Milo mitatu kama hufanyi kazi ngumu ni tamaa na ulafi tu

Sehemu kubwa ya mfumo wa maisha yetu tumerithi kwa wakoloni, vitu vingine vina manufaa vingine havina manufaa yoyote kwetu na mojawapo ni huu ulazima wa kula milo mitatu kwa siku kwa raia wengi.
Ndio utueleze sasa kuna ulazima wa kula milo mingapi?
 
Ukweli mchungu kabisa!! Wazee wa zamani hata akila milo miwili bhasi mafuta ni Tetele, alizeti, Nyonyo au karanga !!

Dona, Mikate ya ngano nyeusi, Maboga, magimbi, viazi, Maziwa ya ngombe ambaye hatumii madawa, Hakukuwa na sukari/blueband/Siagi/Yoghurt/Tambi/Chips/Keki .

Mkunugwa wa zamani hata akiumwa dawa zake ni za mizizi na mimea hakukua na vidonge mkuu!!

Mwanamke wa zamani hakuwahi jifungua kwa Operation, Wala hakuna aliyewahi kuwaza kama kuna kitu inaitwa Operation.

Kuna babu yangu alinisimulia kipindi wako vijana ukipata demu kwenye stori zao walikua wanasimuliana labda utasikia "Nimepiga bao5,6,7" kupiga Bao tatu ndio ilikua tatizo la nguvu za kiume

Mimi ni Introvert lakini Nimeamka na Energy sana leo

HA!HA!HA
 
Shamba darasa wetu Dr Janabi anakataza kula kula kila uonapo chakula, ndipo kisukari kinapoibuka kiurahisi.
 
Fafanua kwa kiswahili na mifano yake mkuu. Sisi wa la Saba B umetuacha mbali
 
Sina cha kuongeza hapa bro; umemaliza kila kitu. Unakuta wale wazee ana wanawake hadi 5 na wote anawapiga mimba kila mwaka, mzee 1 anapiga copy (watoto) zaidi ya 20; leo inashindikana sio kwasababu ya idadi ya milo, ni aina ya vyakula tunavokula na namna tunavyo pika. Zanzibar todate hawanaga diner, angalia idadi ya watoto wanao zaliwa kule but nenda Kigoma, mikoa yote ya kanda ya ziwa except Kagera, familia 1 unakuta mzee kazaa watoto zaidi 12 tena kwa mke 1 na mzee huyo anapiga milo 3 kawaida tu. Fanyeni utafiti vizuri, hizi habari za kusoma majarida ya Ulaya halafu mnaleta huku sio sawa. Hata idadi ya Wazungu wanao zaliwa kwa mwaka ni ndogo sana kulinganisha na jamii za weusi na Wahindi
 
Acha watu wale. Huu upuuzi wa kuwekeana sheria umezidi sasa. Eti usile chini ya masaa matatu kabla ya kulala? Ujinga mtupu. Watu wanapambana wale kuzuia tu msiba halafu nyie mnakuja na pigo kama vile watu wote wana uwezo wa kununua hizo balanced diet. Unafahamu ugali na dagaa mchele mixer kachumbari? Kama chakula kipo watu wale hata mara 10 kwa siku. Hizi kampeni za kipuuzi zitazidi kuchangia kuwa na watu waliodumaa, wenye sura mbaya na wasio na akili.
 
Acha watu wale. Huu upuuzi wa kuwekeana sheria umezidi sasa.Hizi kampeni za kipuuzi zitazidi kuchangia kuwa na watu waliodumaa, wenye sura mbaya na wasio na akili.
Watu waliodumaa mwili na akili kama wewe na wenye kwashakoo inatokana na kubugia ugali, uji, viazi, vitumbua, maandazi, mihogo n.k zaidi bila protein ya kutosha. Ili uwe na afya isiyo na udumavu inabidi ule protein nyingi na wanga kidogo lakini bongo mnafanya kinyume chake ndio maana mnadumaa, ukifika mgahawani inatakiwa uagize nyama ugali sio ugali nyama.
 
Kumbuka iwe Nyama iliyotolewa mafuta, lasivyo kitambi na Heart attack hukwepi!!

My wife ananielewa akichemsha nyama, lazima aiache ipoe au ikae kwenye friji yale mafuta yagande then yatolewe ndio Nakula .
 
Mkuu mimi nadhani pia life style ya siku hizi ni tatizo sana
Unakuta mtu ndani ya masaa 24 ametumia zaidi ya masaa 20 kwa kukaa na kulala
Mwili wa binadamu umeumbwa kuwa active wakati mwingi na kupumzika wakati wa usiku 12/12 ndani ya 24hrs

Mwanzoni Nature ya kazi yangu ni kusafiri sana na gari kwenye maeneo ya vijijini na kuzunguka sana kwa miguu nyumba hadi nyumba, mikiki mikiki ilikua ni mingi sana unalala hoi
Ratiba ya kula ilikua shagala bagala lakini tulikua tunakula sana na kunywa sana pombe lakini nilikua na afya bora na uzito stahiki kabisa

Nilipokuja kubadili kitengo nikawa mtu wa kuamka asubuhi naingia ndani gari, nikifika kazini napiga hatua 10 nipo kwenye lift kisha hatua 5 nipo ofisini
Nakaa ofisini hadi saa 10 jioni nikitoka hapo kwenye gari mbio baa, ntakaa baa hadi saa 2 nakwenda home naoga nakula nalala.... ratiba inajirudia tena.
Aisee kitambi kilikuja kwa speed kali, nikaanza uchovu wa mwili, tumbo kujaa gesi, pressure, performance kitandani ikashuka sana na shida zingine kibao

Nikarudi tena kitengo changu cha mikiki mikiki kitambi na shida zote zikaisha aiseee

Mazoezi na kuufanya mwili uwe active ni muhimu mmno
 
Kula mlo mitatu kwa watu wengi ni ulaku/ulafi au anasa tu, milo miwili inawatosha sana.
 
Hapa pia sina cha kuongeza cause hi yako imewahi kunikuta, sema mimi nilikua nafanya kazi za shift but wakati fulani nature ya kazi yangu ilikua kukaa kwenye kiti, mbele computer na full AC, bahati nzuri sikua mnywaji wa pombe kiviiile. Nilibadiri ufanyaji wangu wa kazi na sasa nipo vizuri ingawa pia umri umeanza kunipa mkono. In less than 10 years nitakua pensioners
 
Kuna jamaa yangu siku nimemtembelea nashangaa saa 6 usiku eti anaenda kutafuta msosi kitaa hajala tangu asubuhi..
Nae alikua na hizo pigo, anakula akihisi njaa tu
saa sita usiku akibakwa atamsingizia nani..?
 
Miili yetu imeumbwa tofauti tofauti sana kiutendaji.....kila mmoja kwa namna yake......hakuna formula kwenye maisha ya watu kuhusu mambo ya kula.......

Kuna watu wana high metabolism rate.....kuna watu wana slow metabolism rate.......watu hawa hawawe kufanana kwenye ulaji.......

Na kuna watu wana shughuli maalumu zinazohitaji mlo fulani.......

Jambo la msingi katika hali ya kawaida pasi na dharula ya maladhi...kila mtu mwili wake unamweleza wakati wa kula......kwani kila mtu mwili wake unapokea njaa kwa namna yake.........

Kabla ya kufuata na kupokea maandiko ya mitandaoni kwanza jifunze kusema na mwili wako......usikilize kwa makini mwili wako........ dunia ya sasa taarifa mkononi unapaswa kuwa makini na taarifa za mitandaoni........
 
Umeandika point ila kusema nimedumaa akili umekufuru. God will punish you
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…