Mikopo kwa walimu, NMB vs CRDB

Mikopo kwa walimu, NMB vs CRDB

Barclays ni nzuri, inakopesha kwa 18% mpaka 22%. Inatoa mkopo kuanzia 1,000,000/= hadi 80,000,000/= muda wake ni kuanzia miezi 12 mpaka 60.
Nenda barclays.

Hawa jamaa ni wezi msithubutu kukopa mie mpaka sasa najuta kuwafahamu. Mnasaini mkataba ukitoka wanafuta na collection fluid, Wana badilisha pia unajaza mkataba wa miaka 5 ukija chukua mkataba unakuta imejazwa miaka 6, wanaanza sound subir miez 6 iishe ufanye top up turekebishe ni wezi tena zaid ya wezi kenge nyie.
 
AC

ACHA UONGO. SALARY SLIP ZA MIEZI SITA NA SIO MITATU KAMA ULIVOAINISHA HAPO JUU

Wewe unachokiongea hukijui,sababu mimi nnaekupa hizi taarifa nna uhakika na nnachokiongea.Japo unaweza ambiwa miezi zaidi ya hiyo (3) kama Benki(kupitia afisa mikopo) wanaona mishahara yako haina consistency,lengo la kukuomba zaidi ya miezi hiyo ni kujiridhisha uhalisia wa hizo salary slip.
 
Hawa jamaa ni wezi msithubutu kukopa mie mpaka sasa najuta kuwafahamu. Mnasaini mkataba ukitoka wanafuta na collection fluid, Wana badilisha pia unajaza mkataba wa miaka 5 ukija chukua mkataba unakuta imejazwa miaka 6, wanaanza sound subir miez 6 iishe ufanye top up turekebishe ni wezi tena zaid ya wezi kenge nyie.
Pole sana.
 
Wakuu baada ya kufanya utafiti kidogo na kuongea na ma afisa mikopo wa hizi benki mbili nimefikia hitimisho CRDB ni bora labda sijajua kuhusu malalamiko ya kuchelewesha kuweka mkopo. Nmb wanaweka fasta ila wizi wao umekubuhu yani eti mkopo wa 10,700,000 wananipa 10,138,250 nyingne wanakata kama processing fee na bima.
 
Hyo processing fee Ni ya nn
 
crdb inatoa mikopo mikubwa ila wana process ndefu hadi wakupatie.nmb wanamikopo midogo ila wanakupa ndani ya muda mfupi sana unaweza ukaanza process ndani ya siku tatu ukachukua mkopo. ukitaka mikopo yenye hela ndefu nenda EQUITY wanaweza kukupa hadi mil20 wanabranch yao mwenge na bagamoyo ila sijajua kwa mikoani.pia ukitaka kukopa inashauriwa nenda kakope mwezi wa sita maana benki nyingi huongeza viwango vya kukopesha.pia kama unataka kukopa bila riba unaweza kwenda kukopa PBZ ipo mtaa wa lumumba,karibu na ofisi ndogo ya ccm hapa dar es salaam,wanatoa mikopo mizuri hata kama mshahara wako unapitia kwenye benki nyingine ila wao hutaka wakukute kwanza kwa miezi mitatu ndo wakukopeshe unachotaka ukopeshwe.
hapo kwenye wakukute cjakuelewa mkuu
 
nilienda kuuliza bank mbili juzi. nikaanza na crdb wakaniambia kwa salari yangu maximum watanipa 11,300,000 kwa miaka 6 na watanikata 257,000. nikaenda nmb wakaniambia maximum watanipa 9,500,000 na watanikata 251,000. Kimsingi hakuna tofauti za riba

=========================================================================== Kwa maelezo yako hapo juu tofauti ya riba ipo kama ifuatavyo:-

1. Tsh. 11,300,000/- kwa miaka 6 na makato ya Tsh. 257,000/- kwa mwezi ni sawa na riba ya 18% kwa mwaka/per annum au 1.5% kwa mwezi.
2. Tsh. 9,500,000/- kwa miaka 6, kwa makato ya Tsh. 251,000/- kwa mwezi ni sawa na riba ya 24% kwa mwaka au 2% kwa mwezi.

Note: Viwango vya mkopo ulivyotaja ni tofauti kama vinavyoonekana hapo juu (Bolded)

- Hivyo kwa uwiano sawa wa viwango vya mkopo makato ni kama ifuatavyo:-

4. Tsh, 11,300,000/- kwa miaka 6 na riba ya 18% au 24% itapelekea makato ya Tsh. 257,728.04 (18%) au 297,493.19 (24%)
5. Vivyo hivyo Tsh. 9,5000,000/- itapelekea makato ya Tsh. 216,674.02 kwa riba ya (18%) au Tsh. 250,104.89 kwa riba ya 24%

Hope umeona tofauti.
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
 
Mikopo mizuri ya wafanyakazi ipo Benki ya Posta.
pia kuna mikopo kama:
- YA VIKUNDI, just cha watu 5-10
-SACCOS
-VICOBA
-WASTAAFU wa PSPF,PPF,NSSF,GEPF,LAPF
-WAFANYAKAZI
-YA ELIMU KWA WANAOCHANGIA PSPF na GEPF
-YA KUANZA MAISHA KWA WANAOCHANGIA PSPF NA GEPF
-BIASHARA KUBWA
-BIASHARA NDOGO NDOGO
Pia,

mikopo ya wafanyakazi inatolewa hadi miaka 6 na kwa wastaafu hadi miaka 4

Riba zao ziko chini sana yaani wafanyakazi ni 13 kwa waajiri wazuri na 15 kwa waajiri wanaochelewesha makato.

Tembelea tawi la Benki ya Posta lililoko karibu kuthibitisha haya.

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Usidanganyike na hicho kiwango cha riba !!!!
 
Mi Nina mkopo hapo nlichukua m 4.5 wanakata 132 kwa 5years
Ina maana unalipa riba ya 3,420,000/= yaani karibia asilimia 100 ya mkopo. Duh...!!! hauwezi kuwa mkopo huo.
 
Back
Top Bottom