Mimi na mzee wangu hatuko sawa, na sioni dalili ya kuja kuwa sawa tena

Wa
Waafrika hawana matatizo mengi ya kisaikolojia kama Wazungu wazungu ni waoga wa sheria tu ila wengi wana matatizo ya akili kuliko sisi.
 
Hayo ni mawazo yako..

Ila kuhusu ku cultivate positive relationship is what am working towards.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚huyo daktari anaapoanza project ya kumhudumia mgonjwa,atataka dhumuni la mogonjwa mwenyewe kwanza.
What if kwa mtu anayesema haoni haja ya kuwa awa tena?
 
Ukifika umri wa kua na familia ya mke na watoto,utagundua kua Baba yako hakukosea kitu bali yalikua ni malezi kwa manufaa yako wewe mwenyewe .
Nilitaka kuandika comment ya namna hii, kuna wakati wazee wetu tunawaelewa ila ni baadae sana, huenda baada ya kuwa na familia, au wao wakishatoweka dunia.

Kuwa baba sio kazi rahisi.
 
I think kwa mental stamina nilonayo na yote nilopitia... Nimesha vuka hayo yote mkuu. Nimesha fanya healing sana by 2023 nilikuwa soo healed. Kilichobaki ni repetition tu ya vile tayari nimesha anza kuvi embody.


So, niko salama salmini
 
Ukifika umri wa kua na familia ya mke na watoto,utagundua kua Baba yako hakukosea kitu bali yalikua ni malezi kwa manufaa yako wewe mwenyewe .
That’s what nilisamehe kila lililotokea mwanzo na kuanza maisha mapya ya furaha na watu wote,tuko pamoja na maisha yanaendelea.

NB:kila mtu ajue nafasi yake tu.

de Gunner samehe,usamehewe buddy no one is perfect.
 
I'm trying my best mkuu
Ukishazoea kitu inakuwa ngumu sana kuacha... Hata misamiati ya kiswahili huwa haiji sana sana... Nimeshazoea kingereza kwa sababu ndo nakitumia sana

Nimekupata mkuu
 
Pole sana. Naelewa kwa kiasi fulani maisha uliyopitia, na bahati mbaya watu wengi wamepitia hali kama hiyo. Kwa wale ambao hawajawahi kuona madhara yake, mfano mzuri ni maisha ya Michael Jackson na baba yake, Joe Jackson.

Joe aliamini kwamba ukali, vipigo na maneno makali vitamjenga mwanawe na kumfanya awe bora. Lakini kwa upande mwingine, malezi hayo yalimwachia Michael majeraha makubwa ya kisaikolojia na kumbukumbu ambazo ziliendelea kumfuata hata alipokuwa mtu mzima. Hapo ndipo tunapojifunza kwamba si kila kitu mzazi anachokiita β€œmalezi” mtoto anakiona hivyo; wakati mwingine mtoto anakiona kama mateso.

Na hili ni jambo muhimu sana ambalo wazazi na walezi tunapaswa kulielewa: mtoto akiumizwa sana na mtu aliyepaswa kuwa sehemu yake salama, maumivu hayo yanaweza kumfanya ajitenge hata akiwa mtu mzima. Anaweza kufikia hatua ya kutotamani kurudi nyumbani, kutotaka kukutana na familia au hata kutotaka chochote alichorithishwa, kwa sababu kila anapokanyaga pale anakumbuka yale aliyopitia.

Ninasema hivi kutokana na uzoefu wangu binafsi. Baba yangu alifariki miaka 10 iliyopita, lakini majeraha ya kisaikolojia aliyoniachia yamekuwa makubwa kiasi kwamba sijawahi kujisikia kugeuka tena nyumbani. Hata baada ya yeye kufariki, sikuhisi kwamba kifo chake kilitosha kufuta yale yaliyopita. Niliwaambia ndugu zangu wazi kwamba kuhusu urithi wake, sitaki chochote; wagawane wao, mimi mniondoe. Si kwa sababu sina thamani ya vitu hivyo, bali kwa sababu kuna wakati amani ya moyo ina thamani kubwa kuliko mali.

Ndiyo maana huwa nawaambia wazazi na walezi: waacheni watoto waishi utoto wao. Msiwapokonye utoto wao kwa kisingizio cha β€œtunawajenga.” Mtoto anahitaji nidhamu, lakini nidhamu si sawa na kumdhalilisha, kumtukana au kumpiga bila mipaka.

Mtoto pia anahitaji kukosolewa, lakini akosolewe kwa heshima. Mfundishe kosa lake, mpe mipaka, msimamie, lakini usimvunje utu wake. Usimfanye mtoto aogope uwepo wako kiasi kwamba akue akitamani siku moja tu aondoke nyumbani na asirudi tena.

Kuna tofauti kubwa kati ya kumlea mtoto kwa ukali na kumuumiza mtoto. Na wakati mwingine tunatambua tofauti hiyo tukiwa tumechelewa.

Wazazi, watoto hawahitaji tu chakula, shule na mavazi. Wanahitaji pia usalama wa kihisia, upendo, kusikilizwa na kuheshimiwa. Utoto unapita mara moja. Usimnyang’anye mtoto utoto wake halafu miaka 20 au 30 baadaye ujiulize kwa nini hataki tena kuwa karibu na wewe.

Mlee mtoto kwa nidhamu, lakini usimlee kwa hofu. Mjenge, usimvunje.
 
πŸ™πŸ™πŸ™
 
Will do
Nashukuru mkuu
 
Kitendo cha kuendelea kukumbuka kua sijui Baba yako alikua mkali kwenu au kukumbuka mabaya yake,kina ashiria kua maisha yamekupiga so far,ungekua na good life usingekumbuka hayo,

Ndio maana kwenye ule uzi wako nilikwambia kua Get a life and you'll be better coz nilishaona tatizo lako,ila wewe ni kiumbe usie shaurika.
 
Actually my life is alot better... Sio kama kipindi naishi naye, financially... Am making a quite decent money.. Siwezi fika hata robo ya mshua. Ila am so good in terms of both aspects of life.. Naweza kuendesha maisha yangu vizuri tu... I see a bright future ahead kwa mipango niliyo nayo

So emotionally, kuishi home ilikuwa even worse.. Ndo maana I feel good in being this way, sioni haja ya kutaka kuvuka stage za mafanikio nitafika tu
 
Kashasaidika mpaka sasa na wala hatuogopani. Mimi nikiwa sipo watoto ndio wananitafuta nirudi so hawaniogopi kwa namna yoyote ila discipline wanayo. Bila kuwanyoosha tutawapa walimwengu adhabu ya KUWALEA.

Kwa wewe umri wako ulipofikia ni muda wa wewe kuanza ku deal na mindset yako. Umri ulionao sio wa kulaumu malezi ya wazazi ni kuendelea kujidekeza. A man must stand strong.

TAfuta ushauri sehemu mbalimbali kama hv stay POSITIVE tiba inaanza na wewe otherwise you will transfer hayo mambo kwa wanao.

Mzee ametimiza wajibu wake na mpaka sasa humdai mengine ni wewe KUJIONGEZA na kurudisha hali ya kawaida maisha yaendelee.

Do that before it is too late...

Just simple question. Wewe ni wangapi kwenu na mpo wangapi? How old is the older one na mdogo ana umri gani?
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£πŸ€£
Kwa namna unavyoandika tu,inaonesha kuwa mzee asingekukazia tungeshakupoteza.Mara mom,mara dad,viingereza vingiii.Tumia lugha moja utaeleweka.Mzee wqko ni jembe,hapa namlaumu mama yako kwa sababu hata hizi chuki dhidi ya mzee inaonekana mama anazichochea.POLE SANA JUNIOR MKUBWA
 
I understand mkuu.
Futhuer questions nitazidi kufanya isiwe na privacy..

Ila I get your point πŸ™
 
Sijaelewa kitu naona vingereza tu.

Kwani ulitakaje? Ulitaka upakwe mafuta kisogoni?

Binti yangu Lamomy naomba unieleweshe hii hoja ya huyu GEN Z.
 
Hayo ni mawazo yako. Hujui kitu kuhusu my mom.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…