Majina tu hayo bro. Labda kama neno breakfast ndio tuseme limeletwa na Wazungu but asubuhi watu wanao fanya kazi ngumu walikua wanakula, tena ugali mkubwa tu, sio chai kama sasa. Jamii za wafugaji as well, nao walikua wanakula kwanza asubuhi ndio wanakwenda kuchunga mifugo yao, labda hawa mchana ndio walikua wana kunywa kunywa zaidi na zio kula or else maporini huko walikua wanakula matunda, mizizi na hata nyama pori as well.
Guys iko hivi, kinacho haribu afya zetu kwasasa sio idadi ya milo, ni aina ya vyakula tunavyo kula, sasa hivi tunakula junk food. Nyama za kopo, aina upishi wake nao ni changamoto, nyama ina mafuta but unatia mafuta mengine tena, chumvi hiyo. Ugali tunakula uliokobolewa kwenye machines, wazee wetu walikua wanatumia vinu kuandaa chakula chao; umewahi kujiuliza vile vyuma vinavoishaga kwenye zile machine za kusaga na kukoboa, particles zake zinaendaga wapi? Or vinaishaje? Njoo kwenye viungo vyetu kama mbogq mboga, nyanya, vitunguu hata hayo mahindi yenyewe, full dawa; hizo dawa zinaendaga wapi kama sio miilini mwetu? Njoo kwenye mayai, yai limetengenezwa bila jogoo, litakua na protein ya wapi? Samaki, dagaa nk vyote hizo ni dawa tu. So kula mlo mmoja au 2 kama with those chemicals, what do you expect?