Milo mitatu kama hufanyi kazi ngumu ni tamaa na ulafi tu

Watu wengi hawajawahi ku experience njaa, Njaa wanazosisema ni hizi ambazo imetokea kuvurugika tu kwa ratiba ya Milo yao mfano mtu mwenye ratiba ya kula Milo mitatu ndani ya mda Fulani ikitokea amechelewa kula ndani ya mda huo atakwambia anahisi njaa ila njaa, njaa kweli ni Ile ambayo mtu anatoboa kuanzia masaa 12 na kuendelea bila kula chochote
Mimi nikitoboa masaa 12 huwa sihisi njaa kabisaaaaaa
 
Acha kabisa, msosi ni muhimu jombaa.

Kuna kipindi nikipitia msoto mpaka kwenda toi ukibanwa na gogo unaogopa, maana unaenda kutoa nini huku na hujala chochote cha maana, nikitoa hiki si ndo tumbo litabaki tupu kabisa.

Hapo umechapa uji tu maana unga hata ugali hautoshi.
Msoto wa njaa sio mchezo tumbo lenyewe unalisikia likikupa taarifa Kwa mitetemo na miungurumo mixture kawenge flani hivi kama cha mlevi
 
Kwanza tufahamu utaratibu wa milo mitatu ni utamaduni wa magharibi ulioibuka karne ya 17 kutokana na mambo mengi mojawapo ikiwa ni mapinduzi ya viwanda yaliyowafanya wafanyakazi wanaofanya kazi ngumu wahitaji kula mara nyingi kuhimili kazi ngumu. Kabla ya hapo binadamu wengi walikuwa wanakula mlo mmoja au miwili kwa siku.

Kwa upande wa daraja tawala na mabepari huko magharibi wao baada ya mafanikio ya kiuchumi walianza kula milo mitatu kama anasa na kufanya networking, baadaye karne ya 19 huko Marekani suala la breakfast(kifungua kinywa) liligeuzwa biashara zaidi baada ya jamaa mmoja kusahau kubeba mahindi yake aliyochemsha kula kazini na yakaharibika ndipo likamjia wazo la kutengeneza cornflakes kwa kuyakandamiza kama chapati na kuyaanika kuyafanya yadumu zaidi, ndipo wazungu wakaibuka na bidhaa chungunzima za breakfast.

Leo hii mtu anakula asubuhi na mchana anashinda dukani, saloon au ofisini anabonyeza keyboard tu ndio mwanzo wa janga la kiribatumbo na vitambi kwa wanawake na wanaume.
Toa njaa zako. Nenda Chato. asubuhi supu la sato na Ugali, mchana ugali na nchima +Usiku ugali kamongo.
 
Sisi tunaokula milo mitano na hatuna kiriba tumbo unene ulopitiliza au kitambi jee
Kwanza tufahamu utaratibu wa milo mitatu ni utamaduni wa magharibi ulioibuka karne ya 17 kutokana na mambo mengi mojawapo ikiwa ni mapinduzi ya viwanda yaliyowafanya wafanyakazi wanaofanya kazi ngumu wahitaji kula mara nyingi kuhimili kazi ngumu. Kabla ya hapo binadamu wengi walikuwa wanakula mlo mmoja au miwili kwa siku.

Kwa upande wa daraja tawala na mabepari huko magharibi wao baada ya mafanikio ya kiuchumi walianza kula milo mitatu kama anasa na kufanya networking, baadaye karne ya 19 huko Marekani suala la breakfast(kifungua kinywa) liligeuzwa biashara zaidi baada ya jamaa mmoja kusahau kubeba mahindi yake aliyochemsha kula kazini na yakaharibika ndipo likamjia wazo la kutengeneza cornflakes kwa kuyakandamiza kama chapati na kuyaanika kuyafanya yadumu zaidi, ndipo wazungu wakaibuka na bidhaa chungunzima za breakfast.

Leo hii mtu anakula asubuhi na mchana anashinda dukani, saloon au ofisini anabonyeza keyboard tu ndio mwanzo wa janga la kiribatumbo na vitambi kwa wanawake na wanaume.
 
Janabi alishasema unatakiwa ule pale unapohisi njaa tu siyo unakunywa chai kwasababu ni Asubuhi kama hauhisi njaa skip breakfast kula hata saa 6 mchana ikifika muda wa lunch huskii njaa skip had saa 11 jion ndo ule, usiku siyo muhimu sana kula kama unataka kula usiku basi kula masaa matatu kabla ya kulala
Yule sio timamu ukimfuata atakuponza. Kasema sana Hadi akanganyikiwa na kusahau alikuwa ana somea Nini.

Niliacha kumsikiliza pale aliposema yeye anashindia maji ya vuguvugu mara ana kula ugali na tomato sauce tu
 
Milo mitatu tumerithi kwa wakoloni
Mkuu kwa muktadha wako huu basi kila kitu tumerithi kwa wakoloni

Nikikwambia unitajie vitu ambavyo sio vya “wakoloni” utapata tabu sana kuvitaja mkuu

Wewe ungekuja tu na hoja yako kwamba ulaji unatakiwa kuwaje dhidi ya ulaji uliopo
 
Yule sio timamu ukimfuata atakuponza. Kasema sana Hadi akanganyikiwa na kusahau alikuwa ana somea Nini.

Niliacha kumsikiliza pale aliposema yeye anashindia maji ya vuguvugu mara ana kula ugali na tomato sauce tu
Janabi amesema anakula ugali??
 
Back
Top Bottom