Milion 10 inatosha kuanzisha biashara ya Baa?

Milion 10 inatosha kuanzisha biashara ya Baa?

bar nazielewa kama unataka kupoteza pesa yako mda mfupi usifungue bar.
Naelewa tabia za bar kwanza zina shiriki nyingi,pili zinataka madanguro mfano kubadilisha wahudumu ili wateja kuchangamkia
Bora mkuu utusaidie kumwambia huyu mtu kwa sabub ana kichwa kigumu halafu hakuna kitu anaelewa ni ubishi tu na kuvimba kichwa!
 
Unapenda ubishi, league na ujuaji wakati umeomba ushauri, una haki ya kuchukua ushauri au kuuacha ila sio kuzodoa na kupingana na wanaokushauri.

Kulingana na vigezo vya baa yako unayotaka, nenda kanunue huo mziki mkubwa, tafuta wadada watatu kama unavyotaka, lipa kodi (kama ambavyo ulienda kuulizia kodi hapo Kibo ambayo ni prime area).

Fanya yote hayo kwa kutumia 10M
Mkuu T14 Armata unaweza kuta tunabishana na mtu ambaye hata hizo 10mil hana yaan yupo kupiga tu porojo hapa! 😀😂😂
 
MWACHE KWANZA NI LAANA ITAMPIGA MPAKA FAMILIA YAKE
Kitu ambacho watu huwa hawajui wengi wanaofungua mabar makubwa, night club, sehem zote za starehe kubwa n.k wanakuwa wamepiga hela zao haramu km utakatishaji fedha, madawa ya kulevya, ujambazi na mengine mengi na weng hufanya kama kivuli cha kujificha wasigundulike kirahisi mtu anatia hata m100 kwenye bar kubwa tu lakin sio kwa kujichanga sijui mil 10 ndo ufungue bar ikimbize mjini huo ni uongo usiopingika.
 
Mkuu uko sahihi. Lakini hapa unaweza kutukanwa ukisema hivi. Jinsi alivyouliza tu tayari kuna possibility kubwa ya kufeli kama atafanya. Kwa nini? Hajazingatia uliyomwambia.
Pia hakuna mchanganuo wa biashara wa aina zote kwasababu kila biashara inachangamoto zake labda Ile inayofanana nayo lakini pia lazima uchunguze upinzani uliopo, (ushindani). Na wateja wako taraji naamini tutajenga jamii yenye kuelewa japokuwa kwenye biashara kuna yasiyoyatarajiwa ambayo mengine husababishwa na binadamu kwakutokujua ama kwa makusudi, (uncertainty),mara nyingi wateja wa bia niwalewale inategemea utakavyo wavuta kwako
 
Wamilliki wa bar wamevamia Uzi kumkatisha tamaa huyu mwamba.

Pole sana mkuu umeona competitors wako walivyo na roho mbaya ?

Ukitaka fundi wa kuzindika na kuvutia wateja kwenye biashara yako mpya nitafute.
 
Kama huna sifa hata moja kati ya hizo za wajasiriamali huwezi kufanya biashara yoyote, mimi ni muelimishaji elimu ya ujasiriamali kwa vitendo na pia naandika kitabu cha ujasiriamali, ambacho utakisoma unakiweka kwapani unaanzisha biashara, (simama dede), karibu

Tupe tips ya vinywaji vya jumla kaka
 
Tupe tips ya vinywaji vya jumla kaka
Usome Uzi huu kuna mdau anavyo vinywaji vya jumla swali fikirishi hivi huwa mnasoma na kuelewa? Mimi naweza kuandika mchanganuo wa biashara mbalimbali ambayo imefanyiwa utafiti wa soko, (andiko la mpango wa biashara,) hata hivyo wauzaji wa vinywaji vya jumla wametapakaa mtaanii
 
Back
Top Bottom