Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,973
Taingia juzi akaunti yangu kwenye benki ya CRDB imepunguzwa balance kiasi cha Milioni 1.7. Cha kushangaza sijawahi fanya huo muamala.
Nimejaribu kuandika email CRDB hawajajibu. Nimewasiliana kupitia pages zao za Social Media hawajajibu.
Leo ni siku ya 3 kiasi hicho hakijarudi na nikiomba Bank statement, transaction ya mwisho inayoonekana kwenye mfumo ni ya tarehe 8 mwezi huu. Malalamiko haya sio mimi tu. Kuna Watanzania wengi sana wanatoa same Malalamiko kwenye mitandao ya Kijamii na mitaani.
Kuna uwezekano kuna the largest bank heist imefanyika Tanzania kwenye hii bank ya CRDB. Kuna uwezekano kiasi hiki kilichoibwa ni kikubwa zaidi kuwahi kuibwa hata Afrika nzima kama sio Afrika Mashariki yote.
Swali ninalojiuliza wako wapi Benki Kuu ya Tanzania kutoa tamko kwenye hili?
Wako wapi Financial Intelligence Unit kutoa tamko kwenye hili?
Wako wapi TAKUKURU kutoa tamko kwenye hili?
Iko wapi Ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai kutoa tamko kwenye hili?
Wako wapi Financial Crimes Centre kutoa tamko kwenye hili?
Wako wapi Jeshi la Polisi kutoa tamko kwenye hili?
Iko wapi Serikali hasa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha kutoa tamko kwenye hili?
Nilitegemea hadi sasa kwa kuwa nchi yetu haina wataalam waliobobea wa IT tamko lingekuwa limeshatolewa na hadi muda huu Serikali ingekuwa imeshaomba msaada iwe kwa Jeshi la Polisi la China ( Marafiki wa CCM) au Polisi wa Uingereza/ Marekani au Israel kuja kusaidia uchunguzi na kuhakikisha Wahusika wanakamatwa na hela husika zinarudi.
Hii nchi sasa ifike wakati Wananchi tufanye kama Nepal