Mimi na mzee wangu hatuko sawa, na sioni dalili ya kuja kuwa sawa tena

Wa

Waafrika hawana matatizo mengi ya kisaikolojia kama Wazungu wazungu ni waoga wa sheria tu ila wengi wana matatizo ya akili kuliko sisi.
Mkuu, waafrika matatizo ya kisaikolojia tunayo sana tu ila ni kwamba hatuna ufahamu wa kutosha na tunachukulia kawaida. Mfano mzuri wa tatizo la kisaikolojia tulilonalo ni uoga kupitiliza, sisi ni waoga mnoo tena hadi kwenye kutetea haki zetu, mzungu mtoto mdogo anaweza kushiriki maandamano au mgomo bila hofu, kitu ambacho sisi hatuna ,tukionewa tunachutama tuonewe zaidi.Pia tunawaabudu watu wengine ambao sio waafrika na kuwaona miungu,yaani mzungu akienda ofisini wahudumu wanamjali kuliko wanavyojali mwafrika mwenzao,hilo ni tatizo la kisaikolojia tayari.
Mifano ipo mingiii
 
Umemaliza yote mkuu, yaani unakuta mzazi anamuita mwanae pumbavu kisa tu kafanya kosa ambalo kwa mtoto ni kawaida. Hivi inakuwaje mtoto wako mwenyewe ghafla awe pumbavu? Mi sielewi wazazi wanaotukana watoto. Mtoto akikosea, atajiwe kosa lake,hata kama kwa sauti ya ukali kidogo ila aambiwe kosa lake,aadhibiwe mfano fimbo kadhaa na akatazwe sana asirudie. Lakini kumtukana matusi aisee hapana aisee,mwanangu nimzae halafu nimbadili jina aanze kuwa pumbavu, mjinga,etc. NO NO NEVER.
 
Sio waoga wa sheria ila wanaheshimu sheria, wanaishi kwa mifumo na wanafuata mpangilio.

Sisi ambao mnasema "tumelelewa vizuri" Lakini vitu vidogo hatuwezi inakuwaje
Yaani mkuu, tunaona tuna malezi mazuri lakini tunazalisha watu wanaokuja kukojoa na kutupa taka barabarani,tunazalisha mafisadi, wapenda rushwa etc. Sio kwamba wazungu wamekamilika hapana,ila malezi yetu bado yana mapungufu mengi hatupaswi kujisifu, tunapaswa kujiboresha.
 
Na hayo matusi huwa yanakuwa yanamuumiza kuliko hata kosa lenyewe la kibinadamu.
 

Binadamu pekee atakayefurahi wewe unapopata mafanikio au unapokuwa bora zaidi yake ni baba na mama yako pekee.

Ukilikubali hilo, utakubali pia kwamba katika mchakato wa kukufanya uwe bora, kuna kukosea pia kama binadamu, na hapo ndipo utakaposamehe na kusahau na kuendelea kuishi kwa furaha, amani na upendo.
 
Kabisaa mkuu, fimbo zinasahaulika ila maneno makali hayaondoki moyoni.
Baada ya kujua how impactful maneno yalivyo... Huwa siyatumii kabisa kuondoa ukakasi..

People forget what you did, but remember how you made them feel
 
Nashukuru kwa maneno ya hekima mkuu🙏
 
Sio waoga wa sheria ila wanaheshimu sheria, wanaishi kwa mifumo na wanafuata mpangilio.

Sisi ambao mnasema "tumelelewa vizuri" Lakini vitu vidogo hatuwezi inakuwaje
Wazungu wameshitakiana sana kwa mambo mengi ya kushangaza ndiyo maana wanaogopa sana sheria.
Huo uongo kwa muda mrefu umejengq hiyo culture ya kuogopana kupita kiasi.
Wazungu wanashitakiana hata kwa kumgusa kwa bahati mbaya.

Sisi bado hatujawa wengi kwenye small settlements ndiyo maana wengi tunaishi wildly kiasi fulani.
 
Kwanza yote uliyoeleza hayareflect matatizo ya akili wala kisaikolojia.

Hayo mengi yamejengwa katika tamaduni tu za waafrica with time yataisha na kujenga jamii tofauti kabisa.
 
Hapo kwa kumgusa mtu hapa Bongo mwanaume anamshika mwanamke hovyoo na hashtakiwi popote,ukiwa wa kike hii inakera sanaa.
 
Kwanza yote uliyoeleza hayareflect matatizo ya akili wala kisaikolojia.

Hayo mengi yamejengwa katika tamaduni tu za waafrica with time yataisha na kujenga jamii tofauti kabisa.
Uoga ni tatizo la kisaikolojia, utamaduni unaweza kuwa chanzo, sikatai. Kila kiumbe kimewekewa hali fulani ya kutaka kupambana pale kinapoona hatari,pale ambapo hiyo hali ya kutaka kupambana inaondoka ilihali uko hatarini ni tatizo la kisaikolojia hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…