GREETINGS.
Haloo wananchi wote wa JF, hamjambo?
Baada ya salamu twende kwenye mada...
INTRODUCTION:-
Mimi ni mtumishi wa umma niliye ajiriwa 2012 na fani x (diploma) kwa level za kata (Afisa wa katani @ SIO MTENDAJI KATA).
2013 nikaenda chuo na kurudi 2018 na masters (niliunga) ya fani y.
Nikiwa na furaha na niite bahati, kurudi tu kazini nikapewa ofisi ya fani y, yaani nilimaliza chuo na kurudi kazini November 2018 na January 2019 nikahamishiwa halmashauri.
Niite bahati kwasababu, imekua ngumu kwa watumishi wengi kutoka Shule tu na ofisi zao za Utumishi wakawabadilishia Kazi zao (rectegorization au kuwahamishia kwenye vitengo walivyosomea).
Nilifanya Kazi kwa furaha na juhudi sana na 2019 nikapokea barua ya kubadilishiwa muundo (recategorization).
Niliona zile ndoto zangu za kuwa mkubwa kama zinaanza kutimia hivi na nilifanya Kazi kwa juhudi sana.
Fani y ndio niliyokuwa naipenda.
Fani x nilisomea tu kwa vile nilikuwa yatima na nilikosaga ada ya kusomea fani y miaka hiyo.
Ila hiyo fani x ndio iliniingiza serikalini.
SCENARIO:-
2020 likatokea jambo kazini, mara TAKUKURU hao, mara CAG huyo, mara kamati ya kutuchunguza hiyo, mara usalama wa taifa huo.
Kifupi vitu vilikuwa vingi, ila iliamriwa tusimamishwe Kazi.
Tukiwa tumesimamishwa Kazi niliamua kufungua biashara.
Baada tu ya kusimamishwa Kazi nilitumia wiki 2 kutafuta frame na kuanza biashara.
Baada ya miezi 7 nikarudishwa kazini na mambo yakaendelea.
Ila biashara yangu ilikuwa ya moto sanaa (inauza sanaa).
PROBLEM.
Baada ya kurudi kazini Kuna mambo nikaona yamebadilika.
1. Upendo na ile Kazi ukapoteaaa kabisaa
2. Nilikuwa mtoro balaa mpaka Mkurugenzi aliandika barua kwenda Utumishi ya Mimi kuvuliwa madaraka na kupewa mwengine.
Yaani aliyekuwa kijana wangu wa chini sasa hivi ni boss wangu..!!!
3. Kuona hii ajira siipendi Tena, nikaona nitafute uhamisho, changamoto sasa, Mkurugenzi kagoma kabisaa kusaini barua zangu za kuniruhusu nikatafute post kwengine.
Anasemaga "bado nakuhitaji sanaa na siwezi kukuruhusu uondoke"
4. Nakiri; kunivua madaraka hata sijamlaumu, kiukweli kabisa nimekuwa mtoro balaa, siipendi Kazi Tena (kwasasa napenda sanaa biashara yangu na wanangu).
5. Yaani kazini naweza pitisha wiki sijasaini daftari la mahudhurio maana naingia saa 3 au 4 asubuhi na "ole wako uniulize lolote juu ya hilo..!!""
6. Yaani kwasasa siipendi Tena hii halmashauri, siipendi Tena hii Kazi (niliyokuwa naiwaza kuifanya miaka hiyo), kifupi HII OFISI NA KAZI YA SERIKALI SIVIPENDI KABISAAA.
BIG PROBLEM.
Kuona nawaze kujiharibia future kazini nikaona nishirikishe wakubwa.
Hao wakubwa nao wamenipa ushauri ambao HATA SIJAUKUBALI.
Ninachonipa "Huu ukichaa wa kutopenda Kazi" ni kwamba NAHITAJI KUWA HURU.
Nahitaji kuwa kwenye biashara zangu masaa 24,
Nataka chochote kinachotokea kwenye biashara nikione, KIFUPI BIASHARA IMENIMEZAA HASAA yaani ROHONI na NAFSINI NAWAZA BIASHARA ZANGU.
Naweza kuwa ofisini kuanzia asubuhi mpaka jioni ila nikaishia ku-google na kusoma mambo ya biashara hiyo, nikaishia kupiga simu dukani na Kwa wateja badala nifanye Kazi za watu..!!!
Ushauri..
1. Shangazi yangu aliniambia "NIOE" halafu mke ndio asimamie halafu Mimi niendelee kupambana na ajira.
HUU USHAURI NILIGOMA KABISAAA
2. Boss mmoja, aliniambia nitafute uhamisho ili niwe karibu na biashara yangu.
Nikaona hili wazo ni sahihi, kwa maana biashara yangu ipo mkoa wa jirani na niliko.
Ila sasa tokea 2021 nianze harakati za kuhama basi Mkurugenzi kagoma kabisaaa kunisainia barua ya uhamisho ili nikatafute post kwengine (mkoa ilipo biashara yangu), hili swala LIMEFANYA NIMCHUKIE KABISA.
Nikawaza kuacha Kazi.
Nina watoto wawili mmoja darasa la 3 mwengine la 2.
Hawa watoto nawaelewa sanaa, nawasomesha Shule ada Mil 2.7 *2 (Mil 5.4, WANASOMA SHULE MOJA).
Wapo Dar kwa mama zao (kila mmoja na mama ake), ila tunawasiliana kila siku.
Nahitaji kuhama niende kwenye biashara zangu halafu niwavute wanangu ili niishi nao.
NAWAPENDA SANAA WANANGU.
Nawaza kuacha Kazi ili nikakomae na biashara yangu.
CONCLUSION.
Sina wazo la kuoa na wala sitaki kuoa, hivyo sihitaji kuwa na mtu wa kusimamia biashara sijui kunisaidia kulea.
Nikiangalia Kazini napata hela na biashara napata pesa.
Kwahiyo nipo dilema, nikisema niache Kazi Kuna pesa itapwaya tu kwenye maisha yangu, sasa naona kama duka litahelemewa na majukumu.
NIA YA KUACHA KAZI NINAYO, ILA SABABU SINA..!!!
Ukicheki nilisoma sanaa kwasababu ya hii Kazi ila SIIPENDI TENA.
Mpaka muda mwengine nawaza KWANINI SASA NALISOMA SANAAA HIVI?
Ushauri wenu na MSAADA WENU MUHIMU SANAA.
Asanteni.
#YNWA