Mikoa mibaya zaidi kufanya biashara ya Real estate au Nyumba

Minaona..... kama duniani tunapita, kwanini nijenge njiani..🙄
 
Pana nyumba zipo Iwambi hapo mwanzo nilikua nafanya na BnB ya USA walikua na makato makubwa sana sasa hivi dogo ananiambia kaachana nao anatangaza mtandaoni sijajua ni platform gani naona zinajaa muda wote na jamaangu yeye kajengea Uyole nae anasema anapata wateja wewe umejenga ili mpangaji huyu anaelalamika mshahara bado haujaingia unaacha kuweka wateja wa dollar..
 
Nilipanga nyumba nzovwe vyumba viwili na sebule kwa 60000 ila choo nje nilikaa hapo chupu chupu niinunue na nyumba yenyewe
 
Hivi nyumba za Avic Town wastani ni ngapi?
 
Kwa mkoa mzima wa Mbeya sehemu pekee yenye maisha ya juu ambapo biashara ya nyumba ni uhakika kukulipa ni Chunya na makongorosi, sababu kubwa ni biashara ya dhahabu wenye hela wapo wengi kwaiyo wanamudu gharama,na kwa mkoa wa Songwe nenda wilaya ya songwe maarufu kama mkwajuni imepakana na makongorosi,pia wana dhahabu nyingi na mgodi mkubwa zaidi wa dhahabu nyanda za juu kusini upo hapo mkwajuni,wao chumba Cha kawaida ni elfu hamsini mpaka 70, master zinaanzia elfu70 mpaka laki moja kulingana na standard ya nyumba
 

Nimeishi Mbeya kwa muda mrefu kidogo.Hela pale ni ngumu sijawahi kuona.biashara pale ni ngumu sana.Nyumba ni baadhi ya vitu ambavyo ni anasa hiv.

Ndugu yangu aliwahi jenga nyumba maeneo ya Ilomba,nyumba ilisumbua sana kuiuza.mwisho akauza m8 nazo nadhani alilipwa kwa mafungu kadhaa.

Na mwingine alijenga maeneo isanga.nyumba ya kisasa saana.alipostaafua akaona maisha kule magumu akaamua kurudi zake Dar alikoanzia kazi.sasa ikaja iaaue ya aiza aiuze au apangishe.wapangaji wanaishia 100k kwa mwezi.akaona isiwe shida,aiuze tuu. offer ya juu zaidi ni m12.ndipo akaamua kuiuza kwa m12.Kumbuka ni nyumba ya kisasa sana.

Kwa hiyo.ni kweli mbeya nyumba siyo biashara.labda fremu maeneo ya mwanjelwa na soweto
 
Watu wa status ya juu wanalipa vizuri ukiwapata ila sasa hawataki kukaa mashenzini wao wana maeneo wanayapenda. pia kuwapata ni changamoto ingine maana sio wengi. inatakiwa usiwe na haraka na hiyo pesa maana hao wa kundi hilo sio wengi.

huku changanyikeni unatakiwa usiweke kodi kubwa hautapata watu au weka chumba kimoja na sebule na kodi ya kawaida apo utawapata ila uwe na moyo wa kuwafatilia ulipaji ni changamoto sana.
 
offer ya juu zaidi ni m12.ndipo akaamua kuiuza kwa m12.Kumbuka ni nyumba ya kisasa sana.
daah hlf umestaafu? ukitoka apo presha moyo vyote vinakupitia kwa pamoja. ila uyo labda alikuwa na haraka tu angeweza kupata ela zaidi ya apo.
 
Sasa unataka.watu wahame kwenye nyumba zao kisha wakapange? Wafanyakazi.wenyewe kama Katavi akikaa kidogo anatafuta kiwanja anajenga sasa akapange wapi! Jenga nyumba za wageni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…