiyo Arusha ingechora chini.
 
Uongo upi? Mfano mdogo TBL ,Mo energy,Alaf nk Wana Matawi Mbeya ila wamesajiliwa kama walipakodi wakubwa Kwa Tin namba ya kiwanda Mama Cha Dar so Kodi yake inalipwa Dar ila haiwezi kusoma kwenye TRA Mbeya.

Lakini GDP Ina track source ya Kila activity na ku valuate kwenye currency value ndio inakupa jawabu la mchango wa Uchumi wa Mkoa.

Sasa hiyo haifanyiki Kwa TRA,ndio maana nakwambia hiyo sio Kipimo pekee Cha malipo.

Mwisho mfano Makusanyo ya Halmashauri,mwaka huu 2023/24 Mbeya ni namba 2 baada ya Dar ila hayo hayapo kwenye TRA ila GDP inaya account yakiwemo ya TRA na mengineyo.👇👇View attachment 3063554
Hivi madini ya chunya yako mbeya au songwe mkuu?
 
Back
Top Bottom