Mikoa 13 Kinara wa Kuchangia Kodi ya TRA mwaka 2023

Mikoa 13 Kinara wa Kuchangia Kodi ya TRA mwaka 2023

Jibu basi swali!
Mapato ya majiji hayajumuishwi kwenye mapato ya mkoa?
Kwa maana ya Mapato ya Mkoa kutoka chanzo Cha TRA haihusiani.

Lazima ujue kuna vyanzo vya TRA,vyanzo vya Halmashauri,Vyanzo vya Taasisi zingine mfano Tume ya Madini,TCRA,TMDA , Mahospital nk zote hizo ni taasisi zinakusanya pesa.

Ila wakusanyaji Wakuu ni TRA(Kodi) ,so Mapato ya TRA hayahusiani na ya Halmashauri
 
Hii mikoa iliyo mizigo kama Katavi na Lindi ifutwe Tu ni kope kwa Dar Ar na Kilimanjaro! Yaani makusanyo ni 10 bilioni kwa mwaka TRA halafu Una hadhi ya kuwa mkoa?
Hapana Bado ni Mikoa michanga mfano Katavi.

Pia TRA nao Bado hawajawekeza staff wa kutosha ku capture vyanzo vya Mapato huko.

Mwisho Mkoa kama Lindi una makusanyo makubwa kwenye sekta zingine mfano Halmashauri wanakusanya zaidi ya Bilioni 40 Kwa mwaka ,Bado uvuvi,gesi nk.
 
Vigezo vya kuanzishwa mikoa viangaliwe! Visiwe kisiasa Tu ni lazima kuwe na uwezo lijitehegemea! Mtoto kama anataka kuoa asitegemee Baba akishoa! Yaani 10 bilioni makusanyo kwa Lindi na Katavi ni aibu kubwa Bora ziwe wilaya na mji kama Kahama upandishwe hadhi kuwa mkoa
 
Baada ya Miaka 5 Mtwara itakuwa iko Top 5, uwekezaji kule ni mkubwa sana. Kama sio Vurugu za Msumbiji nadhani ingekuwa top 3 hapo. Kule ndio kuna miradi mikubwa mikubwa yenye kuingiza pesa za moja kwa moja ukiitoa Dar.
 
Kigezo namba Moja ni jiografia,hayo mengine yanategemea uwezeshaji wa kiserikali na sio Mapato au Wingi wa watu,ikiwa hivyo Wilaya za Dar zitakuwa Mikoa Sasa.
 
Baada ya Miaka 5 Mtwara itakuwa iko Top 5, uwekezaji kule ni mkubwa sana. Kama sio Vurugu za Msumbiji nadhani ingekuwa top 3 hapo. Kule ndio kuna miradi mikubwa mikubwa yenye kuingiza pesa za moja kwa moja ukiitoa Dar.
Hakuna Cha Uwekezaji wowote na upepo wa uvunaji wa Makaa ya Mawe ambao Kwa miaka ya Karibuni umepata mara 200 baada ya vita za Russia vs Ukraine, Wazungu walikacha gesi ya Urusi wakaanza kutumia vyanzo vingine vya Nishati ikiwemo makaa ya Mawe.

Pili unakumbuka Rais aliagiza korosho zote zipitie Mtwara? Hayo mambo 2 ndio yameleta hizo pesa hapo Sasa ila kabla yake ilikuwa hakuna kitu,angalia mwaka uliopita utaona.
 
Back
Top Bottom