Kasema wanakopesha hadi 50% ya gharama ya gari kama unanunua hapa hapa Tanzania yaani kwenye yard ila wanakopesha 45% ya gharama kama gari ndio ipo Japan inaagiziwa kuja Tanzania.
So wewe utaangalia unatakaje. Mfano unanunua gari la milion 20 ila ndani una milion 15 it means umekosa milioni 5 na unahitaji kukopeshwa milioni 5. Wao watakupatia mkopo unaohitaji kulingana na mahitaji yako ya kiasi cha pesa kilichopungua kwenye bajeti hawakupangii ukope kiasi gani ili mradi tu kisizidi 50% ya bajeti mzima kama unanunua hapa hapa tanzania kutokea yard na watakusapoti 45% kama unaimport kutokea japan au Dubai, au china, UK, marekani, Germany, South Africa etc. Wewe sasa ndio ujipange.