"Jambazi ni mwanaume inabidi apambane na mwanaume mwenzake"
Hapana mi nasema huo ni ubaguzi wa kijinsia.
Mali mbona ni za mwanaume lakini tukiachana share inakatwa 50/50?
Mwanamke kupambana na jambazi wa kiume sio mwiko unaohusiana na jukumu la kimaumbile.
Hata feminism huwa haiwataji nyinyi kama watu dhaifu. Unawaangusha wenzio wanaokuangalia wewe kama mfano.
Feminism inasisitiza ujasiri kwa mwanamke dhidi ya mwanaume, feminism inasisitiza kuondoa mfumo dume.
Mfumo dume ni pamoja na dhana ya mume kama kichwa cha familia, kichwa cha familia ni pamoja na kuwa mlinzi kuhakikisha usalama wa familia
Kwenye mfumo dume ni wajibu wa mwanaume kumuacha mke ndani kisha yeye kutoka nje kwenda kupambana na jambazi.
Feminism imekuja kuondoa hiyo kingdom ya mwanaume na kumpa miliki mwanamke.
Maana yake wewe ndio unatakiwa utoke mbele u prove kwamba ni kweli mnao uwezo wa kusimamia majukumu ya mwaume.
Sasa wewe unaogopa
Halafu unabidi ujue kuwa matokeo ya mwisho (kufeli) sio jambo la msingi.
Yani kupigwa au kuzidiwa nguvu na jambazi sio kitu kinacho matter, kinacho matter ni ule uthubutu (ujasiri)
Maana yake hata mwanaume pia anaweza akapigwa na huyo jambazi kwa hiyo hoja ya kusema kwamba hutaki kutangulia mbele kwasababu maumbile sioni kama ni utetezi wenye mashiko.
Maana.
Hata nyinyi wanawake mbona huwa tunawaoma mkiwa mnapigana?
Kwenye huo ugomvi kwani ni mara zote umekuwa ukishinda?
Sometimes mnapigana wenyewe kwa wenyewe na sometimes mnajitutumua kupigana hadi na waume zenu kisa hiyo spirit ya feminism kuona kuwa ndani ya nyumba wote mna haki sawa.
Sasa linapokuja swala la kukabiliana na jambazi kwanini usitangulie mbele na kuithibitishia dunia kuwa mwanamke sio kiumbe dhaifu bali ni mkakamavu?
Mkuu unaposema "mali mbona ni za mwanaume ila mkiachana zinakatwa 50/50" unamaanisha nini, je wakati wa ndoa yenu ulikuwa unamsaidia kufanya majukumu ya nyumbani ikiwemo kulea watoto tangu wakiwa wachanga, na je alikuwa hakupi ile heshima na utii kama mwanaume au hayo hayawi considered
Na hata hivyo mbona wapo wanawake wengi tu wanaopambana na wanaume katika mazingira tofauti tofauti na wanashinda, nilichogundua wanawake wengi bado wanasita kuitumia hiyo 50/50 kwa asilimia mia kwa sababu wanaume wengi bado mnataka mfumo dume, siku mkiachana kabisa na mfumo dume basi hata wanawake nao watakubali kufanya hayo mnayotaka wafanye bila hiyana
Na ukizingatia siku hizi wanawake wengi tu wanafanya kazi ngumu mnazoziita za kiume kuna hadi makomandoo wanawake kwenye majeshi ya nchi mbalimbali, ila ninyi hadi leo bado mnakomaa kwamba majukumu ya nyumbani ni ya mwanamke na kwamba bado mwanaume anatakiwa amtawale mwanamke, sasa kwa mitazamo hiyo wanawake wanaona kama mnataka kuwatapeli yani eti wakubali majukumu sawa ndio muwape haki sawa
Lakini kumbe shida yenu mnataka wafanye majukumu mengi zaidi huku hiyo haki sawa yenyewe mnasuasua kuwapa na mnaitafutia visingizio vingi, na kama nilivyosema hii haki sawa kwa asilimia kubwa ililenga zile day to day activities sasa mambo ya kupigana vita na kupambana na majambazi siyo day to day activities kwenye individual life, kuna wanaume wengi tangu wanazaliwa hadi wanakufa wazee hawajawahi kupigana vita au kupambana na majambazi kabisa
So hicho siyo kigezo cha kuzuia wanawake wasidai haki sawa hizo ni uncertainties tu kwenye daily individual life, kwa sababu hata wanaume ambao hawajawahi kukutana na hayo masaibu (ambao ndio wengi kuliko waliowahi kukutana nayo) nao watajifichia kwenye hicho kichaka, na kingine wengi mnapotosha feminism maana yake siyo mwanamke amtawale mwanaume bali kusiwe na wa kumtawala mwenzie kila mmoja ajitawale mwenyewe