Milo mitatu kama hufanyi kazi ngumu ni tamaa na ulafi tu

Milo mitatu kama hufanyi kazi ngumu ni tamaa na ulafi tu

Acha kabisa, msosi ni muhimu jombaa.

Kuna kipindi nikipitia msoto mpaka kwenda toi ukibanwa na gogo unaogopa, maana unaenda kutoa nini huku na hujala chochote cha maana, nikitoa hiki si ndo tumbo litabaki tupu kabisa.

Hapo umechapa uji tu maana unga hata ugali hautoshi.
Ungejitihadi uwe unakula mboga za majani mkuu ambazo ni bei rahisi tu mtaani.
 
Hili suala hata mimi limenifikirisha sana na nimeanza kulifanyia kazi yapata miezi miwili sasa. Najaribu ku eliminate msosi wa usiku mostly. Nakunywa chai na vipande viwili vya muhogo kabla ya sa mbili usiku hapo ndio imetoka.
 
Watu wengi hawajawahi ku experience njaa, Njaa wanazosisema ni hizi ambazo imetokea kuvurugika tu kwa ratiba ya Milo yao mfano mtu mwenye ratiba ya kula Milo mitatu ndani ya mda Fulani ikitokea amechelewa kula ndani ya mda huo atakwambia anahisi njaa ila njaa, njaa kweli ni Ile ambayo mtu anatoboa kuanzia masaa 12 na kuendelea bila kula chochote
Kuna ile unapigwa njaa mpaka nguvu za kutembea unakosa.

Au kutwa nzima unashindia andazi la mia mbili. Au maembe ya mia mbili.

Hii imenipiga kipindi fulani.
 
Kwanza tufahamu utaratibu wa milo mitatu(breakfast, lunch na dinner) ni utamaduni wa magharibi ulioibuka karne ya 17 kutokana na mambo mengi mojawapo ikiwa ni mapinduzi ya viwanda yaliyowafanya wafanyakazi wanaofanya kazi ngumu wahitaji kula mara nyingi kuhimili kazi ngumu. Kabla ya hapo binadamu wengi walikuwa wanakula mlo mmoja au miwili kwa siku.

Kwa upande wa daraja tawala na mabepari huko magharibi wao baada ya mafanikio ya kiuchumi walianza kula milo mitatu kama anasa na kufanya networking, baadaye karne ya 19 huko Marekani suala la breakfast(kifungua kinywa) liligeuzwa biashara zaidi baada ya jamaa mmoja kusahau kubeba mahindi yake aliyochemsha kula kazini na yakaharibika ndipo likamjia wazo la kutengeneza cornflakes kwa kuyakandamiza kama chapati na kuyaanika kuyafanya yadumu zaidi, ndipo wazungu wakaibuka na bidhaa chungunzima za breakfast.

Leo hii mtu anakula asubuhi na mchana anashinda dukani, saloon au ofisini anabonyeza keyboard tu ndio mwanzo wa janga la kiribatumbo na vitambi kwa wanawake na wanaume.
Kazi ngumu unaipima vipi
 
Sina cha kuongeza hapa bro; umemaliza kila kitu. Unakuta wale wazee ana wanawake hadi 5 na wote anawapiga mimba kila mwaka, mzee 1 anapiga copy (watoto) zaidi ya 20; leo inashindikana sio kwasababu ya idadi ya milo, ni aina ya vyakula tunavokula na namna tunavyo pika. Zanzibar todate hawanaga diner, angalia idadi ya watoto wanao zaliwa kule but nenda Kigoma, mikoa yote ya kanda ya ziwa except Kagera, familia 1 unakuta mzee kazaa watoto zaidi 12 tena kwa mke 1 na mzee huyo anapiga milo 3 kawaida tu. Fanyeni utafiti vizuri, hizi habari za kusoma majarida ya Ulaya halafu mnaleta huku sio sawa. Hata idadi ya Wazungu wanao zaliwa kwa mwaka ni ndogo sana kulinganisha na jamii za weusi na Wahindi
Zanzibar hatuna dinner? 🤣🤣🤣
 
Pia hakunaga chai Nzito ni kukosa hela tu
 
Nakula nikihisi njaa, lakini Fanya ufanyavo Ili ulale vizuri usiku hakikisha umekula.
 
Sitasahau Mwaka 2017-2018 nilipatwa na majanga maisha yangu yaliyumba sana, Kuna siku nilikaa siku tatu bila kula..... Namwelewa sana mtoa mada
Huo mwaka na Mimi Nina historia nao wa kupitia maisha magumu ambayo sidhani kama nitakuja kuyapitia
 
Back
Top Bottom