Mimi naona dunia iachane na mfumo dume na rasmi 50/50 ishike hatamu

Huwezi kuhalalisha jambo kwa kutumia makosa. Wanaume tumeambiwa tuwapende wanawake zetu. Kwa hiyo hao wanaume walikosea.

Kama tukizingatia kumsikiliza Mungu anachotuelekeza kuhusu mwanaume na mwanamke masuala kama mfumo dume na mwanamke kuwa wajeuri hayata tokea.

Mungu ametoa mwongozo mzuri ila sisi binadamu ni wakaidi. Je, hiyo 50/50 imewahi kutatua changamoto? Unaweza kusema ndio kwa ujeuri lakini kimsingi ndio kwanza matatizo yamezidi kuongezeka na kuathiri vizazi na vizazi.

Haya tunayoyaona leo watu kutokuwa na maadili ni matokeo ya 50/50. Ili tuweze kutatua haya turejee kwenye maandiko na tufuate anachokisema Mungu.

Tukiweka akili za kibinadamu kwa kujiona tumeelimika sana lazima tuangukie pua. Maana kwa sasa watu wanaongoza kwa kumkataa Mungu ni wasomi. Nimeshuhudia watu kadhaa ambao ni wasomi wenye shahada na kuendelea wakiamini Mungu hayupo!, hakika ni harari kweli! Mungu atusamehe na atusaidie.
 
Mungu hayupo ndio , nilishatoka huko kuishi kwa kufuata maandiko na hadithi za kutunga , kama unampenda mke wako mpka uambiwe unafeli sana mkuu , ila nashukuru kwa mchango wako na sitaki ubishi kutoka kwako wa uwepo wa Mungu na hauna uthibitisho🙏🙏
 
Majukumu ya wanaume ndio kama yapi ?
 
Kutokana na hili usitegemee changamoto zitaisha.
 
Pia kumkataa Mungu ni sawa na kuzuia kisicho zuilika, Mungu ndiye aliyeumba vyote unavyoona na usivyo ona. Ndio maana nikaweka neno automatic lazima uishi katika mstari ambao yeye Mungu ametuagiza.

Shetani alijifanya mwamba ona kilichomkuta, eti na sisi binadamu tunajitutumua kuwa hakuna Mungu!? Wewe sio wa kwanza wala sio wa mwisho kumkataa Mungu ila utakuja kuelewa baadaye naomba uje uelewe kabla hujachelewa.

Na suala la kumjua Mungu ni lazima wala sio uamuzi (automatic). Mungu atusamehe na atusaidie.
 
Umehubiri tu na kutoa hisia zako kwa kile ulichoaminishwa toka ukiwa mtoto , kitendo cha watu kupinga uwepo wake ni uthibitisho tosha kwamba hayupo , huna uthibitisho kaa kimya ,kuamini ni haki yako , ukileta habari za kuaminisha wengne lazima upigwe.
 
Siwezi kuwa kimya kwa jambo ambalo ni la kweli na halisi. Turudi kwenye mada. Mungu ametoa muongozo kwa mwanaume na mwanamke je, tumeishi katika maagizo yake? Bila kufuata miongozo wake ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

50/50 haitakuja kusimama kamwe kwa sababu asili ya binadamu imetokana na Mungu hivyo narudia tena "automatic" lazima ufuate alicho sema Mungu la sivyo ni kazi bure tutaangukia pua kama ilivyo sasa. Ndoa nyingi hazidumu, watoto wa mitaani, mashoga, ulevi uliokithiri, wizi, ufisadi, n.k.

Huwezi kutegemea akili yako binadamu bila kumuhusisha Mungu. Lazima utafeli kama ilivyo sasa. Usiwe kiburi.
 
Mkuu kama hamtaki 50 50 basi hudumieni wake zenu 100%, na siku mkiachana gawaneni mali pasu kwa pasu, simple tu
haina noma ila kwenye mali labda tulizochuma wote, kama alinikuta nazo BIG NOOOOOO
 
Mkuu unaposema "mali mbona ni za mwanaume ila mkiachana zinakatwa 50/50" unamaanisha nini, je wakati wa ndoa yenu ulikuwa unamsaidia kufanya majukumu ya nyumbani ikiwemo kulea watoto tangu wakiwa wachanga, na je alikuwa hakupi ile heshima na utii kama mwanaume au hayo hayawi considered

Na hata hivyo mbona wapo wanawake wengi tu wanaopambana na wanaume katika mazingira tofauti tofauti na wanashinda, nilichogundua wanawake wengi bado wanasita kuitumia hiyo 50/50 kwa asilimia mia kwa sababu wanaume wengi bado mnataka mfumo dume, siku mkiachana kabisa na mfumo dume basi hata wanawake nao watakubali kufanya hayo mnayotaka wafanye bila hiyana

Na ukizingatia siku hizi wanawake wengi tu wanafanya kazi ngumu mnazoziita za kiume kuna hadi makomandoo wanawake kwenye majeshi ya nchi mbalimbali, ila ninyi hadi leo bado mnakomaa kwamba majukumu ya nyumbani ni ya mwanamke na kwamba bado mwanaume anatakiwa amtawale mwanamke, sasa kwa mitazamo hiyo wanawake wanaona kama mnataka kuwatapeli yani eti wakubali majukumu sawa ndio muwape haki sawa

Lakini kumbe shida yenu mnataka wafanye majukumu mengi zaidi huku hiyo haki sawa yenyewe mnasuasua kuwapa na mnaitafutia visingizio vingi, na kama nilivyosema hii haki sawa kwa asilimia kubwa ililenga zile day to day activities sasa mambo ya kupigana vita na kupambana na majambazi siyo day to day activities kwenye individual life, kuna wanaume wengi tangu wanazaliwa hadi wanakufa wazee hawajawahi kupigana vita au kupambana na majambazi kabisa

So hicho siyo kigezo cha kuzuia wanawake wasidai haki sawa hizo ni uncertainties tu kwenye daily individual life, kwa sababu hata wanaume ambao hawajawahi kukutana na hayo masaibu (ambao ndio wengi kuliko waliowahi kukutana nayo) nao watajifichia kwenye hicho kichaka, na kingine wengi mnapotosha feminism maana yake siyo mwanamke amtawale mwanaume bali kusiwe na wa kumtawala mwenzie kila mmoja ajitawale mwenyewe
 
Vipi na lile andiko la mwanaume kula kwa jasho nalo umeliona au limepotea ghafla kwenye biblia, sijaona sehemu mungu alipomuambia mwanamke ale kwa jasho lake, hudumia mwanamke ndio umtawale na ndio mada yangu inachohusu
 

Lakini kwenye wodi zote za vichaa huwezi kuwakuta magenius, nimekuambia hivi taja hizo nchi zinazoongozwa na wanawake ambazo zipo kwenye hasara kubwa unaniletea habari za magenius hivi mzima kweli wewe, halafu nikakuambia kwenye nchi kama Tanzania hao wanaume ambao wameongoza kwa miaka 60 tangu nchi imepata uhuru wamefanya lipi la maana ikiwa hadi leo huduma muhimu ni tatizo huna cha maana ulichojibu zaidi ya pumba tu hebu ficha ujinga wako basi
 
Sasa unadhani wanawake walikuwa wanapenda kufanya hayo au walikuwa wanafanya sababu hawakuwa na sauti ujue siyo kisa tu babu zetu walifanya hayo basi maana yake ni sahihi, sababu hiyo zamani hata ukeketaji ni babu zetu ndio walikuwa wanalazimisha wanawake wakeketwe kwa maslahi yao ila si kwamba bibi zetu walikuwa wanapenda na si kwamba ukeketaji ni mzuri, kwahiyo hiyo siyo justification ya wanawake kuendelea kuwa watumwa kwa wanaume eti kisa tu zamani kuna vizazi viliishi hayo maisha
 
Hili nakubadliana nalo asilimia 100 wala sipingi, nmejaribu kuelezea tu kwa sababu hata sasa hakuna baba anatamani mtoto wake wakike aolewe na mwanaume mnyanyasaji na mwenye maono ya kifedhulu dhidi ya wanawake

Ukiwa kijana mdogo usie na mtoto au usie na mapenzi ya kweli na watoto wako unaweza changia chochote ili mradi tu kujiponya hisia zako .
 
Kama wote mnahusiana na mnapendana na mna mahitaji sawa ya kihisia kwanini wanaume ndio mnalihitaji sana hilo tendo na mko tayari kuhonga chochote kilicho ndani ya uwezo wenu ili tu mlipate ilihali kwa wanawake haiko hivyo, na je kwanini baada ya kuwa kwenye hayo mahusiano mkishaachana matusi na lawama huenda kwa wanawake kuwa hawajitunzi na hawajiheshimu ndio maana wanaachwa huku wanaume wakisifiwa, na je kwanini kwenye mahusiano mnapozini mwanamke ndio huitwa malaya kwa kuzini bila ya ndoa huku mwanaume akionekana rijali
 
Sawa hatujakataa hilo lakini huo utawala unakuja pamoja na majukumu juu ya hao wanawake, uzi wangu unasema kama unataka kumtawala mwanamke basi ni lazima umhudumie bila kutaka naye akufanyie hivyo, mkishaanza kutaka kusaidiwa majukumu yenu na wanawake hapo ndipo mfumo dume unapokosa maana na kuanza kupingwa
 
Si ndio na mimi nawashangaa yani hawa wanachoshindwa kuelewa ni kwamba sisi hatupingi mfumo dume, kama wanataka huo mfumo dume basi wakubaliane na majukumu yanayoambatana na mfumo dume, siyo mwanaume anataka heshima na mamlaka tu ila majukumu hayataki
 
Mkuu hakuna jipya chini ya jua maovu yote yalianza tangu kipindi cha agano la kale, kipindi ambacho mfumo dume ulikuwa umeshika hatamu na feminism ilikuwa haina hata dalili, au wewe unaweza ukaniambia ni maovu gani ambayo hayakuwepo enzi hizo na je mfumo dume umefanya nini kuzuia maovu yaliyokuwepo
 
Lakini kwa mfano kama wewe mkuu huwa unasema unakataa ndoa kwa sababu wanawake wanafuata pesa na mali kwenye ndoa, maana yake ni kwamba unataka wanawake nao wajitafutie pesa na mali zao wasitegemee za mwanaume si ndio, sasa nakuuliza je unaona ni sahihi wewe kutaka mfumo dume kumtawala mwanamke ikiwa hutaki kutekeleza majukumu yako juu ya huyo mwanamke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…