Umeongea kitu kikubwa sana ambacho watu wengi hawakijui, Mimi si mshabiki wa CCM ila niseme kiukweli kama siyo Plan za mama Tanzania tulikuwa tumekwisha. Hali hii ngumu ya uchumi kwa sasa ingekuwa mara kumi zaidi hivi sasa kama mwenda zake angekuwepo, kwani alishafukarisha wafanya biashara wote wakubwa kwa wadogo, Deni hili la taifa limeongezeka kwa kasi sio kua mama Anakopa sana ila ni madeni na pesa tulizokopa Kw kausha Damu. Nimpongeze mama kwa kiasi fulani kwa hatua alizo chukua lakini bado anapaswa kukaa chini na kusugua kichwa kwa kina. Pia ahakikishe anapata muafaka na wapinzani kwani wanaweza wakamchafulia na kuanza kumanga manga, kwani hali kwa ujumla kwa sasa siyo kabisa, Watanzania wanataabika ile mbaya.