Milo mitatu kama hufanyi kazi ngumu ni tamaa na ulafi tu

mimi binafsi

Nataka kula chochote ila kichanganywe na

Nyanya
Kitunguu
Karoti
Nyanya chungu
Hoho
Birimganya
Embe bichi
N.k



Iwe nyama au utumbo au samaki au yai..ila liwe na mchemsho huo na kwenye fry pain kikaangiwe pale
 
Mimi nikitoboa masaa 12 huwa sihisi njaa kabisaaaaaa
 
Msoto wa njaa sio mchezo tumbo lenyewe unalisikia likikupa taarifa Kwa mitetemo na miungurumo mixture kawenge flani hivi kama cha mlevi
 
Toa njaa zako. Nenda Chato. asubuhi supu la sato na Ugali, mchana ugali na nchima +Usiku ugali kamongo.
 
Sisi tunaokula milo mitano na hatuna kiriba tumbo unene ulopitiliza au kitambi jee
 
Yule sio timamu ukimfuata atakuponza. Kasema sana Hadi akanganyikiwa na kusahau alikuwa ana somea Nini.

Niliacha kumsikiliza pale aliposema yeye anashindia maji ya vuguvugu mara ana kula ugali na tomato sauce tu
 
Milo mitatu tumerithi kwa wakoloni
Mkuu kwa muktadha wako huu basi kila kitu tumerithi kwa wakoloni

Nikikwambia unitajie vitu ambavyo sio vya “wakoloni” utapata tabu sana kuvitaja mkuu

Wewe ungekuja tu na hoja yako kwamba ulaji unatakiwa kuwaje dhidi ya ulaji uliopo
 
Yule sio timamu ukimfuata atakuponza. Kasema sana Hadi akanganyikiwa na kusahau alikuwa ana somea Nini.

Niliacha kumsikiliza pale aliposema yeye anashindia maji ya vuguvugu mara ana kula ugali na tomato sauce tu
Janabi amesema anakula ugali??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…