Milion 10 inatosha kuanzisha biashara ya Baa?

Naona yeye ametaja mtaji wake tu huenda kutokana na ujuzi duni juu ya biashara husika ameitaja kama bajeti ?
Yeah na mimi nikamrekebisha na kumpa ushauri ninaouona kuwa ni mzuri kwake.
Ana uhuru wa kuuchukua au kuuacha. Upande wangu sitaathirika na chochote.
 
Namaanisha budget haielezewi kihivyo. Au wewe unaona kuwa hiyo aliyoielezea ni budget?
Kuanzisha Bar at least awe na 30m.
Alafu anasema afungue bar aweke wahudumu wa3, hivi anajua anachokiongea kweli huyu?? Ili bar iuze inahitaji wahudumu wa kutosha hapa namaanisha bila kuweka wahudumu utatafuta san waganga yaan utachelewa sana! Labda kam unaingia kujaribu biashara! Kuna bar moja Maarufu Mbey niliwahi kwend ina wahudumu 70 inawez kuwa si kweli lakin yule jamaa anauza vibaya mno yaan ukifika saa 2 usiku hamna pa kukaa😂😂😂😂😂
 
Kwanza wahudumu wenyewe tu wanavuta wateja kwa kiasi kikubwa.
 
Mkuu una milioni 10 alafu unakimbilia sehemu ya Kodi ya milion 3 kwa mwezi???? Strange
Shida sio kodi suala ni kujiuliza iyo sehemu imaweza ingiza faida kias gan

Ata soko kuu la kariakoo kodi yake sehemu nying huanzia million 3 ila watu wanapanga sabu wanajua return yake ni kubwa
Mi sio mkazi wa dar ila kwa uelewa wangu dar vitu ving bei nafuu
Tv,mziki mzito,viti, jokofu ni bei poa na ata used unaweza pita
 
Mkuu hii biashara kwa sehemu kama dar ina ushindani mkubwa sana kulinganisha na sehem zingine hvyo hawezi kuifanya local tu akategemea atawini kirahisi hvyo na sikuhizi watu wamejiongeza sana kweny hii biashara kwenye kujibrand mpka mitandaoni sasa akianza tu kma waliofungua bar miaka ya 90 huko lazima aangukie pua!
 
Sikuhizi kuna watu wenye akili, (smart people) wao wanafikilia jinsi ya kuiondoa bidhaa yako sokoni
 
HAKIKISHA KUWA NA MGANGA NA UZIZI USHIKE KASI HAPO KWENYE BAR YAKO
 
Kama ni kuuza nyapu hapo Sawa ila kama pombe mtaji hautoshi
Cc: ephen_
 
theory nyingi sana! sina uzoefu na bar ila nina uzoefu wa biashara zingine iyo ni tofauti na mtu ambaye hajawai fanya biashara kabisa.
Unapenda ubishi, league na ujuaji wakati umeomba ushauri, una haki ya kuchukua ushauri au kuuacha ila sio kuzodoa na kupingana na wanaokushauri.

Kulingana na vigezo vya baa yako unayotaka, nenda kanunue huo mziki mkubwa, tafuta wadada watatu kama unavyotaka, lipa kodi (kama ambavyo ulienda kuulizia kodi hapo Kibo ambayo ni prime area).

Fanya yote hayo kwa kutumia 10M
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…