Mikutano inayozungumzia mikataba haitokuwa na maana bila kutaja MOU ya Serikali na kanisa

Za serikali hazijengwi kwa kodi yako? kama ni hivyo kwa nini utake hospitali za kimisheni peke yake zitoe huduma bure kwa sababu tu serikali inachangia uendeshaji wake?

Amandla...
Sasa hicho ninachochangia kwenye Kodi kwa nini nije nichangie tena??
 
Nadhani somo la civics lilikupita ,hivi unajua gharama za hospital za binafsi na serikalini? Fanya utafiti kisha uje kuuliza swali lako....inaonekana haujui kazi ya serikali kwenye kutoa huduma kwenye jamii huwa wanafanya kitu gani....Kama Serikali inawapa mabilioni makampuni ya simu wajenge minara ku serve wateja wao ndiyo unashangaa serikali kuwapa TEC fedha?

Ndiyo Civic uliyosomeshwa kanisani hiyo ? Yaani kampuni ya simu kwa mfano Tigo ya Waswedish ipewe pesa na Mtanzania kuendesha kampuni ya simu ? 😝😝😝
Hujajibu swali kwanini serikali itoe pesa kuendesha hospitali Za kanisa halafu sisi tuendelee kulipa tena huduma ?
 
Sasa maswala madogo kama hayo hauyajui ,je makubwa ya MOU ya TEC na GOT utayajua?
 
Kama kuna mikutano inayozungumzia mikataba mibovu basi kusiwe na ubaguzi.Muda umefika sasa wa kuitaja mmoja mmoja. Mengine irekebishwe na mingine ipo haja ya kuvunjwa mjoja kwa moja

Mpaka sasa wale wanaokosoa mkataba wa bandari naona wamekaa kimya kwa mkataba ule wa kanisa na serikali wa mwaka 1992.Si lazima wausome wote hata kutaja tu udhaifu wa hoja za wale wanaotilia shaka mkata huo ingetosha kusawazisha hoja za utetezi wa zinazoonekana kasoro za mkataba wa DP World.

Naamini wote walikuwa wanaujuwa na kama ilikuwa bado basi wamesikia kelele za walalahoi.Kelele hizo ni kama hizi kwenye bandiko hapo chini :

WAKATI MNAPAMBANA KUONDOA KIFUNGU HEWA CHA MKATABA WA MILELE (ambacho hakipo) WEKENI NA AKIBA YA MANENO.

TUKUMBUKE MWAKA 1992

Mwaka 1992, Serikali iliingia Mkataba na Makanisa kupitia Taasisi zao za TEC na CCT. Chini ya Makubaliano yale, hospitali za Makanisa zitatumika kwa wananchi wote pale ambapo Serikali haina hospitali.

Kwa kufanya hivyo, Serikali itakuwa na wajibu wa kuyapa Makanisa fedha za kuendesha hospitali hizo ingawa umiliki wa hospitali utabaki kuwa wa Makanisa.

Ifahamike kuwa fedha hizo zinatokana na kodI za Watanzania wote; Waislamu, Wakristo, Mabaniani, Magoha, Makadiani, na hata wale wasio na dini.

Nini athari za Mkataba huu ? Mkataba huu wa kibaguzi una athari nyingi. Kwanza:

Serikali inatumia kodi za wananchi kuyapa Makanisa kuendesha shughuli zake za kuimarisha Ukristo.

Tunasema hivyo kwa sababu utaratibu unaotumika ni kuwa Serikali inatoa fedha kwa Makanisa ambayo wao ndio wanapanga matumizi ya fedha zile na sio Serikali.

Pili, kwenye Jamii, Makanisa yanaonekana ndio yanatoa huduma za Jamii na hivyo kujenga saikolojia kwa wananchi kuwa Ukristo ndio unajali wananchi.

Athari ya tatu ni kuwa Makanisa yananyonya wananchi kwa sababu pamoja ya kuwa hospitali zile zinapata fedha kutoka Serikalini, bado wananchi wanalipia huduma.

Nne, Mkataba hauna ukomo, yaani ni wa milele. (Wakristo wataendelea kupewa hayo mabilioni na Waislamu watanyimwa milele).

Kwa tafsiri nyingine ni kuwa Serikali imejivua kwenye wajibu wa kutoa huduma za Jamii na kuchagua Makanisa kuwa ndio wakala wake.

Tunapenda kuwakumbusha Watanzania kuwa wakati Mkataba huo unasainiwa aliyesaini Mkataba ni Bwana Edward Lowassa aliyekuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu. Huyu ni Mkristo

Kwa utaratibu wa Serikali, Lowassa alikuwa Waziri wa Nchi, hivyo basi Waziri mwenye dhamana ni yule mwenye ofisi yake kwa maana ni Waziri Mkuu.

Wakati unatiwa saini Mkataba, huo Waziri Mkuu alikuwa John Samwel Malecela ambaye ni Mkristo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ndie aliyeishauri Serikali isaini Mkataba ule ambao kwanza hauna ukomo (mkataba wa maisha) na pili unatumia kodi za wananchi kuimarisha Ukristo alikuwa Damian Lubuva ambaye ni Mkristo.

Kwa upande wa Kanisa mwanasheria wao alikuwa Prof Balozi Costa Mahalu, Mkristo.
Kwa maana hiyo, upande wa Serikali, Mkataba ule umeasisiwa na kusimamimwa na Wakristo watupu. Waziri wa Nchi Mkristo, Waziri Mkuu Mkristo, Mwanasheria Mkuu Mkristo.

Ni Wakristo! Wakristo! Wakristo!

Kama kwenye hoja ya makubaliano ya Bandari ni Wazanzibari wawili (ambao ni Waislamu) wamesaini makubaliano ya kuiuza Tanganyika, Mbona Waislamu hawakulalamika pale Wakristo 3 wazito Serikalini walipobuni mbinu za kutumia kodi za wananchi kuimarisha dini yao Ukristo Tanzania?

Kama hoja ni ukomo wa mkataba, mbona Mkataba huu wa Serikali na Makanisa hauna ukomo? Ni mkataba wa milele na ndio maana mpaka leo (miaka 30 sasa) bado unaendelea kutumika.

Bado Serikali inaendelea kutekeleza Mkataba wa kibaguzi ambapo inatumia kodi za wananchi wote kuimarisha shughuli za Kanisa.

USHAHIDI

Tarehe 23 Januari 2019, Rais Magufuli alikutana na viongozi wa dini zote IKULU. Kwenye Mkutano ule Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Tanga Bwana Maimo Mndolwa alilalamika kwa Rais Magufuli kuwa Serikali inavunja Mkataba kwa kujenga hospitali kwenye maeneo ambayo Kanisa imeachiwa kuwa na hosptali ambazo zinapewa fedha na Serikali.

Amelalamika hivyo kwa sababu Mkataba wa Makanisa na Serikali hauna ukomo. Kila penye hospitali ya Kanisa, Serikali haikutakiwa kujenga hospitali yake. Badala yake, Serikali inatakiwa kuendelea kutoa fedha za kodi kuwapa Makanisa ili ziendeshe hospitali zao na kuimarisha Ukristo kwa kutumia jasho la Watanzania.

Katika kusisitiza madai yake, Askofu Mkuu alitoa ushahidi wa hospitali zilizojengwa na Serikali katika …
Wilaya ya Ifakara, Ngara na Muheza ambazo kwa mujibu wa Mkataba wa 1993, Serikali haikutakiwa kujenga hospitali hizo za Wilaya.

Kitendo cha Serikali kujenga hospitali hizo kinatafsiriwa na Kanisa kuwa Serikali imevunja Mkataba kwa sababu sasa inatoa huduma hiyo muhumu kwa wananchi.

Askofu Mkuu alifafanua kua matatizo haya yapo kwenye ngazi ya Wilaya kwa sababu kwenye ngazi za juu, hakuna tatizo kwa kuwa kuna Msimamizi anaesimamia Mkataba huo.

Hapa Askofu Mkuu alikuwa ana maana kuwa hospitali za KCMC ya Moshi, Bugando ya Mwanza na CCBRT ya Dar es Salaam ambazo zote ni mali ya Kanisa bado zinaendelea kupata fedha za kodi huku zikiendelea kuwalipisha wananchi kwa huduma wanazopewa kwenye hospitali hizo.

Rais Samia Suluhu Hassan alifanya Mkutano na Baraza la Maaskofu la Kanisa Katoliki Tanzania uliofanyika Kurasini tarehe 25 Juni 2021. Katika risala yao, Baraza la Maaskofu limeilaumu Serikali kwa kujenga hospitali zake kinyume cha Mkataba wa 1992, na Makanisa.

Kwenye risala hiyo, Baraza la Maaskofu limeshangaa kuona Serikali inajenga hospitali kwenye Wilaya ambazo Makanisa tayari yana hospitali zao. Wamehoji kwa nini kuwepo na ushindani wa kutoa huduma hizo?

Kwa maana nyepesi, kwa nini Makanisa yasiachiwe kuendesha hospitali maisha (milele) na kuendelea kupewa ruzuku zinazotokana na kodi za wananchi?

Risala hiyo ni ya chombo cha juu kabisa katika Kanisa Katoliki ambao leo viongozi hao hao wanaohoji na kulalamika kuhusu makubaliano ya Serikali na DP World kuwa hayana ukomo!

Kanisa hilo hilo ambalo linapiga kelele kuhusu mkataba wa Serikali na DP World, ndilo ambalo kiongozi wake Askofu Method Kilaini alipewa shs. 80.9 milioni, Askofu Eusebius Nzigirwa alipewa shs. 40.4 milioni na Mchungaji Alphonce Twimanye Simon alipewa shs 40.4 milioni fedha za Rushwa zilizotokana na kashfa ya akaunti ya Tegeta ESCROW.

Hadi leo Kanisa halijatangaza hadharani hatua za kinidhamu iliyowachukulia viongozi hao. Ukimya huu tuutafsiri vipi? Kwa ukimya huu, Kanisa linapata wapi “moral authority” ya kupinga mkataba wa DP World.
Ni kweli kabisa 100% na si kanisa tu pia marais wastaafu waislamu, mzee mwinyi, JK na huyu Samia na mawaziri waislamu waliowhai kuwa mawaziri wa afya kama Ummy Mwalimu na Hussein Mwinyi wanatakiwa wajibu kwa nini hawakufuta MOU hii.
 
Serikali ya Mkapa ilichukua Chuo Kikuu cha Taasisi ya Serikali kilichokuwa Morogoro na kuwapa waislamu watumie kama Chuo Kikuu chao na hamna mmisheni aliyelalamika. Na tuambie kama waislamu wanasoma bure katika hicho Chuo Kikuu chenu.

Huu Mkataba unaopigia kelele ulihusu shule na hospitali zilizojengwa na taasisi za kidini ambazo serikali ilitaifisha . Tuambieni ni taasisi ngapi za kiislamu ambazo hospitali zao zilitaifishwa na serikali?

Kanisa halina mamlaka au nguvu za kuizuia serikali kujenga hospitali sehemu yeyote wanayotaka. Wanachofanya ni kutoa ushauri kuwa ni bora serikali itumie resources zake kujenga hospitali mahali ambapo hakuna kabisa hospitali kuliko kujenga mahali ambapo tayari kuna hospitali ambayo inatoa huduma hizo kwa gharama nafuu. Kama hauoni mantik ya ushauri huu basi hauwatakii mema watanzania ambao hadi leo wanasikia huduma za hospitalikwenye redio tu. Hii MoU imewawezesha watanzania wengi bila kujali dini zao kupata huduma bora na kwa gharama ndogo kuliko ambavyo serikali ingeweza kutoa kwa kutegemea tu resources zake yenyewe.

Amandla...
Ujanja ujanja tu huo kama wa sungura.Na itakuwa hukusoma hayo malalamiko yote.Umeambiwa viongozi wa kanisa wamewahi kulalamika mikutanoni na pia kuandika barua kulalamika kwanini serikali inajenga hospitali maeneo yao.
 
Kama kuna mikutano inayozungumzia mikataba mibovu basi kusiwe na ubaguzi.Muda umefika sasa wa kuitaja mmoja mmoja. Mengine irekebishwe na mingine ipo haja ya kuvunjwa mjoja kwa moja

Mpaka sasa wale wanaokosoa mkataba wa bandari naona wamekaa kimya kwa mkataba ule wa kanisa na serikali wa mwaka 1992.Si lazima wausome wote hata kutaja tu udhaifu wa hoja za wale wanaotilia shaka mkata huo ingetosha kusawazisha hoja za utetezi wa zinazoonekana kasoro za mkataba wa DP World.

Naamini wote walikuwa wanaujuwa na kama ilikuwa bado basi wamesikia kelele za walalahoi.Kelele hizo ni kama hizi kwenye bandiko hapo chini :

WAKATI MNAPAMBANA KUONDOA KIFUNGU HEWA CHA MKATABA WA MILELE (ambacho hakipo) WEKENI NA AKIBA YA MANENO.

TUKUMBUKE MWAKA 1992

Mwaka 1992, Serikali iliingia Mkataba na Makanisa kupitia Taasisi zao za TEC na CCT. Chini ya Makubaliano yale, hospitali za Makanisa zitatumika kwa wananchi wote pale ambapo Serikali haina hospitali.

Kwa kufanya hivyo, Serikali itakuwa na wajibu wa kuyapa Makanisa fedha za kuendesha hospitali hizo ingawa umiliki wa hospitali utabaki kuwa wa Makanisa.

Ifahamike kuwa fedha hizo zinatokana na kodI za Watanzania wote; Waislamu, Wakristo, Mabaniani, Magoha, Makadiani, na hata wale wasio na dini.

Nini athari za Mkataba huu ? Mkataba huu wa kibaguzi una athari nyingi. Kwanza:

Serikali inatumia kodi za wananchi kuyapa Makanisa kuendesha shughuli zake za kuimarisha Ukristo.

Tunasema hivyo kwa sababu utaratibu unaotumika ni kuwa Serikali inatoa fedha kwa Makanisa ambayo wao ndio wanapanga matumizi ya fedha zile na sio Serikali.

Pili, kwenye Jamii, Makanisa yanaonekana ndio yanatoa huduma za Jamii na hivyo kujenga saikolojia kwa wananchi kuwa Ukristo ndio unajali wananchi.

Athari ya tatu ni kuwa Makanisa yananyonya wananchi kwa sababu pamoja ya kuwa hospitali zile zinapata fedha kutoka Serikalini, bado wananchi wanalipia huduma.

Nne, Mkataba hauna ukomo, yaani ni wa milele. (Wakristo wataendelea kupewa hayo mabilioni na Waislamu watanyimwa milele).

Kwa tafsiri nyingine ni kuwa Serikali imejivua kwenye wajibu wa kutoa huduma za Jamii na kuchagua Makanisa kuwa ndio wakala wake.

Tunapenda kuwakumbusha Watanzania kuwa wakati Mkataba huo unasainiwa aliyesaini Mkataba ni Bwana Edward Lowassa aliyekuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu. Huyu ni Mkristo

Kwa utaratibu wa Serikali, Lowassa alikuwa Waziri wa Nchi, hivyo basi Waziri mwenye dhamana ni yule mwenye ofisi yake kwa maana ni Waziri Mkuu.

Wakati unatiwa saini Mkataba, huo Waziri Mkuu alikuwa John Samwel Malecela ambaye ni Mkristo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ndie aliyeishauri Serikali isaini Mkataba ule ambao kwanza hauna ukomo (mkataba wa maisha) na pili unatumia kodi za wananchi kuimarisha Ukristo alikuwa Damian Lubuva ambaye ni Mkristo.

Kwa upande wa Kanisa mwanasheria wao alikuwa Prof Balozi Costa Mahalu, Mkristo.
Kwa maana hiyo, upande wa Serikali, Mkataba ule umeasisiwa na kusimamimwa na Wakristo watupu. Waziri wa Nchi Mkristo, Waziri Mkuu Mkristo, Mwanasheria Mkuu Mkristo.

Ni Wakristo! Wakristo! Wakristo!

Kama kwenye hoja ya makubaliano ya Bandari ni Wazanzibari wawili (ambao ni Waislamu) wamesaini makubaliano ya kuiuza Tanganyika, Mbona Waislamu hawakulalamika pale Wakristo 3 wazito Serikalini walipobuni mbinu za kutumia kodi za wananchi kuimarisha dini yao Ukristo Tanzania?

Kama hoja ni ukomo wa mkataba, mbona Mkataba huu wa Serikali na Makanisa hauna ukomo? Ni mkataba wa milele na ndio maana mpaka leo (miaka 30 sasa) bado unaendelea kutumika.

Bado Serikali inaendelea kutekeleza Mkataba wa kibaguzi ambapo inatumia kodi za wananchi wote kuimarisha shughuli za Kanisa.

USHAHIDI

Tarehe 23 Januari 2019, Rais Magufuli alikutana na viongozi wa dini zote IKULU. Kwenye Mkutano ule Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Tanga Bwana Maimo Mndolwa alilalamika kwa Rais Magufuli kuwa Serikali inavunja Mkataba kwa kujenga hospitali kwenye maeneo ambayo Kanisa imeachiwa kuwa na hosptali ambazo zinapewa fedha na Serikali.

Amelalamika hivyo kwa sababu Mkataba wa Makanisa na Serikali hauna ukomo. Kila penye hospitali ya Kanisa, Serikali haikutakiwa kujenga hospitali yake. Badala yake, Serikali inatakiwa kuendelea kutoa fedha za kodi kuwapa Makanisa ili ziendeshe hospitali zao na kuimarisha Ukristo kwa kutumia jasho la Watanzania.

Katika kusisitiza madai yake, Askofu Mkuu alitoa ushahidi wa hospitali zilizojengwa na Serikali katika …
Wilaya ya Ifakara, Ngara na Muheza ambazo kwa mujibu wa Mkataba wa 1993, Serikali haikutakiwa kujenga hospitali hizo za Wilaya.

Kitendo cha Serikali kujenga hospitali hizo kinatafsiriwa na Kanisa kuwa Serikali imevunja Mkataba kwa sababu sasa inatoa huduma hiyo muhumu kwa wananchi.

Askofu Mkuu alifafanua kua matatizo haya yapo kwenye ngazi ya Wilaya kwa sababu kwenye ngazi za juu, hakuna tatizo kwa kuwa kuna Msimamizi anaesimamia Mkataba huo.

Hapa Askofu Mkuu alikuwa ana maana kuwa hospitali za KCMC ya Moshi, Bugando ya Mwanza na CCBRT ya Dar es Salaam ambazo zote ni mali ya Kanisa bado zinaendelea kupata fedha za kodi huku zikiendelea kuwalipisha wananchi kwa huduma wanazopewa kwenye hospitali hizo.

Rais Samia Suluhu Hassan alifanya Mkutano na Baraza la Maaskofu la Kanisa Katoliki Tanzania uliofanyika Kurasini tarehe 25 Juni 2021. Katika risala yao, Baraza la Maaskofu limeilaumu Serikali kwa kujenga hospitali zake kinyume cha Mkataba wa 1992, na Makanisa.

Kwenye risala hiyo, Baraza la Maaskofu limeshangaa kuona Serikali inajenga hospitali kwenye Wilaya ambazo Makanisa tayari yana hospitali zao. Wamehoji kwa nini kuwepo na ushindani wa kutoa huduma hizo?

Kwa maana nyepesi, kwa nini Makanisa yasiachiwe kuendesha hospitali maisha (milele) na kuendelea kupewa ruzuku zinazotokana na kodi za wananchi?

Risala hiyo ni ya chombo cha juu kabisa katika Kanisa Katoliki ambao leo viongozi hao hao wanaohoji na kulalamika kuhusu makubaliano ya Serikali na DP World kuwa hayana ukomo!

Kanisa hilo hilo ambalo linapiga kelele kuhusu mkataba wa Serikali na DP World, ndilo ambalo kiongozi wake Askofu Method Kilaini alipewa shs. 80.9 milioni, Askofu Eusebius Nzigirwa alipewa shs. 40.4 milioni na Mchungaji Alphonce Twimanye Simon alipewa shs 40.4 milioni fedha za Rushwa zilizotokana na kashfa ya akaunti ya Tegeta ESCROW.

Hadi leo Kanisa halijatangaza hadharani hatua za kinidhamu iliyowachukulia viongozi hao. Ukimya huu tuutafsiri vipi? Kwa ukimya huu, Kanisa linapata wapi “moral authority” ya kupinga mkataba wa DP World.
Karibu uendelee kutibiwa na wanao waendelee kupata elimu bora.

Leo Ndiyo serikali inahimiza ujenzi was zahanati za Kijiji, ushajiuliza hawa watu walikuwa wanatibiwa katika hospital zipi. Na hata leo wakikosa matibabu wataenda wapi kutibiwa . Ni ktk hospital za misheni sababu Hiyo ya serikali haipo na km ipo haina dawa, wahudumu wala vifaa tiba.

Uislam unajaza watu Ujinga kichwani Sana.
 
Ishaurini serikali sikivu irudishe kwa kanisa hospitali nyingi nchini za kanisa ili ziwahudumie walengwa na ziwe private.
Kuna hospitali za KCMC na Bugando na nyingine nyingi tu.
Na tusiishie katika mahospitali.
Shule za Misheni na za makanisa ni bora zirudi tu kwa wenyewe.
Kama serikali inafuata ushauri kama huo basi ni heri.Chukueni kila hospitali munayoona ni ya kwenu hata ikiwa si kweli lakini baada ya hapo MOU ife na muendeshe wenyewe na wengine waendeshe wenyewe.Ardhi Tanzania ipo na watu kila siku wanajenga maeneo mapya.
 
Dp world anaahidi kujenga misikiti. Ntaenda kutibiwa msikitini.

Amkeni toka usingizini.

Nikimsikia muislamu analalamikia vitu km hivi nachekaga Sana.

Wakristo wanajenga kanisa sambamba na shule na hospitali. WENZANGU mmekalia majungu tu. Msikiti siyo maendeleo.

Pigeni kelele sababu Ni wajinga Sana nyie baadhi ya Muslims.
 
Makosa ya wengine hayafuti makosa ya Samia. Ya Samia tutayakabiri kama yalivyo na memgine kama yalivyo.
Wewe thinking capacity yako ni poor, unalinganisha escrow na uuzwaji wa bandari, maziwa, anga etc etc ...
Haitasaidia mnapoteza muda.

Lastly nyinyi hamna hospitali za maana sana sana mnanufaika na huduma ya makanisa ya hospital, shule etc etc
Hiyo yote ni kutapatapa ili kutaka kupoteza hoja ya Samia kusaini mkataba wa kifisadi na DpWorld!! Kama mna hoja na mikataba mingine mje nazo baada ya kumalizana na Samia na sio kutaka kuwandoa watu kwenye hoja ya KITAIFA ya kulinda rasilimali za nchi kwa faida ya vizazi vijavyo!!
 
Kama serikali inafuata ushauri kama huo basi ni heri.Chukueni kila hospitali munayoona ni ya kwenu hata ikiwa si kweli lakini baada ya hapo MOU ife na muendeshe wenyewe na wengine waendeshe wenyewe.Ardhi Tanzania ipo na watu kila siku wanajenga maeneo mapya.
Hayo ni maneno ya mtu aliyefaidika na uwekezaji wa makanisa , halafu wivu unamjaa moyoni na kufurika.
 
Huu ni uamuzi wa busara na wa kuepusha shari.Chukueni hospitali zote munazosema ni za kwenu na zilizojengwa kwa kodi zetu sote halafu MOU kufutwa musiingilie uhuru wa kujenga.Hapo zamani wahindi walitaifishiwa mali zao na wengi wakakimbia ilikuwaje.Majumba muliyoyafanyia choyo mbona yamebaki magofu.Na hospitali zenu bila MOU nazo zitakuwa magofu.
 
Mimi sijauona huo mkataba .

Ila nitachangia kama ifuatavyo , je kwenye huo mkataba kuna sehemu imekataza waislamu kujenga hospitali?

Maana kwa ulivyoandika ni kuwa serikali ndio ilikatazwa ila hakuna katazo kwa waislamu so waislamu ruksa kujenga.
 
Huu ni uamuzi wa busara na wa kuepusha shari.Chukueni hospitali zote munazosema ni za kwenu na zilizojengwa kwa kodi zetu sote halafu MOU kufutwa musiingilie uhuru wa kujenga.Hapo zamani wahindi walitaifishiwa mali zao na wengi wakakimbia ilikuwaje.Majumba muliyoyafanyia choyo mbona yamebaki magofu.Na hospitali zenu bila MOU nazo zitakuwa magofu.
Mkuu utaugua tu, zikirudishwa , halafu itabidi ulipie gharama full 100%
 
Napenda sana viongozi wa madhehebu ya kikristo
Ni watu makini wana elimu ya kawaida na elimu ya dini
Na ata nyie mashia mnaruhusiwa kujenga hospitali na kuingia mkataba na serikali kama kanisa lilivyofanya.
Hapana, hatutaki dini ichanganywe na serikali.

Wangekuwa na elimu wangebanduana?
 
Makosa ya wengine hayafuti makosa ya Samia. Ya Samia tutayakabiri kama yalivyo na memgine kama yalivyo.
Wewe thinking capacity yako ni poor, unalinganisha escrow na uuzwaji wa bandari, maziwa, anga etc etc ...
Haitasaidia mnapoteza muda.

Lastly nyinyi hamna hospitali za maana sana sana mnanufaika na huduma ya makanisa ya hospital, shule etc etc

Samia kosa lake nini?

Au wema wake ndiyo kosa lake?
 
Back
Top Bottom